AN-NUUR
Gazeti la Kiislamu la kila wiki - Tanzania
Toleo la Internet

Kufungwa kwa Benki ya Greenland:
Museveni kutembelea Misikiti kujieleza
Na Mwandishi Wetu

RAIS Yoweri Museveni wa Uganda amesema kwamba atakwenda Misikitini kuelezea ni kwanini serikali yake imeifunga Benki ya Greenland na kwamba hataifungua abadan.

Akihutubia Kamati ya Utendaji ya chama chake kinachotawala Uganda huko Jinja wiki iliyopita Rais Museveni amesema alipoamua Benki hiyo ifungwe baadhi ya watu wamedai kwamba kuna siasa.

Hivyo akasema kwamba ataitembelea Misikiti nchini Uganda kutoa ufafanuzi . Hata hivyo Rais Museveni hakutoa ufafanuzi nini maana ya kuwa na siasa katika jambo hili na kwanini awazungukie Waislamu Misikitini kutoa ufafanuzi badala ya kuwaeleza wananchi wa Uganda kwa ujumla.  Endelea...
 

Wasilimisha Kijiji
Na B. Mwakangwale

WATU kadhaa wasiokuwa Waislamu katika kijiji cha Mchito Dodoma Vijijini wameufuata na kuingia katika Uislamu imefahamika.

Akiongea na Mwandishi wa habari hizi katika ofisi za gezeti hili, Sheikh Salum Abubakar Kazi, alieleza kuwa yeye ni wa kwanza kusilimu kijijini kwao tangu mwaka 1991, baada ya kusilimu alipata mafunzo yake ya Uislamu Kimamba (Morogoro) kwa Sheikh Abubakar Swalehe Bombaheka kwa muda wa miaka mitatu (1993-95).

Baada ya kurejea nyumbani (Mchito) alikuta kuna Waislamu wawili, hivyo pamoja na yeye wakawa watatu; "Tulikuwa tukiendesha ibada zetu chini ya mwembe", alisema. Endelea...


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook
 
Gazeti hili huchapishwa na Islamic Propagation Centre, Box 55105, Dar es Salaam