Kitumbini watoa mazulia kwa Msikiti wa Ilola, Rukwa
 

Na Mwandishi Wetu

MSIKITI wa Kitumbini wa Jijini Dar es Salaam umetoa sadaqa ya mazulia kwa Msikiti wa Ilola ulioko tarafa ya Ilala wilayani Mpanda mkoani Rukwa.

Msaada huo wa mazulia umefuatia baada ya ukarabati wa Msikiti kukamilika hivi karibuni.

Akiongea katika hafla ya makabidhiano ya mazulia hayo, Mratibu wa shughuli za uimarishaji Uislamu huko Ilola, Bwana Ismaili Mwiga alisema kuwa msaada huo ni kichocheo cha umoja miongoni mwa Waislamu.

"Msaada toka pembe ya mashariki ya nchi (Dar es Salaam) hadi pembe ya kusini magharibi ya nchi (Rukwa) utaimarisha umoja wa Waislamu nchini kote", alisema Mratibu huyo.

Aidha, Bwana Mwiga ameishauri Misikiti mingine mikubwa kuiga mfano wa Kitumbini kusaidia Misikiti midogo hasa ile ya vijijini.

Bwana Mwiga amesema katika kuiga mfano wa Kitumbini wao wataiga kwa kuboresha Misikiti ya tarafa hiyo.

Msikiti wa Ilola ambao ni wa muda mrefu katika tarafa hiyo ulikarabatiwa kwa nguvu za wenyeji wa tarafa hiyo bila ya misaada kutoka kwa "wafadhili".

Wakati huo huo, Waislamu wa tarafa ya Ikola wameamua kufanyakazi bega kwa bega na wenzal wa kijiji cha Karema ambacho hakijawahi kuwa na Msikiti ili kujenga Msikiti kwa ajili ya Waislamu wa huko.

Hadi sasa wameshatengeneza matofali ya kuchoma kuwezesha ujenzi kuanza hivi karibuni.

Akielezea harakati hizi Khatibu wa Msikiti wa Ijumaa wa Ikola Bwana Haruna Mte alisema kuwa hivi sasa wanafanya kazi ya kuhamasisha Waislamu wote wa huko ili kujitolea kujiletea maendeleo yao wenyewe.

Tarafa ya Ikola iko kwenye ufukwe wa ziwa Tanganyika ambako kuna vijiji kadhaa vyenye Waislamu kama vile Ikola, Kalema, Kapala Msenga na vinginevyo.
 

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook