DONDOO ZA SAIKOLOJIA
 
Na Abu Halima Sa Changwa
 
AGGRESSION (Ushari - Onevu)
 

AGGRESSION (ushari - onevu) ni tabia ya kutenda jambo lenye lengo la kuwadhuru au kuwaumiza wengine, iwe kwa makusudi tu au kwa sababu maalumu.

Wana-Saikolojia wamejaribu kwa muda mrefu kuisoma tabia hii kwa sababu inaiathiri jamii, hasa pale inapotoka katika hali ya kudhurika mtu mmoja na kufikia hali ya jamii nzima kuathirika.

Ubongo wa binadamu wa leo umeendelea kiasi kwamba umewazesha kutengeneza silaha zinazoweza kuleta mauaji na uharibifu wa kila aina kwa binadamu wenzao, tena bila ya kukutana nao ana kwa ana, na tendo hili la kuua na kuangamiza, au kuleta uharibifu, likachukuliwa na watu wa upande fulani kama ni ushujaa.

Takwimu zinaonyesha kwamba kati ya mwaka 1820 na 1946, binadamu waliua binadamu wenzao wapatao milioni hamsini na tisa, katika vita na mashambulizi mengine ya kimauaji (soma kitabu cha Richardson, L.S. kiitwacho Statistics of Deadly Quarrels. yaani Takwimu za magomvi ya hatari, cha mwaka 1960). Sasa hivi watu wanaambiwa wameshastaarabika zaidi, lakini ndio wamekuwa zaidi na ushari- onevu.

Takwimu za mwaka 1972 za Marekani zinaonyesha kuwa Marekani ilikuwa ikitumia dola milioni 200 kwa mwaka kuhakikisha kila mtoto anapata elimu, lakini ikawa inatumia dola milioni 2800 kuwafundisha askari mbinu za vita. Nimetoa mfano wa Marekani kwa vile wao ndio vigogo vya ushari-onevu na hii takwimu ni ya wakati uliopita sijui sasa hivi.

Kwa ujumla, ushari-onevu umekuwa kwa kiasi kikubwa kuanzia katika ngazi ya familia hadi kimataifa.

Wanasaikolojia wamejaribu kutoa sababu mbalimbali za ushari-onevu. Kuna wale waliosema kuwa ushari-onevu unatokana na historia ya binadamu kwamba zamani alipokuwa mnyama, ilibidi awe mshari-onevu (aggression) kwa sababu maisha yake yalitegemea kuwinda viumbe wengine. Lakini wanasaikolojia wanauliza, mbona mtu keshatoka huko na ndio amekuwa mshari-onevu zaidi?

Kuna wale wanaosema kuwa ushari-onevu ni tabia ya asili ya binadamu kama ilivyo kwa viumbe wengine, isipokuwa wapo viumbe wanaokuwa washari-onevu mara nyingi hawadhuru viumbe wa jamii yao, kwa mfano simba kumdhuru au kumuua simba mwenzie. Viumbe au wanyama wengi waliotoweka sasa hivi duniani ambao hawakuwa na faida kwa wanyama au viumbe wengine walitoweka kwa ajili ya kuua wenyewe kwa wenyewe. Binadamu hufikia wakati wakachoka kuuana na kutaka suluhu. Lakini je, ushari-onevu ni tabia asilia? Wanasaikolojia wengine wanasema hapana, la sivyo jamii ya binadamu isingeendelea kuwapo leo, kwa vile mtu mmoja anaweza kuua mamilioni.

Wanasaikolojia wengine wanasema ushari-onevu ni tabia inayopandikizwa ubongoni mwa mtu, kwamba watu hujifunza kuwa washari-onevu kama wanavyojifunza mambo mengine ambayo hawayajuwi au tabia nyingine ambazo hawakuwa nazo. Madhali ushari-onevu unawapa utulivu wa moyo basi watajifunza na wakiuweza ndio inakuwa raha kwao.

Sababu inayokubalika zaidi sasa hivi, ya ushari-onevu ni ya kisaikolojia. Ushari-onevu unaweza kuja kwa njia kadhaa, kitaalamu zinaitwa Defence mechanisms (njia za kujikinga/kujiliwaza).

1. Sublimation (mchemko)

Mara nyingi watu huwa na ushari-onevu wanapokosa kile kinachoweza kuwa maslahi fulani, na ushari-onevu huo huelekezwa kwa wapinzani wao. Ubongo wa mtu huchemka anapokosa ushindi au anapoona anapoteza malashi ya kiushindani na mcheko wake unafikia kumfanya amdhuru au ikiwezekana hata kumuua mpinzani wake, bila ya haki. Haya inaonekana ndio yanayowapata Waislamu wa leo duniani kote kutoka kwa makafiri, na ndio kinachowaponza Waislamu hata humu mwetu, wakafungwa, kupigwa na hata kuuawa bila ya haki ya kisheria, kwa vile wanaonekana kuishinda kihoja dini nyingine ambayo pia ni dini ya baadhi ya wakuu.

Displaced aggression:

Huu ni ushari-onevu unaoelekezwa kwa mtu au kiumbe asiye na kosa, madhali tu ni mdhaifu. Kwa mfano mtu anaweza akakorofishwa kazini, labda na bosi wake, akapandwa na jazba ya hasira, lakini kwa hofu akacheka tu jino pembe wakati ndani ya moyo anaungua. Mtu huyu anaporudi nyumbani, anaweza akatoa hasira zake kwa viumbe au watu wengine, mfano ampiga paka teke, akamzaba makofi wanawe na kumshambulia mke wake bila ya kosa la msingi. Hapa tunatizama kiwango cha familia. Katika kiwango cha kitaifa au mataifa, ushari-onevu umekuwa ukiwaangukia watu wasio na hatia. Miaka ya nyuma, kuna waandishi wawili waliofanya uchunguzi, mnamo mwaka 1940. Hawa ni Carl Hovland an Robert Sears. Wao waligundua kwamba kati ya mwaka 1882 hadi 1930, weusi wapatao 3386 walinyongwa bila mashitaka. Hawa walinasibisha kunyongwa huku na hali ya uchumi. Wameandika kwamba katika kipindi chote hicho, idadi ya walionyongwa ilipungua mno wakati wa hali nzuri ya kiuchumi, na ulizidi mno wakati wa hali mbaya. Hii inaonyesha hasira za Wazungu zilikuwa zinawaangukia sana weusi wakati wa hali mbaya.

Pengine hii inatokea hata leo. Hivi karibuni uvumi umeenea kwamba hasira za Rais Clinton wa Marekani za kushambuliwa kwa kashfa za uasherati zimekuwa zikiwaangukia watu wa Iraq. Hii ni defence mechanism kuondoa hasira zake na vile vile kuwafanya watu wa Marekani wamuone zaidi ni mwamba kuliko muasherati.

Inawezekana pia hii ndio inayowakuta Waislamu sehemu nyingi tu. Nchi inaweza kuwashinda watawala, hasa inapokuwa na hali mbaya uchumi. Sasa wanaposhindwa kuonyesha umwamba wao kwenye kutatua matatizo, wanatafuta umaarufu sehemu nyingine. Hivyo kwa kuwafunga, kuwapiga na kuwaua Waislamu, wanadhani watapata sifa zitakazoficha uozo wao kwenye uongozi. Hivyo mtawala huyo kwa kuwa mshari-onevu kwa kundi moja, anajipatia sifa kutoka kwa wasiokuwa Waislamu, na vile vile kutoka kwa Waislamu wasiojitambua.

Historia, hata hivyo inaonyesha kuwa ushari-onevu haudumu. Wanaonewa hufika mahala wakasema basi. Kwa hiyo, kama washari-onevu hawatakumbwa na kifo ambacho mshari-onevu asiyechagua, basi waonewa wataamua tu kufa
 
 

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook