MAKALA
 
Umoja wa walimwengu wote-2

Na Tahir Kajia

Sasa ni kauli gani hiyo ambayo ukiikurubia unakuwa dhalimu? Dhalimu unayeonywa usimkaribie ambaye Mwenyezi Mungu anatupigia mfano kwa kumuita "mti" ni yule atakayesema miongoni mwetu: "Mimi ni mungu (kiongozi au mfalme au Rais) badala Yake, (kwani) huyo ni dhalimu (21:29). Kwa tafsiri hii adhimu, tumeachwa hoi. Kwani wao Wazungu wamepotosha tafsiri wakisema kuukurubia uwongo wao ule ni kuzini Adamu na Hawa. Naye Allah kawafichua uwongo wao (2:35) kwani wao Adamu waliingia bustanini kama mume na mke.

Hivyo madhalimu ni watu wanaomtii binadamu mwenzao mungu waliomteua kuwa kiongozi wao. Na hapa nini tujue?

JUWA kwamba Berlin Conference awamu ya pili, mpango waliouita Uhuru; (1961) ulielekezwa kutufikisha katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu bila sisi kujua pale mwaka 1962 tulipomjaalia mweusi mwenzetu kuwa mungu (rais) (15:94-96). Na hapa ndipo maisha yetu yalipoanzia kuporomoka (22:31). Kwa ulaini sasa Rais huyu akaunda Baraza la Mawaziri (Idara za serikali) (27:48) lililolishughulikia dunia tu (7:51). Na kwa jina la Jamhuri akalisajili taifa letu jipya katika nyumba ya maangamizo - Umoja wa Mataifa - New York (14:28).

Kabla hatujaenda mbali, hebu tuangalie huyu Rais ni nani?

Manabii wa uwongo!

Visa vingi vimenukuliwa kwamba mwisho huko (akhri zamani), Manabii wa uwongo watakuwa kibao. Sisi tukawangojea wajie Misikitini na Makanisani! Kumbe la. Tayari wapo mijini na wameshikilia hatamu za uongozi bila sisi kujua. Kwani Nabii huletwa ili kuongoza (9:33)? Na leo viongozi wetu wa ngazi ya juu huitwa Rais?

Kumbuka ni Nabii Mussa (a.s.) aliyemteua ndugu yake Haruna kuwa Waziri (20:29-30). Hivyo Allah (s.w.) ndani ya buku hili (Qur'an), anatufundisha kuwa Mawaziri huteuliwa na Manabii. Ikiwa hivyo ndivyo, na leo tunao Mawaziri kibao ambao huteuliwa na Rais, juwa basi kuwa kumbe hawa Marais ndio Manabii lakini wa uwongo.

Na kweli Allah anataka kutuongoza katika njia iliyonyooka. Na wao Marais huzua njia zingine k.v.: Njia ya ujamaa, njia ya nyago n.k. na hivi sasa ulimwengu mzima - njia ya demokrasia. Je! Hujagundua kuwa katika njia hii ya demokrasia kukampeni na kumsimika Rais, gharama zote zilizotolewa na Umoja wa Mataifa? Kwa nini? Wanapata nini? Na pia gharama zote za kampeni za Wabunge? Sikia mambo yalivyo, Mola wetu Allah atujuze.

Neno Mzungu kamusi inafasiriwa kuwa ni "mbinu". Kwa hiyo ukisema Wazungu maana yake ni watu wenye mbinu. Sasa ni mbinu gani hii waliyoitumia kutegemea?

Ili tuukurubie ule mti tulioonywa (7:27), iliwachukua Wazungu miaka sabini na tano kupitia mashule kukata mahusiano ya malezi kati ya wazazi na watoto weusi. Watoto hawa wakawa wamefanywa kuchukia kila kilicho chao na waone kila kilicho cha Wazungu kuwa ndio ndicho.

Kwa hiyo wakaonyeshwa tupu zao (7:27) na kuingiwa mashakani (20:117). Hivyo mambo manne yakawasibu: Njaa (kujilisha) (20:118) na kuwa uchi (mavazi) (20:118). Na hapa zingatia ni kuwa uchi kimwili na kiroho. Na tatu yaliyowasibu ni kiu (kiu cha kinywaji na kiu cha kimaumbile) na nne joto (ukame) na sasa wanachoita Global heating. (20:119).

Kumbe mambo manne haya ndipo waungu wenye akili walipojengea mradi wao pale walipo jenga viwanda vya kutengeneza vifaa vya kilimo na mashine. Mashine za kusaga nafaka n.k. Viwanda vya nguo na kuanzisha dini kibao za uwongo. Viwanda vya vinywaji kama pombe, soda, juisi n.k. Viwanda vya kutengeneza sabuni na marashi, vipodozi na mapambo. Viwanda ya kutengeneza vifaa vya baridi kama majokofu na viyoyozi, n.k. tayari kwa kutuuzia sisi soko lao.

Soko hili litawezekana tu ikiwa watupoteza na kututumainisha ili watuamuru tubadili dini (mila) (4:119) (utaratibu wetu wa maisha). Tukavaa utaratibu wa maisha unaohitajia mazao yanayotoka viwandani mwao. Mradi wao huu wakauita serikali. Na ndio basi kwa kutumia Makanisa na mashule wakawatayarisha wenzetu weusi, jamaa zetu ambao walifanywa kuwa na udugu wa kidini na Wazungu (Wakristo); na kuwapa uongozi wa nchi pale tulipopewa uhuru wa bendera.

Hivyo mtoto wa kwanza mweusi aliyekalia kiti cha gavana aliunda wizara tisa (27:48) kama alivyofunzwa na waungu wenye akili (wazungu). Nazo ni Wizara ya Ustawi wa Jamii na Wanawake, Wizara ya watoto (elimu), wizara ya fedha, wizara ya madini na nishati, wizara ya usafirishaji, wizara ya mifugo, wizara ya kilimo, (3:14) wizara ya biashara na viwanda ya nyumba (9:24).

Mambo yakawa hivi: Kila mwezi wa sita na wa saba, Bunge hukaa na kuidhinisha kugawa mfuko wa hazina (beitil maal) na kila wizara kupewa fungu lake. Na mchezo ndio uko hapa. Kumbe wakuu wa wizara wote ni wahitimu wa vyuo vikuu (miungu 9:31) waliofunzwa na miungu yenye akili (Wazungu). Kwa hiyo huzigawa fedha walizopangiwa mafungu mawili. Moja ni maendeleo. Ambazo moja kwa moja ni za kwenda kununulia mali za viwandani Ulaya. Na fungu la pili niza matumizi ya ndani. Ambazo hutumika, moja kuwalipa mishahara wafanyakazi wasio zalisha chochote ila kusimamia mradi huu ulio siri. Hata hivyo fedha zao hizo za mishahara hurudi tena Ulaya kwa sababu huzitumia kununulia vitu madukani. Na vingi vilivyoko madukani ni vya Wazungu.

Pili, fedha hizi za matumizi ya ndani hununulia vifaa vya maofisi na makaratasi, vitu ambavyo vyote hutengenezwa ng'ambo. Na usisahau vipando, mafuta na ulinzi.

Hivyo turudie kusema tena kuwa Mhadhiri Masoud kasema kweli na aliona mbali. Si miungu (wanavyuoni 9:31) wa Wazungu wamewajengea watu wao uchumi yaani wanaochuma kutoka migongoni mwetu na majasho yetu; tena kwa gharama zetu. Na zoezi hilo linasimamiwa na mingu (wanavyuoni 9:31) yetu, tena kwa gharama zetu. Hivyo wao Wazungu wana kila kitu na sisi tumegeuzwa na kuwa omba omba (22:13). Kwa kuwaomba Wazungu misaada, huko ndiko kuwaabudu 6:56). Kwa hiyo juwa kwamba madhalimu (4:160) ni wale walioukurubia ule mti (2:35); nao ni neno baya (14:26).

Neno gani hilo? Yule atakayesema: "Mimi ni Rais mungu, (kiongozi)". Kaa mbali na kiumbe huyo. Huyoni dhalimu (21:29) anayefuata matamanio yake bila kujua (30:29) ambaye Mwenyezi Mungu amemuacha kupotea na anataka nasi tukengeuke mkengeuko mkubwa (4:27). Na imeshakuwa (34:20). Lakini kwa kutokujua haya, ndipo mtoto wa kwanza aliyeingia Ikulu (nyumba iliyoko mji mkuu) alipokuwa akikaa gavana, mwaka 1962 akaisajili nchi yetu katika nyumba ya maangamizo (New York). Hivyo tukawa madhalimu kwa sababu nyumba hiyo ni Kibla cha wale waliopewa kitabu ambayo tumekatazwa tusiielekee (2:145). Kwa kufuata matamanio yao hao watu wa kitabu (2:145), tumefanya yale tunayoyataka sisi kuwa mungu (45:23) (25:43). Kwa hiyo wengi wetu hatusikii wala hatufahamu, bali ni kama wanyama (25:44) na ndio tulioghafilika (7:179).

Walioghafilika Mola wetu anatujuza (19:39) kuwa ni madhalimu na wamo katika upotofu ulio dhahiri (19:38). Nao ni wale walioshika miungu mingine badala yake (36:23-24). (Kumbuka wasomi wetu waliohitimu vyuoni ndio mingu yetu 9:31), na ndio tuliwashika, hivyo tumekufuru (19:37) kwa kugawanywa makundi (28:4) na sasa tuko katika vyama vya upinzani (38:2). Kumbe hivyo tunapinzana na Mtume bila kujua (47:32), kwa hiyo Mwenyezi Mungu anaviangusha vitendo vyetu (uchumi unaanguka) tumefanywa watumwa (23:47). Hivyo kuwafanya (wasomi) wetu kuwa Marais (Rais si ndiye Jemedari (mlinzi) Mkuu?) (18:102) tumepata hasara kubwa (7:23 (18:103). Mamilioni kwa mabilioni ya mali na fedha miaka arubaini sasa tangu tupate uhuru yamesagika kwa maisha yetu kuwa duni isivyoelezeka.

Kumbe ni kwa sababu bidii yetu hiyo imepotea bure katika (maisha ya dunia (3:14, 9:24) huku tukifikiri kuwa tunajenga nchi (18:104) Wallah! Kumbe utaratibu huu wa kushika mingu mingine badala ya Allah ukiwauliza ni mambo gani haya? Husema: "Sisi ni mazungumzo na mchezo ... (9:65). Tambua hapa Mola wetu anatufundisha kitabu kuwa wao husema: "Hii ni siasa". Kwani si kweli? Hebu waulize siasa ni nini? Watasema Politics is a game. Kwa hiyo utaratibu huu ambao watu humteua mja wa Allah kuwa Rais ni dini hiyo. Na ndiyo dini ya Kiyahudi (4:160).

Lakini imebatizwa, badala ya kuitwa dini ya Kiyahudi, imeitwa Siasa. Hivyo wale wenzangu weusi waliosimikwa madarakani (wanasiasa Wakristo) kusimamia sera hii iliyo siri na kali (serikali) (mradi wa wakoloni unaosimamiwa kwa siri na viongozi wa Makanisa weusi bila wao kujua), ukiwatajia Mungu katika suala la uongozi; mara moja watahamaki: "Usichanganye dini na siasa".

Masikini mwanasiasa huyu hajui kwamba kusema "usichanganye dini na siasa" (Ufalme) wa Mungu na uongozi (Urais) wetu". Lakini huyo huyo ukimkuta Kanisani utamkuta anaimba "Ufalme wa Mungu uje duniani kama uilvyo huko mbinguni" Ajabu! Ajabu! Huku ndiko kulogwa (2:102)?

Mradi huu wa Wazungu (serikali) sera yake ya pili ni kutuharamishia vitu vizuri tulivyohalalishiwa. Na ni nini kitakachokujulisheni hata ukajua ni vitu gani vizuri alivyotuhalalishia Mwenyezi Mungu, lakini waungu wetu wameviharamisha?

Alivyotuhalalishia Allah ni amri kumi (za Musa) (6:151-153), nayo ndiyo njia ya (Mtume) iliyonyooka (6:153). Kwa maana iliyohalali kwetu ni njia iliyonyooka ( na sio njia ya demokrasia(! Na hiyo njia ya Mtume iliyonyooka, ndio njia ya Allah (42:52-53). Kwa maana iliyohalali kwetu nji ya Allah (na sio ya twaghut). Na kufuatwa hiyo njia ya Allah iliyonyooka (6:126) ndio kumuabudu Yeye (43:64). Kwa maana iliyohalali kwetu ni kumuabudu Allah (na sio kumuabudu shetani 36:60).

Itaendelea toleo lijalo

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook