Mashairi
 
 

Wako wapi Wajahidi? (Ushauri)

Niondoe mashakani, Mola uliye Jabali,
Unijaze yako shani, nipate kutawakari,
Fahari isiwe fani, nisije kutahayari,
Kikong’ona songa mbele, Mjahidi tawaona.

Uliko huko nyumbani, Kikong’ona zingatia,
Morogoro mlimani, jihadi wakumbushia,
Mjahidi watamani, akilini  kuingia,
Kikong’ona songa mbele, Mjahidi tawaona.

Haki yako ya thamani, usikae kulalama,
Haki yako ithamini, uwe mfano nahoza,
Ukipita majumbani, vijana kuwaandaa,
Kikong’ona songa mbele, Mjahidi tawaona.

Watamka makusudi, jihadi kukumbushia,
Watokee mashahidi, haki kuipigania,
Haki ipate kurudi, dhulma kuiondoa,
Kikong’ona songa mbele, Wajahidi tawaona.

Kutokea mashahidi, yafaa maandalizi,
Kikong’ona ushahidi, hujitaji simulizi,
Kwa zile zako stadi, umepata ung’amuzi,
Kikong’ona songa mbele, Mjahidi tawaona.

Uwe nahodha jadidi, kufanya hii kazi,
Hutauliza shahidi, kwa hili jambo azizi,
Itashitadi jihadi, kwa ule wako ulinzi,
Kikong’ona songa mbele, Mjahidi tawaona.

Kusonga mbele sitaki, saba beti kituoni,
Kikong’ona uhaki, wasi wangu thamani,
Sitaki kukuzihaki, kwenye hii yako fani,
Kikong’ona songa mbele, Mjahidi tawaona.

Mlangano Mpunga Kawapa Wala,
Ubungo Islamic College of Education,
P.O. Box 55105,
DAR ES SALAAM
 

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook