Hijab kuvaliwa rasmi mashuleni

Na Mwandishi Wetu

WANAFUNZI wa Kiislamu wa shule za Msingi wataanza rasmi uvaaji wa sare ya shule yenye kuzingatia imani yao baada ya Afisa wa Elimu Jiji kusambaza barua kwa Maafisa wa Wilaya ukiwataka watekeleze maelekezo ya mkutano wao uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Februari 20, mwaka huu.

Katika barua hiyo ya Machi 24, mwaka huu yenye Kumb. Na. DCC/W/23/52 Vol.1/6 ambayo gazeti hili lina nakala yake, Afisa huyo Bwana A.S. Mbegu ameambatanisha waraka wa Wizara ya Elimu wenye kuruhusu vazi hilo kwa wanafunzi wasichana wenye kutekeleza mafunzo ya dini yao.

Waraka huo wa Wizara wenye Kumb. Na. EDC.10/62/Vol. 417 wa Agosti 28, mwaka 1995 ulifuatia kauli ya Rais kuhusiana na vazi la Hijab lenye kuzingatia sare ya shule kwa wanafunzi husika.

Mkutano wa waalimu wakuu ukumbi wa Karimjee ulitoa ufafanuzi wa aina ya "hijab" itakayoruhusiwa mashuleni ambapo ukaazimia kuwa iwe ni sketi "ndefu" ya bluu, blauzi nyeupe mikono mifupi na mtandio mweupe.

Hata hivyo ufafaunzi huo huenda ukazua utata kwa wanafunzi kwani kwa mujibu wa maamrisho ya Uislamu mikono haitakiwi kuwa wazi isipokuwa viganja vyake.

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook