Dodoma wasema:
Damu ya Waislamu haitamwagika bure
 

Na Mwandishi Wetu

Damu ya Waislamu iliyomwagwa pale Mwembechai haitapotea bure. Wamesema kile kilichofanya damu yao imwagwe watakiendeleza kwa juhudi zao zote.

Wametoa kauli hiyo kufuatia ratiba ya mihadhara inayoendelea mkoani Dodoma ambapo watu kadhaa washasilimu.

Mihadhara hiyo ambayo imedumu kwa zaidi ya wiki moja inaendeshwa na vijana wa AL-MALLID chini ya uonozi wa Bw. Bilal N. Miromo.

ANNUUR imebahatika kupata baadhi ya majina ya watu waliosilimu ambao ni Bi. Salma (Happy Boniphace - Katoliki), Bi. Aisha (Agnes Thomas - Katoliki) na Bw. Salum (Joel Paul Masuka - Katoliki).

Wengine ni Farida Ntenga (Felister Ntenga - Katoliki) na Aisha Colnel (Joyce Colnel Chamanzi - Moravian).

Kufuatia mihadhara hiyo na watu kuanza kusilimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Viwandani katika Manispaa ya Dodoma aliandika barua kusimamisha mhadhara uliokuwa ukifanyika Masjid Qubaa kwa hoja kuwa hauna kibali cha Mkuu wa Wilaya.

Ni kutokana na tishio hilo, waumini na viongozi kadhaa walioongea na gazeti hili wameeleza kwamba katu hawatakubali damu ya Waislamu iliyomwagwa pale Mwembechai ipotee bure.

Viongozi hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe gazetini kwa hoja kwamba muhimu ni kazi kufanyika na wala sio majina yao; wamesema kwamba mihadhara itafanyika bila ya kutegemea kibali cha mtu maadhali hawavunji katiba wala sheria za nchi.

Wamesema kwamba chanzo cha kuuliwa Waislamu Mwembechai ni fitna za Maaskofu kwamba mihadhara inayowaita watu katika Uislamu ni kashfa.

"Kusita kufanya mihadhara itakuwa ni kukubali propaganda hiyo ya Maaskofu na hivyo kuhalalisha damu ya Waislamu iliyomwagwa", wamedai viongozi hao.

Kutoka Dodoma mjini, kundi hilo la AL MALLID lilitarajiwa kuelekea Mpwapwa.
 

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook