MADRASA
Ijue Madrasat Daarul-l-Uluumi ya mjini Dodoma

Na Abu Zubeir, Dodoma

AL-MADRASATI Daarul-l-Uluumi ipo katika eneo la Area ‘A’ Kata ya Chamwino mjini Dodoma. Madrasa hii ilianza mwaka 1986 ikiwa na wanafunzi 40 na kuwa na idadi ya walimu wanne kati ya 1989 - 1997. Na mwaka 1997 ilishikwa na na Ustadh Mustafa Rajab Shabani ambaye anaendelea na kutoa taaluma yake hadi sasa.

Muasisi wa Madrasa ni mzee Uwesu Omari Mikuli ambaye amejitolea sehemu ya jengo ya nyumba kwa kutoa chumba kimoja kwa ajili ya shughuli ya Madrasa.

Mzee Mikuli amefanya hivyo kwa kutafuta radhi za Allah (s.w.). Madrasa hiyo ambayo kwa sasa imefikia kuwa na wanafunzi 100 wakiwemo wasichana 40 na wavulana 60, ina idadi ya masomo manane yanayofundishwa.

Nayo ni Qur’an, Tawhiid, Hadith, Siira, Tajwid, Fiqh, Lugha na hifadhi ya Qur’an. Aidha, masomo hayo ni kwa wanafunzi wa miaka kati ya 10 - 17. Na kwa watu wazima kuanzia miaka 18 - 30 ambao idadi yao ni wanafunzi 10 wanasoma masomo ya Ahkami, Tajwid, Hadith, Fiqh, Lugha, Nahau na Swarfa.

Aidha, madrasa hii pia ina watoto yatima 10, watoto wa kike sita na wa kiuma wanne. Na utaratibu wa kuandikisha wanafunzi ni kutoa ada ya shilingi 500 tu; kwa muda wote wa mtoto atakapokuwa anasoma hapo, aidha, mwanafunzi awe na vifaa vyake mwenyewe kama juzuu, daftari n.k.

Maendeleo yaliyopatikana makubwa ni pamoja na watoto wengi kumaliza masahafu, kuelewa ibada zao kama kusali, hija, saum n.k.

Matatizo yaliyopo ni pamoja na mahudhurio hafifu katikati ya wiki kutokana na watoto wengi kuhudhuria masomo ya ziada (tuition), hivyo kuzifanya siku pekee za kusoma ni Jumamosi na Jumapili.

Mlezi wa madrasa hii mzee Mikuli anawaomba Waislamu kuchangia madrasa ambayo inazidi kupanuka na jengo la kusomea kuwa dogo sana.
 
 

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook