RAIS Benjamin William Mkapa anakabiliwa na mtihani kuhusiana na malalamiko ya wananchi juu ya kudhulumiwa haki zao na kufanyiwa vitendo vya kinyama na mamlaka au vyombo vya Dola. Katika malalamiko ya hivi karibuni wananchi wa Yombo Vituka Lumo waliodai kuwakilisha familia 200 wamemlalamikia Mh. Rais kwamba wamebomolewa nyumba zao kinyume cha sheria na katika hali ya kudhalilishwa. Endelea.. |
KUTUMIA lugha ya kigeni katika uendeshaji wa kesi mahakamani ni uvunjaji wa haki za binadamu. Hayo yamesemwa na mwanasheria Dk.Abdallah Saffari alipokuwa akihojiwa na mmoja wa wataalamu wa lugha ya Kiswahili nchini Bwana Mohammed Mwinyi juu ya muswada wa kitabu chake "Sheria ya Mashitaka na Utetezi". Dk. Saffari amesema wakati umefika kwa wanasheria nchini kuondokana na taasubi (ung’ang’anizi) kwamba Kiswahili hakijitoshelezi kuweza kutumika katika masuala ya sheria. Endelea.. |
|
|