Aya hii inatufundisha kuwa Mwanadamu ameletwa hapa ulimwengu ili awe Khalifa wa Allah (s.w.). Kuwa Khalifa wa Allah (s.w.) hapa ardhini ni kusimamisha ufalme wa Allah kwa niaba yake. Kusimamisha ufalme wa Allah (s.w.) ni kusimamisha sheria za Allah katika jamii na kuiongoza jamii kwa mwongozo wake. Ni pale tu mwanadamu atakapokuwa Khalifa wa Allah (s.w.) ndipo atakapoweza kuishi kwa furaha na amani na kulifikia lengo halisi la maisha yake hapa ulimwenguni. Ukhalifa wa Allah (s.w.) si cheo anachojipachika mtu bali atavishwa cheo hiki yule mwenye kumuamini Allah (s.w.) ipasavyo na kufanya vitendo kama mwenyewe Allah (s.w.) anavyoahidi katika Qur'an:
Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na kufanya vitendo vizuri kuwa atawafanya Makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya Makhalifa wale waliokuwako kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia dini yao aliyowapendelea, na kwa yakini Atawabadilishia amani baada ya hofu yao. Wawe wananiabudu hawanishirikishi na chochote. Na watakaokufuru baada ya hayo basi hao ndio wavunjao amri zetu (24:55).
Katika aya hii Allah (s.w.) anaahidi kuwa wale watakaoamini vilivyo kwa kufanya yale yote anayoyaridhia na kuyaacha yale yote aliyoyakataza atawawezesha kuwa watawala katika ardhi watakaohakikisha kuwa sheria za Allah (s.w.) ndizo zinazotawala katika jamii. Hii ni ahadi ya kweli yenye kutekelezwa pasina shaka. Na nani mkweli wa kutekeleza ahadi hii kuliko Mwenyezi Mungu kama ilivyo dhihiri kwa Mtume Muhammad (s.a.w.) na jamii ya Kiislamu aliyoiunda katika kipindi cha miaka 23.
(c) Lengo la maumbile na lengo la maisha ya hapa Ulimwenguni
Mtazamo wa Uislamu juu ya lengo la maisha ya mwanadamu na lengo la kuwepo ulimwengu uliomzunguka ni tofauti na ule wa kikafiri. Mtazamo wa makafiri tumeshauona kuwa ulimwengu huu hauna Muumba na kwa hiyo haukukusudiwa ufikie lengo lolote. Uislamu unatufundisha kuwa, haiwi kwa mwenye akili kukubali kuwa ulimwengu huu na vyote vilivyomo vimekuwepo tu bila ya lengo. Lengo la kuumbwa ulimwengu na vilivyomo limebainishwa katika Qur'an:
ya hayo tukaawandikia wana wa Israel ya kwamba atakayemuua mtu bila ya yeye kuua mtu, au bila ya kufanya fisadi katika nchi, basi ni kama ameua watu wote, na mwenye kumwacha mtu hai (kumsaidia kuishi) ni kama amewaacha hao watu wote. bila shaka Mitume waliwafikia na hoja zilizo wazi; kisha wengi katika wao baada ya haya walikuwa waharibifu sana katika nchi (5:27-32).
Katika ya hizi majina ya watoto hawa wa Adam hayakutajwa. Bali majina hayo yamechukuliwa kutokana na maandishi mengi ya historia - hasa historia ya Mayahudi. Wafasiri wengi wa Qur'an wanataja katika kuzitafsiri aya hizi kuwa, habil na Kabil ni watoto wa moja kwa moja wa Adam na Hawwa. Na sio imetajwa kwa ishara tu kwa kuzingatia kuwa watu wote wametokana na Adam na Hawwa. Kwa mujibu wa maelezo ya Sheikh A.S. Farsy, hiki ndicho kisa cha awali cha mtu kumuua mwenziwe. Na aliyeuawa ndiye mwanadamu wa mwanzo kufa. Kwa sababu hiyo basi aliyefanya mauaji hakujua nini la kufanya na yule maiti. Ndipo Allah (s.w.) akamleta kunguru kumwonyesha namna ya kuhifadhi maiti ya ndugu yake.
Ili kuyafahamu vyema mafundisho ya kisa hiki cha watoto wa Adam ni vyema tuyazingatie mazingira na wakati ziliposhuka aya za kukielezea kisa chenyewe.
Tunafahamu kuwa awali Allah (s.w.) aliwachagua Mayahudi na kuwapa ujumbe wake ili watekeleze wao wenyewe na kisha waufikishe kwa watu. Kwa hiyo akawatuma Mitume wengi miongoni mwa Mayahudi. Kutokana na neema hii waliyopewa kuletewa mwongozo na kupewa jukumu la kuusimamia, wakawa ni watu wenye hadhi kubwa.
Enyi kizazi cha Israili (Mayahudi); Kumbukeni neema zangu nilizokuneemesheni na nikakutukuzeni kuliko viumbe wengine (wa wakati huo) (2:47).
Hata hivyo Mayahudi hawakuithamini neema hii ila wachache tu. Zaidi ya wao wenyewe kutofuata mwongozo waliwaua Mitume na kufuata baadhi ya kitabu huku wakiacha sehemu nyingine. Hii iliwapelekea kupata laana ya Allah. Aidha, Mayahudi walibashiriwa kuja kwa Mtume (s.a.w.) na waliahidi kuwa watamfuata. Bali alipokuja walimkataa.
Na (wakumbushe) aliposema (Nabii) Isa bin Maryam (kuwaambia Mayahudi); "Enyi wana wa Israil; mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, nisadikishaye yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na kutoa habari njema ya Mtume atakayenijia nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad (Muhammad).
Lakini alipowajia kwa hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni udanganyifu ulio adhahiri. (61:6).
Mayahudi hawakuishia kumkataa tu Mtume (s.a.w.) walidhamiria kumua pia. Hapakuwa na jingine lililowapelekea kufanya hivyo, bali ni husuda na kiburi.
Ni katika mazingira haya, Allah (s.w.) anabainisha kisa hiki cha watoto wa Adam ili kuwaonya Mayahudi na sisi sote kuwa: Tusiwe na husuda juu ya Neema na amali njema za watu wengine hata tukaingia kwenye makosa kama ya mtoto wa Adam. Bali nasi tuzitakase nafsi zetu kwa kutenda mema kwa ajili ya Allah (s.w.) nasi atuinue daraja. Allah hawaongoi na kuwapokelea maombi watu madhalimu. Aidha, uongofu haupatikani kwa kumwonea husuda na kijicho mwenye kufanya mema. Bali kwa kujitakasa na kufanya amali njema.
...Akasema (yule asiyekubaliwa sadaka yake): "Nitakuuwa" Akasema (yule aliyeahidiwa kuuawa): "Mwenyezi Mungu huwapokelea wamchao tu" (5:27).
Vile vile Uislamu unatutaka tusiwe ni wenye kulipiza ubaya juu ya ubaya tunaotendewa. Mtu anatakiwa ajitetee na awatetee wengine dhulma inapotaka kufanyika. Lakini asipange kuwafanyia uovu wengine. Bali amwogope Allah na kuishika njia iliyo sawa.
"Kama utanyoosha mkono kwangu kuniua; mimi sitakunyooshea mkono wangu kukuua, Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu. Mola wa walimwengu pia". (5:28).
2. Historia ya Nabii Nuhu (a.s.)
Mtume Nuhu alitumwa kwa watu
ambao walikuwa wa mwanzo kupotosha mafundisho ya njia sahihi ya maisha
ya Nabii Adam. Kutokana na vidokezo vilivyo ndani ya Qur'an na mabaki ya
kihistoria (archaelogical remains) hivi leo simulizi za historia zilizopokelewa
kutoka kwa wakazi wa kale wa Kurdistan na Armenia zathibitisha pia kauli
hii.
|
|