Sehemu ya tatu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano - Haki ya usawa wa binadamu
Hapa Tanzania kumejengwa ubaguzi kwa misingi ya udini ambao umeenea katika maeneo yote muhimu ya uendeshaji wa nchi, na ubaguzi wenyewe unafanywa dhidi ya Waislamu.
Katiba iliyopo inakataza wazi wazi kufanya ubaguzi ama kwa mtu au kwa kikundi cha watu, kwa misingi ya dini, kabila, unakotoka au jinsia. Tazama vifungu vifuatavyo: Usawa mbele ya sheria ya 1984 Na. 15 Ib.6 sheria Na. 4 ya 1992 Ib.8. Katika hali halisi ubaguzi unafanyika bila kificho kama inavyodhihirika katika uteuzi wa Tume mbalimbali, nafasi za masomo, ajira na katika nafasi za uongozi.
Kwa misingi hiyo tunapendekeza marekebisho yafuatayo:
(a) Iwe ni marufuku kwa mamlaka, tume au chombo chochote kinachotekeleza madaraka yake chini ya sheria kuwa na wajumbe au watendaji wake ambao wote ni wa dini, kabila au jinsia moja. Kila mamlaka, chombo au tume lazima ionyeshe uwiano uliopo katika jamii.
(b) Iwepo haki ya mtu, kikundi cha watu au
jumuiya kuzuia kupitia mahakama tukio lolote la kibaguzi la dhahiri au
kwa taathira au kuzuia uteuzi wa kiongozi yeyote mwenye sifa za ubaguzi.
(a) Kuwepo kwa serikali tatu tutaondoa dhana ya kumezwa kwa nchi ya Zanzibar na kuleta haki ya kujitawala kwa nchi ya Tanganyika.
(b) Kuwepo kwa serikali tatu kutatuwezesha kupatikana kwa Muungano imara:
(i)Kila serikali itajishughulisha na madaraka maalumu iliyopewa bila ya kuingiliana na madaraka ya Jamhuri au kinyume cha hivyo. Serikali ya Jamhuri itakuwa na maeneo maalum ya kushughulikia kwa niaba ya Tanganyika na Zanzibar.
(ii) Kwa mujibu wa i. hapo juu, serikali ya
Muungano itakuwa na gharama ndogo za kujiendesha.
(a) Katika nafasi ya kisiasa, uteuzi wa Waziri Mkuu, Mawaziri na Manaibu Waziri uthibitishwe na Bunge ili kuhakikisha kukubalika kwa wateuliwa hao na wawakilishi wa wananchi.
(b) Katika nafasi ya Mahakama, uteuzi wa Jaji Mkuu, Majaji wa Mahakama Kuu na Rufaa uthibitishwe na Bunge ili kukuza uhuru wa mahakama.
(c) Katika nafasi za watendaji waandamizi serikalini, uteuzi ufanywe na Tume Ajiri kwa njia ya uwazi kufuatana na kanuni za upandaji wa madaraka kazini.
(d) Madaraka ya kutangaza hali ya hatari yabaki
kwa Rais, lakini baadaye yathibitishwe na Bunge.
Uchaguzi wa Rais lazima uthibitishwe na mahakama,
lakini mahakama iwe na haki ya kuhoji ikiwa dosari za wazi zimejitokeza
katika kusimamia kuendesha na kutoa matokeo ya uchaguzi huo.
2. Utaratibu wa uwiano wa wingi wa kura utumike katika kugawa viti maalum kama vile viti vya wanawake.
3. Kusiwepo na Wabunge wateuliwa na Rais ili kuimarisha demokrasia.
4. Raia wapewe uwezo wa kumwondoa Mbunge wao
kabla ya kipindi cha miaka mitano ikiwa itadhihirika kuwa anajihusisha
na rushwa au kiwango chake cha utendaji wa kazi hakiridhishi watu wa jimbo
lake. Utaratibu huu utahimiza uwajibikaji wa Wabunge kwa wapiga kura wao.
Haki ya kumuondoa Mbunge ni ya wapira kura na siyo ya chama kilichompendekeza
Mbunge.
(a) Wakuu wa Mikoa na Wilaya wote watawajibika katika maslahi yote ya wapiga kura wao.
(b) Watalazimika kusimamia maendeleo ya mikoa na wilaya zao na kuleta mashndano ya kuitendaji kwa manufaa ya mikoa na wilaya.
(c) Masharti ya uteuzi wa nafasi hizo ni uwezo wa utekelezaji katika kuimarisha na kubuni maendeleo na wala sio kupendeza mbele ya chama chake au kwa Rais.
Sifa zilizotajwa hapo juu zitachochea maendeleo katika mikoa na wilaya na kwa hivyo nchi nzima kwa ujumla.
Sala la kuleta ubaguzi kwa kupigiwa kura wakuu wa Mikoa na Wilaya halina uzito kwani chaguzi za Ubunge na Serikali za Mitaa ambazo ziko karibu na watu zinafanyika bila ya athari ya ukabila.
|
|