KATIBU wa Bakwata Mkoani Arusha Alhaj Major Mohammed Mollel amedai tuhuma anazovishwa na waumini hazina ukweli wowote. Aidha Bw. Mollel amesema wanaochochea jambo hili ni kikundi cha vijana ambacho huko nyuma kilishamwita Askofu na hata kumwita kafiri.
Akiongea na gazeti hili kwa njia ya simu tokea Arusha Alhaj Mollel hakutaka kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma dhidi yake bali alisisitiza kwamba wapo watu Arusha ambao kazi yao ni kumzulia na kumpaka matope.
Habari zaidi toka Arusha zimeeleza kwamba wafanya biashara waliokodishwa sehemu za biashara na makazi wamepangishwa kwa mikataba ya zaidi ya miaka 25 ambapo makusanyo ni zaidi ya shilingi milioni kumi na mbili kwa mwezi.
Kwa mujibu wa maelezo ya watu wanaolifuatilia suala hili wamedai kwamba kwa kipindi cha miezi 65 aliyokaa Bw.Mollel katika nafasi ya Ukatibu, ukitoa matumizi Msikiti Mkuu ungekuwa na akiba isiyopungua milioni 230,000,000/=.
Hata hivyo, watu hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe gazetini hawakuweza kutoa mchanganuo wa hesabu hiyo yapi mapato na yapi matumizi na ushahidi wake.
|
|