Mneselusewa na Ismail Ameir wa Morogoro MSJ
MAENDELEO ya nchi huletwa na wananchi wenyewe pamoja na viongozi wao waliowapa mamlaka na madaraja ya kushika usukani wa jamii husika.
Mipango mizuri ya uendeshaji nchi, utekelezaji wa kufaa wa mipango hiyo na nguvu kazi imara huwa chachu miongoni mwa chachu za maendeleo katika taifa.
Kinyume cha hayo nihali tuliokuwa nayo hivi leo nchini, ambapo maendeleo yamekuwa ni kitu cha kufikirika kama si kusadikika kuwa kipo katika sura ya dunia tunayoishi.
Maendeleo yamekuwa ni "hadithi" muhimu ya kuombea kura nyakati za chaguzi mbalimbali nchini.
Kibaya zaidi vijana ambao ni sehemu ya nguvu kazi ya maendeleo hayo kutumiwa vibaya au kupuuzwa kabisa na serikali waliyoichagua wenyewe hususan vijana wa Kiislamu.
Licha ya kuwa na elimu nzuri, mwenendo wa kuridhisha na umri wa kufaa, kupata ajira imekuwa kama "ngekewa" (mnyama mdogo ambaye ni nadra sana kuonekana) kwao.
Kwa wasichana wa Kiislamu wenye msimamo thabiti wa dini yao hulazimishwa kutoa rushwa ya mwili ili kupatiwa ajira, na hao ni wale wenye umbile lililomvutia muajiri, wasio na sifa hiyo au mwenye kukataa matokeo yake ndiyo hayo ya kuishia katika sufuria za mama ntilie au mito ya Msimbazi, Ubungo n.k. kuchimba mchanga na kuponda kokoto.
Wale wasiojimudu kiimani huangukia Ohio Street kuuza miili yao au kujihusisha na uhalifu mwingine.
Vivyo hivyo kwa wavulana, biashara za madawa ya kulevya, pombe, kushiriki ujambazi, kamari n.k. huwa ndiyo chaguo lao kuu.
Na hii ndiyo sababu ya wao kujaa magerezani ama kuwa wengi katika kila tukio la uhalifu.
Aidha, mamia kama si maelfu mengine ya vijana wa Kiislamu kunyimwa elimu ya juu (ya sekondari na vyuo) ni sababu nyingine ya wao kuangukia katika uhalifu. Sasa tujiulize hii ni bahati mbaya au mpango wa serikali?
Marehemu Franlin D. Roosevelt aliyepata kuwa Rais wa Amerika aliwahi kusema: "Nothing happens in politics which is not planned". Akimaanisha kuwa jambo lolote halitokei katika siasa ila huwa limepangwa.
Sasa tuwaulize serikali ya
CCM iweje wawe mabingwa wa kutunga sheria kalikali dhidi ya wahalifu, bila
kuangalia kile kilichopelekea wafanye uhalifu. Iweje utumie silaha nzito
kuua inzi mmoja mmoja badala ya kuondoa mzoga ili udhia uishe? Na hilo
ndilo suluhisho la kudumu. Serikali ya CCM isiangalie pale walipoangukia
vijana bali watazame pale walipojikwaa.
|
|