Na Kassim Bilo, Tanga
UTARATIBU wa Hijja ni tendo linalochukua muda wa siku tano (5) likianza mwezi wa 12 (Dhul-Hijja) kalenda ya Kiislamu ambapo itakuwa tarehe 26 au 27 Machi, 1999 hutegemea muandamo wa mwezi.
Kwa sehemu ya mwanzo ni utekelezaji wa mipango ya Masjid Al-Haram Msikiti Mtakatifu wa Makkah. Wakati wa Hija Mahujaji watakuwa wakikaa sehemu tatu tofauti, na kwa nyakati tofauti.
Siku ya tisa ya Dhul-Hijja, mahujaji watawasili kutoka Arafat, kwa njia mbalimbali, kama vile kutoka Minna na Mazdalifa, kwa kila kundi litafika kwa njia yake ya usafiri, wengine kwa ndege na wengine kwa mabasi na vyombo mbalimbali vya usafiri. Arafat ni umbali wa kilomita 15 kutoka Makkah.
Watapumzika kwa siku nzima pia pale watasikiliza hotuba kutoka kwa Msikiti wa Namira, na pia kushiriki kwa sala ya Adhuhuri, kuweko kwa Mahujaji katika mji wa Arafat ni lazima na muhimu katika tendo la Hijja, japo laonekana tendo dogo lakini Mtume Muhammad (s.a.w.) alihimiza tendo hili katika kauli yake.
Hotuba za Hijja ni hotuba za kusisimua zinazohusu binaadamu wote, ni vyema kwa mwanaadamu mwenye uwezo kwenda kuhiji japo mara moja katika uhai wake ili kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na pia awe na moyo wa ucha Mungu na pia kuweza kupata baraka za Allah (s.w.) kwani mtu anapokwenda kuhiji huweza kuziona sehemu takatifu ambazo zinawapa motisha walimwengu kwa kujifunza na kuona msimamo bora wa Kiislamu katika mataifa mbalimbali ya ulimwengu pamoja na kuwka udugu wa Kiislamu.
Jambo la kufurahisha katika tendo la Hijja ni kwamba Muislamu atakuwa na moyo wa kujua kwamba Waislamu wote ni ndugu bila kujali rangi zao wala makabila yao wote wakiwa na haki sawa na kumuabudu Allah (s.w.) kufuatana na muongozo ulioletwa na Mtume (s.a.w.).
Kauli ya Mtume (s.a.w.) inasema baada ya kumtukuza Mwenyezi Mungu pia inatakiwa uwafahamishe wengine juu ya Uislamu.
Kauli ya Mtume (s.a.w.) katika hotuba mojawapo ya Hijja:
"Enyi watu jueni ya kwamba nyinyi ni
waja walioumbwa na Mwenyezi Mungu na kwamba mali yako; ufalme wako hautambuliki
mbele ya Mwenyezi Mungu ila vitendo vyako vizuri ndivyo utakavyouliziwa
mbele wa MOLA wao.
|
|