| Soma Toleo la Wiki iliyopita |
KITENGO cha Huduma ya Kikristo ya Haki za Binadamu kimeeleza kwamba muda wowote kuanzia Aprili 21, askari wa kutuliza ghasia (F.F.U) watatumika kuutwaa Msikiti wa Masjid Mwinyi ambao Bw. Daniel Zakaria anadai kwamba ni nyumba yake ya urithi.
Akiongea na gazeti hili kwa njia ya simu juzi, Mchungaji Elias Kibela alisema kwamba waumini wa Masjid Mwinyi wamepewa siku 21 toka Aprili 21 kuhama Msikiti huo vinginevyo wamlipe Bw. Daniel shilingi milioni 20 au wamtafutie nyumba nyingine nzuri ya vyumba sita katika eneo la Ilala au Kariakoo. Endelea...
Na Kassim Billo, Tanga
KUTOKANA na njaa iliyowakumba wananchi wa Kabuku wilayani Handeni, Shirika moja la kidini la Kanisa Katoliki limepeleka misaada ya chakula katika eneo hilo la Kabuku lakini msaada huo wa chakula cha mahindi hawapewi wasiokuwa Wakristo na ukitaka upate mahindi hayo ya msada waambiwa ubadili dini yako uwe Katoliki ndipo upewe.
Inasemekana kuwa kundi hilo
la Wakristo wanatumia hali hiyo ya njaa kufanya kampeni kubwa kwa kuwageuza
Waislamu kuingia Ukristo kwa kuwaambia kuwa atakayekuwa Mkristo atapewa
mahindi. Endelea...
|
|