Waumini 15 wakamatwa Nzega
 

Na Mwandishi Wetu

WAUMINI 15 wametiwa mbaroni wilayani Nzega mkoa wa Tabora kwa madai ya kuendesha mhadhara uliokashifu dini nyingine.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Nzega msako wa kuwakamata waumini ulianza baada ya kiongozi mmoja wa dini mjini humo kupeleka taarifa za uongo polisi.

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili kutoka mjini Nzega, muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jumanne alisema hali ya wasiwasi iliwaingia viongozi wa dini nyingine baada ya kikundi cha mhadhara cha AL MALLID kutoka jijini Dar es Salaam kuwasili mjini humo na kufanya mhadhara kwa siku tatu mfululizo ambapo waumini kadhaa wa madhehebu waliripotiwa kusilimu.

Kufuatia kufikishwa taarifa hizo polisi, OCD alitoa amri kusitisha mhadhara huo.

Hata hivyo imedaiwa kuwa mhadhara uliendelea na ndipo polisi wa kawaida na wale wa kutuliza fujo (FFU) walipotawanywa wilaya nzima kuwasaka vinara wa mahubiri hayo ya dini.

Gazeti hili liliwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora Bwana Ignas Mtana ambaye alithibitisha kukamatwa kwa watu hao kwa madai ya kutumia matusi na kashfa katika mahubiri.

"Watu hao wamekiuka sheria kwa kuendesha mhadhara nje ya muda uliopangwa na kutumia lugha ya matusi kwa dini nyingine", alidai kamanda Mtana.

Kufuatia kukamatwa kwa waumini hao polisi mkoani Tabora imeimarisha ulinzi wilayani Nzega kwa kuhofu vurugu zinaweza kufanywa na wananchi wenye hasira.
 

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook