Badili dini tukupe mahindi waambiwa Waislamu
 

Na Kassim Billo, Tanga

KUTOKANA na njaa iliyowakumba wananchi wa Kabuku wilayani Handeni, Shirika moja la kidini la Kanisa Katoliki limepeleka misaada ya chakula katika eneo hilo la Kabuku lakini msaada huo wa chakula cha mahindi hawapewi wasiokuwa Wakristo na ukitaka upate mahindi hayo ya msada waambiwa ubadili dini yako uwe Katoliki ndipo upewe.

Inasemekana kuwa kundi hilo la Wakristo wanatumia hali hiyo ya njaa kufanya kampeni kubwa kwa kuwageuza Waislamu kuingia Ukristo kwa kuwaambia kuwa atakayekuwa Mkristo atapewa mahindi.

Habari hizi zimethibitishwa na kiongozi mmoja wa dini ya Kisilamu ambaye anasimamia kituo cha taasisi ya Ansaar Muslim kule Kabuku Mudir Ayub Deman aliyesimulia kisa hiki akiwa mjini Tanga mnamo mwishoni mwa wiki.

Osmani ametowa mwito kwa Masheikh watembelee sehemu hiyo ya Kabuku ili kuwaokoa ndugu zao Waislamu ambao huenda wakatekwa nyara na kutumbukizwa katika dini ya Kikristo kwa ajili ya njaa waliyonayo hivi sasa.

Masheikh hao waende kufanya mihadhara na pia ikiwekana kupelekwa msaada wa haraka wa chakula kuwasaidia Waislamu ambao wameathirika kimaisha kwa ajili ya njaa.


Akinamama wakutana Gombo la Mboto Wazindua Kamati yao

Na Muhibu Said

KAMATI ya akina mama ya kutetea haki za Waislamu nchini hivi karibuni imezindua rasmi kamati yake teule tawi la Gongo la Mboto, Jijini Dar es Salaam.

Shughuli ya uzinduzi wa Kamati hiyo ilifanyika Jumamosi ya Aprili 3, mwaka huu, katika Msikiti wa Ijumaa uliopo Gongo la Mboto Mwisho Jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo uliandamana na mhadhara mkubwa wa akina mama wa Kiislamu wa Jijini uliofanyika Msikitini hapo ambapo mada mbalimbali ikiwemo vazi la mwanamke wa Kiislamu (hijab), nafasi ya Qur’an tukufu na nafasi ya Muislamu nchini zilizungumzwa.

Mapema akizundua tawi hilo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati hiyo, Bi. Fatma Lazaro, Ukti Ummu Hamza aliwataka akinamama wa Gongo la Mboto kujenga umoja wao kupitia tawi hilo.

Ili kuimarisha umoja huo, Bi Ummu Hamza aliwataka pia akina mama hao kuhakikisha wanafanya sensa, kudumu katika kutembeleana nyumba hadi nyumba na kufahamiana kwa kila hali.

Aidha, aliwapa majukumu mengine kwa kuwataka waanzishe mfuko wa kusaidia kina mama ili kuondokana na shida mbalimbali za kimaisha zinazowakabili na kuanzisha shule za awali zitakazokidhi mahitaji ya elimu kwa watoto wa eneo hilo.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Kamati hiyo teule, Bi Mayasa R. Sadallah, Kamati yake inakusudiwa kuzuru vijijini ili kuwazindua walioghafilika.

Taarifa za awali zilieleza kuwa Imamu wa Msikiti huo, Ustadh Hassani, siku moja kabla ya kufanyika uzinduzi huo, aliitwa na kuhojiwa na polisi wa kituo kidogo cha Gongo la Mboto kwa muda wa masaa kadhaa.

Kwa mujibu wa Ustadh huyo, polisi walimtaka awaeleze ni akina nani walioandaa mhadhara huo na nini kingezungumzwa.

Hata hivyo, baada ya kujibiwa kuwa waandaaji walikuwa ni akinamama wa Kiislamu na kwamba walipanga kuzungumza mambo yanayohusu dini yao, polisi hao walimwachia na kumtaka akawaeleze akina mama hao kwamba katika mazungumzo yao wasijaribu kugusia CCM!
 

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook