MISAHAFU ya dini inawafundisha wanaadamu sanaa ya kuchinja wanyama kabla ya kuwala. Baadhi ya mafundisho hayo ni haya:
"Nawe umchinjie pasaka BWANA, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng'ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina lake" (Kumbukumbu la Tofati 16:2)
"Hata siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, ni wapi utakapo tuende tukuandalie uile pasaka? (Marko 14:12)
"Basi sali kwa ajili ya Mola wako na uchinje (kwa ajili ya Mola wako" (Qur'an 108:2)
Licha ya maandiko hayo matakatifu kusisitiza sanaa ya kuchinja wanyama kabla ya kuwala, kuna watu kadhaa wanaokula wanyama bila ya kuwachinja. Wanachofanya ni kuwanyonga au kuwapiga nyundo (au kitu kizito) ili wazimie au wanawaua kwa silaha kama vile bunduki na hatimaye wanawatoa ngozi au manyoya na kuwakatakata na kuwatia jikoni.
Baadhi ya watu wanaokula wanyama bila ya kuwachinja si waumini wa dini iliyofundishwa na Mitume (Manabii) wa Mwenyezi Mungu. Kwa jina maarufu watu hao wanaitwa wapagani.
Na watu waliobaki kati ya wale wanaokula wanyama bila ya kuwachinja, wenyewe wanadai kuwa ni wafuasi wa dini sahihi iliyofundishwa na Mitume (Manabii) wote.
Ukiwauliza, kwanini wanafanya kinyume na maandiko, watu hao hawakosi cha kujibu. Baadhi yao wanadai kuwa sheria za kuchinja ni za kimwili na hazimpeleki mtu peponi! Wengine wanazidi kusema kuwa hayo ni mapokeo ya Wayahudi, kwa hiyo kwa sasa hayana nafasi!
Lakini mtu wa aina hii akipata maradhi na kushauriwa na daktari kuwa kuanzia sasa asile nyama ya mnyama asiyechinjwa, hapo tena hatakuwa na hoja. Lakini sheria za Muumba wake anadai hazimpeleki peponi. Huu ni mtazamo finyu kuhusu sheria za Mungu Muumba. Kwa maneno mengine, sheria za Mwenyezi Mungu zina faida za kimwili (afya, n.k) na pia zile za kiroho (watu watiifu kuingizwa peponi).
Kuna mambo mengi yaliyohimizwa katika misahafu ya dini ambayo hikma yake bado haiko wazi katika akili za kibinadamu. Yaani sayansi na teknolojia ya mwanaadamu hazijaweza kuzigundua hikma hizo.
Hata hivyo, kuna mambo mengine yaliyofundishwa katika misahafu ambayo hikma yake iko wazi katika akili za mwanadamu. Moja kati ya mambo hayo ni kuwachinja wanyama.
Kwa mujibu wa sayansi ya vyakula na teknolojia yake (Food Sicience and Technology), kitendo cha kuwachinja wanyama ni cha kisayansi. Yaani kina faida kubwa kisayansi. Katika makala hii nitaeleza faida moja.
Damu ya mnyama yoyote yule
ni makazi mazuri ya vimelea vyenye kuweza kuambukiza maradhi (Pathogens).
Aina mojawapo ya vimelea hivyo ni Salmonella. Salmonella
wanaambukiza maradhi mbalimbali kama vile homa ya matumbo (typhoid fever).
Kwa hiyo, unapomchinja mnyama ile damu yake inatoka nje. Pamoja na vile
vimelea. Katika hali kama hiyo mlaji wa nyama ya aina hiyo huwa katika
mazingira ya usalama zaidi ya kutokuambukizwa maradhi ikilinganishwa na
yule anayekula nyama ya mnyama asiyechinjwa.
|
|