'Mbezi - Kisiju waungwana hatutaki Kanisa'
 

Na Mwandishi Wetu

WAISLAMU wa Mbezi-Kisiju wamesema kwamba wao ni waungwana asilia (Waislamu) hivyo hawawezi kupokea Ukristo wala kuruhusu Kanisa lijengwe.

Aidha, wamesema Uislamu na Ukristo ni itikadi mbili zisizokutana na kwamba Uislamu umekuja kupambana na kufru ya kudai miungu watatu katika umoja. Na hivyo wamesema kwamba anayetamani Kanisa imani yake ni sifuri kama sio kafiri.

Waislamu hao wa Mbezi wameyasema hayo Machi 26, 1999 walipokutana Msikitini kwao kujadili taarifa kwamba serikali ya kijiji imekusudia kutoa ardhi lijengwe Kanisa wakati hakuna Mkristo hata mmoja.

Waislamu hao wamesema kwamba wanapinga ujenzi wa Kanisa kwani katika vijiji vyote vya Mbezi - Kisiju hayupo hata Mkristo mmoja si wa asili au wa kuritadi.

Waislamu hao wa Mbezi chini ya Maimamu na Masheikh wao wamewatuhumu viongozi wa kitongoji kwa kutumia madaraka yao vibaya kwa kutoa idhini ya kujengwa Kanisa katika mashamba ya Waislamu bila ya ridhaa yao.

Wamewataka viongozi hao watengue kibali hicho na waepuke kuwaletea kitu kinachodhuru Uislamu wao.

Wamesema kisiasa watasimama katika msingi wa "Lakumdiinu Kum Walyadiin" lakini hawataruhusu wavurugiwe dini yao.

Kabla ya kumaliza kikao chao waliazimia kuleta kunuti katika Ijumaa ili kumuomba Allah awaepushie laana.
 
 

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook