wazo binafsi
 
Dawa ni kurejea kwa Allah
 

Na Abubakar S. Marwillo

NINAPENDA kutoa mchango wangu kuhusu kichwa cha habari kilichochapishwa katika gazeti la ANNUUR Na. ISSN 0856-3856, Na. 189 la tarehe ya mwezi wa Dhulkada 1419 sawa na tarehe za Kirumi Februari 19-25, 1999. Kichwa cha habari kiliaandikwa: "Ulaji wa ‘Kiti moto’ hadharani, umoja wa kitaifa wafikia hatma yake, Wakristo wajitenga, ujirani mwema sasa basi".

Kwanza, ninaeleza masikitiko yangu makubwa kwa Mwenyekiti wa Tume ya Jiji Bwana Charles Keenja kwa agizo lake alilolitoa la kueneza na kuuza nyama ya nguruwe hadharani, ambayo siku hizi inatiwa ‘Kiti moto’. Agizo hli limesambazwa na vyombo vya habari, tumefahamishwa hivyo.

Si vibaya hata kidogo nikisema Bwana Charles Keenja amekosea kuchukua hatua na mazingira yake. Sheria hizi haziruhusu ufugaji wala uuzaji katika miji ambayo ina wakazi wengi wa jamii ya Waislamu. Wakoloni ndiyo waasisi wa sheria hizo na walifanya hivyo kwa lengo kuu la kuleta salama na amani katika jamii na kwa kiasi fulani kuonyesha heshima kwa Waislamu. Mpaka sasa sheria hizo bado hazijaondolewa wala kubadilishwa na kikao chochote cha Halmashauri ya Jiji wala miji. Hivyo agizo halitaweza kuwa juu ya sheria.

Wakati wa kuendesha Halmashauri ya Jiji au miji kutoa maagizo umekwisha. Wanasiasa wa nchi hii wanatuambia, kila siku iendayo kwa Mwenyezi Mungu, kuwa Tanzania nchi ya uwazi, sheria na utawala mzuri mara tu baada ya mabadiliko ya kisiasa na uchumi yaliyotokea duniani; baada ya siasa ya ukomonisti au ujamaa kuanguka na kufa. Charles Keenja anapingana na sifa za uwazi, sheria na utawala mzuri.

Si kweli hata kidogo kuwa umoja wa kitaifa upo. Rais wa kwanza wa Tanzania wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere alijitahidi kwa kutumia umoja wa kitaifa kwa kutumia falsafa ya ujamaa, fikra za Kirumi na Kigiriki. Wakati huo huo, kuwaacha wananchi wengi katika umasikini mkubwa na ujinga. Hivi unategemeaje wananchi wa namna hii kuwa na umoja wa kitaifa. Umasikini na ujinga unapokithiri katika jamii hizo. Jingine ni kwamba watu hivi sasa wanarejea kwenye itikadi zao ambazo wanaziona ni sahihi kuliko umoja wa kitaifa. Upo udhaifu mkubwa katika umoja wa kitaifa.

Fikra za watu haziwezi kujenga chochote cha kudumu na kuwafaa watu. Binadamu ni lazima afahamu fika uhusiano wake na mazingira yetu au dinia yetu; na uhusiano wake na Mwenyezi Mungu. Kinyume cha hivyo ni vurugu tupu na machafuko ya fikra.

Ili kuepuka vurugu na machafuko ya fikra katika dunia hii, kuna haja kubwa ya kuwaepuka watu kama akina Charles Keenja. Kuwaepuka tu hakutoshi hata kidogo. Mtume (s.a.w.) amefundisha nini hasa tunapoona jambo baya katika jamii yetu? Ametufundisha yafuatayo:

Kuondoa baya hilo kwa mikono yetu (nguvu, madaraka na kadhalika). Kusema dhidi ya baya hilo (kuandika, kufanya mihadhara na kuvitumia vyombo vya habari). Kuchukia dhidi ya baya hilo (lakini huu ni udhaifu mkubwa).

Napenda kutoa tahadhari kwa ndugu zangu Waislamu kuwa tusione nguruwe ni mbaya kwetu na mengine mabaya yanayochangiwa na Waislamu kuwa yanafaa kutegwa mgongo. Mabaya haya mengine ni mengi lakini nitalazimika kuandika moja tu linalohusu ulevi. Idadi kubwa ya Waislamu ni walevi wa kila siku.

Wenye maduka ya ulevi wanasema kuwa Waislamu ndiyo wanaochangia sehemu kubwa ya mapato yao yanayotokana na mauzo ya ulevi; na bila ya wao maduka ya pombe yengelifungwa. Ni hivi majuzi tu katika mwezi wa Ramadhani wenye maduka haya walilalamika kuwa mwezi huo uliwanyima fursa za biashara zao. Baadhi ya Waislamu wanajiepusha kunywa pombe mwezi wa Ramadhani. Baadaye hurejea katika uasi huo.

Pombe yoyote ile katika jamii ina hasara kubwa kuliko faida. Lakini kwa bahati mbaya watu wa leo wanaangalia manufaa kuliko hasara. Kwa mfano viwanda vya pombe vinachangia kiasi kikubwa cha kodi ya mapato serikalini kuliko viwanda vingine hapa nchini.

Mtume Muhammad (s.a.w.) amesema: "Mama wa mabaya yote ni ulevi/pombe". Maulamaa wa Kiislamu wamefafanua Hadith vizuri kabisa kwamba mtu akinywa ulevi/pombe basi inakuwa rahisi kwake kufanya uzinifu, inakuwa rahisi kwake kuuwa na inakuwa rahisi kwake kufanya mambo yote ya aibu. Pia pombe inaathiri sana akili na kwa ujumla afya ya mtu.

Haya yote sasa dhahiri katika jamii yetu. Msimamo wa jamii zetu hizi ni kuwa pombe ndiyo asili au urithi wa Tanzania. Msimamo huu ni ulaghai mtupu na pumbazo tu. Msingi wa ustawi wa jamii yoyote ni kuimarisha mema na kukataza mabaya. Lakini msingi huu ni kwa watu maalum wenye kuwa na imani ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kufuata kwa vitendo mafundisho yake Mtume wetu Muhammad (s.a.w.). Jamii hii ya Kiislamu; na wala siyo ile leo inaamini na kisha kesho inakufuru au inachanganya imani na kufru katika wakati mmoja.

Ni jambo la bahati mbaya sana kuona kuwa washirikina na watu waliopewa kitabu leo tumewafanya ndugu kiasi kwamba ule udugu wa Kiislamu tumeusahau au kuupuuza kabisa. Tunaimba mwimbo wa pamoja: "Utaifa kwanza na Uislamu pili". Hili litatuangamiza kwani watu tunaoshirikiana nao ni waovu. Mwenyezi Mungu alikwishaliweka wazi hili katika suratul Bayyinah aya ya 6: "Bila shaka wale waliokufuru miongoni mwa watu waliopewa kitabu na washirikina wataingia katika moto wa Jahanamu, wakae humo milele; nao ni waovu wa viumbe".

Ifahamike kuwa utaifa hauna ubora wowote mbele ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema katika sura ya 49 aya ya 13: "Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni kwa mwanamume na mwanamke. Na tumekufanyeni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika ahishimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye habari (za mambo yote).

Waislamu waliopita walikuwa wachache sana kiasi kwamba walistaajabisha dunia nzima. Madola makubwa mawili kwa wakati huo - Madola ya Persia (Ajemi) na Urumi yaliporomoka na Uislamu ukashika usukani wa uongozi wa dunia. Nini kilichowapa nguvu? Sababu ni kwamba walimwamini Mwenyezi Mungu, ambaye ni Mjuzi, na kisha wakaamua kinaga ubaga kubadili yale waliyokuwanayo kwenye nafsi. Hawakurudi tena kwenye ujahili. Qur’an ndiyo ilikuwa umbile lao pamoja na mafundisho ya Mtume wetu (s.a.w.).

Hivi leo ujahili unachanganywa na Uislamu, hapa ndipo makafiri wanapata sababu ya kimsingi kufanya wanavyotaka, kuturudisha kwenye ukafiri wao badala ya Uislamu wetu. Pia makafiri tunawatii kwa maamuzi yao yote wanayopitisha kwa jamii nzima hata kama maamuzi hayo yanaathari mbaya kama hili la kuruhusu ‘kiti moto’ kuliwa hadharani.

Mwenyezi Mungu anasema katika sura ya tatu aya ya 100 kuwa: "Enyi mlioamini! Mkiwatii baadhi ya wale waliopewa kitabu, watakurudisheni kuwa makafiri baada ya Uislamu wenu".

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameachwa peke yake; na mafundisho ya Mtume yamewekwa kando, Waislamu wamepoteza uongozi wa dunia hii. Sasa uongozi wa dunia hii umetwaliwa na nchi au watu wa Magharibi. Masuala ya Bosnia, Palestina, Lebanon, Algeria, Kosovo, Afghanistan na mengine mengi makubwa yanashughulikiwa na nchi za Magharibi huku Waislamu walio wengi wanayatazama kama ni masuala yasiyowahusu. Kwa hakika Waislamu tumeanguka.

Jamaludeen Afghani ambaye alikuwa mtangazaji maarufu wa Uislamu katika wakati wake uliopita, aliulizwa kwa nini Waislamu wamekuwa nyuma ya watu wa nchi za Magharibi. Alijibu tu kwamba Waislamu wamekuwa nyuma kwa sababu wameacha dini yao ambao watu wa Magharibi wako mbele kwa sababu nao wameacha dini yao. Jibu hili liliwachanganya sana. Jamaludeen Afghani aliliweka sawa kama hivi: "Uislamu una nguvu na kwa kuuacha, Waislamu wamekuwa nyuma. Ukristo hauna nguvu/umetuwama na ulipoachwa na watu wa Magharibi yamefanywa maendeleo.

Waislamu warejee kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.) ili tuweze kuitengeneza dunia yetu. Katika safari hii ndefu tujitakase kwa ajili ya maendeleo yetu na amani ambayo hivi sasa walimwengu wanaitafuta wka ‘udi na uvumba’ Tukifanya hvi tutashinda kwani sisi Waislamu ndiyo tunao mwongozo na sharia kwa manufaa ya ubinadamu. hii Qur’an ndiyo mwongozo wetu usiyokuwa na shaka yoyote ndani yake.wale waliopewa kitabu, watakurudisheni kuwa makafiri baada ya Uislamu wenu".

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameachwa peke yake; na mafundisho ya Mtume yamewekwa kando, Waislamu wamepoteza uongozi wa dunia hii. Sasa uongozi wa dunia hii umetwaliwa na nchi au watu wa Magharibi. Masuala ya Bosnia, Palestina, Lebanon, Algeria, Kosovo, Afghanistan na mengine mengi makubwa yanashughulikiwa na nchi za Magharibi huku Waislamu walio wengi wanayatazama kama ni masuala yasiyowahusu. Kwa hakika Waislamu tumeanguka.

Jamaludeen Afghani ambaye alikuwa mtangazaji maarufu wa Uislamu katika wakati wake uliopita, aliulizwa kwa nini Waislamu wamekuwa nyuma ya watu wa nchi za Magharibi. Alijibu tu kwamba Waislamu wamekuwa nyuma kwa sababu wameacha dini yao ambao watu wa Magharibi wako mbele kwa sababu nao wameacha dini yao. Jibu hili liliwachanganya sana. Jamaludeen Afghani aliliweka sawa kama hivi: "Uislamu una nguvu na kwa kuuacha, Waislamu wamekuwa nyuma. Ukristo hauna nguvu/umetuwama na ulipoachwa na watu wa Magharibi yamefanywa maendeleo.

Waislamu warejee kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.) ili tuweze kuitengeneza dunia yetu. Katika safari hii ndefu tujitakase kwa ajili ya maendeleo yetu na amani ambayo hivi sasa walimwengu wanaitafuta wka ‘udi na uvumba’ Tukifanya hvi tutashinda kwani sisi Waislamu ndiyo tunao mwongozo na sharia kwa manufaa ya ubinadamu. hii Qur’an ndiyo mwongozo wetu usiyokuwa na shaka yoyote ndani yake.

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook