Wanyimwa sehemu ya kuswalia

Na Mwandishi Wetu
 

WANAFUNZI wa shule ya Jangwani wamedai kuzuiwa kutumia chumba walichokuwa wamepewa kuswalia awali.

Kutokana na maelezo ya Mkuu wa Shule hiyo wanafunzi hao wamezuiwa kutumia chumba hicho baada ya yeye kupata habari kutoka Usalama wa Taifa kwamba upo mpango wa baadhi ya watu kujenga Msikiti shuleni hapo.

Awali wanafunzi hao walipewa chumba cha kuswalia ambapo waliamua kukifanyia ukarabati kwa vile kilikuwa na ubovu. Kabla ya zoezi hilo kufanyika Mkuu wa Shule aliwazuia wasikitumie.

Mwalimu Mkuu huyo Mama Theresia Mkamati amedai kuwa yeye aliendewa na watu wa Usalama wa Taifa wakidai kwamba panajengwa Msikiti shuleni hapo.

Kutokana na ujio huo inaonekana katika hali ya kujihami na kujitakasa ndipo hatua ya kuzuia sehemu ya majengo ya shule kufanyia ibada ikachukuliwa.

Juhudi za gazeti hili kuongea na mwalimu huyo kwa njia ya simu hazikuweza kufanikiwa, hata hivyo mwalimu wa dini shuleni hapo amethibitisha taarifa hizo, hata hivyo akadai kuwa Mkuu huyowa shule hakutaka kutoa ufafanuzi wowote zaidi ya kusisitiza kuwa alifikiwa na watu wa Usalama wa Taifa.
 

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook