CHAKULA NA LISHE
 
Chakula ni silaha ya kuwamaliza wanadamu
 

Na Mjahid Mwinyimvua

WATU wengi wanadhani kuwa silaha ya kummaliza binadamu ni vitu kama vile bunduki, bomu, panga, kisu, sumu na mfano wa vitu vya aina hiyo. Ukiwaambia watu kuwa vyakula vinavyotengenezwa viwandani ni silaha kubwa ya kumaliza kizazi (fulani) cha wanadamu, hawakuelewi. Makala hii inaweka wazi dhana hiyo ili wale ambao wagumu kuelewa waelewe. Na kama wataendelea kukaidi, sisi kama wanahabari hatutakuwa na lawama, kwa sababu tumetimiza wajibu wetu.

Katika teknolojia ya utengenezaji wa vyakula vya viwandani, vitu kadhaa vyenye au visivyokuwa na hatari kiafya vinaweza kuingia kwa kukusudiwa au bila ya kukusudiwa. Vitu vingi vinavyowekwa makusudi katika vyakula huwa vina madhara kidogo au havina madhara kabisa. Vitu hivyo huwa na malengo mazuri kama vile kukifanya chakula kisioze, kuongeza ladha ya chakula, kutia rangi chakula, kuongeza virutubisho, kuongeza uzito au wepesi wa chakula, n.k.

Hata hivyo, mbali ya nia hiyo njema kuna baadhi ya watengenezaji wa vyakula huweka vitu fulani katika vyakula wanavyovitengeneza kwa lengo la kuwamaliza wanadamu wenzao, hasa kizazi cha kesho. Kwa vile baadhi ya watu huwa wagumu kuelewa hoja kama ya hapo juu, bila ya kutolewa mfano, nachukua fursa hii hapa chini kulinukuu jarida (Magazine) moja lenye mfano halisi wa dhana ninayoizungumza katika makala hii.

Gazeti la Echo of Islam la Januari, 1998, Na. 163, likinukuu gazeti la Washington Post, limeripoti kuwa wafanyabiashara wa Kiyahudi wamesambaza vyakula kwa Wapalestina wa ukingo wa Magharibi (wa Mto Jordan) ambacho ni hatari kwa afya na pia kinapunguza uwezo wa binadamu kuweza kuzaa.

Gazeti hilo likiwanukuu maafisa wa Kipalestina linapasha kuwa, utawala wa Kiyahudi umesambaza bazoka (Chewing gum) ambazo zina dawa inayojulikana kama Sex Hormone. Bazoka hizo ambazo zinauzwa kwa bei ndogo katika mashule mbalimbali yaliyoko katika ukingo wa Magharibi (wa Mto Jordan), zinauwezo wa kupunguza uwezo wa kuzaa na kubeba mimba.

Washington Post kama lilivyonukuliwa na Echo of Islam linazidi kutupasha kuwa kiwanda cha kutengeneza maziwa ya kopo ya watoto, kimepeleka (ukanda wa Magharibi) maziwa yaliyokwisha muda wake (Expired consumption date).

Vile vile gazeti hilo limeripoti kuwa, wafanya biashara wa Kiyahudi wamepeleka unga uliooza katika ukanda wa Magharibi (wa Mto Jordan).

Ndugu wasomaji, jambo la kuzingatia katika rejea ya hapo juu siyo tu kuhujumiwa kwa Wapalestina na Wayahudi. Kwani wengine (wasiokuwa na ubinadamu) wanaweza kusema hao ni Wapalestina na sisi Watanzania!

Wengine wanaweza kufanya ushabiki wa kidini, na kudai kuwa hao Wapalestina ni Waislamu. Waache yawakute yanayowakuta! Bali pia ninalotaka watu (hasa viongozi wa nchi) wazingatie ni kuwepo kwa teknolojia ya kukitumia chakula kama silaha kuwaangamiza hasa watoto wetu, ambao ndiyo taifa la kesho.

Katika hali ya sasa ya Tanzania ambapo wananchi wanakufa kwa njaa (wiki hii baadhi ya vyombo vya habari (Mtanzania) vimeripoti vifo vya wananchi 45 Mahenge, wilayani Ulanga, mkoa wa Morogoro) na huku serikali inawauzia wenye njaa chakula kilichotolewa bure na shirika la mpango wa chakula duniani WFP (Tazama gazeti la Kiongozi linalotolewa na Catholic Publishers Limited toleo la Aprili 18-24, mwaka huu).

Katika hali kama hiyo, jambo la kutisha zaidi mambo hayaishii hapo. Viongozi kadhaa wa madhehebu ya dini ya Kikristo nchini wamemsifia Rais Benjamin William Mkapa kwa jitihada alizozifanya kurekebisha uchumi toka alipoingia madarakani.

Pia viongozi hao wamesema kuwa shutuma za Prof. Lipumba ni za kisiasa tu (turejee gazeti la Msema Kweli Aprili 18-24, 1999).

Kama mwanahabari naimalizia makala yangu kwa kuwaambia wananchi kuwa, katika hali kama hii ambapo serikali imeshindwa kutimiza ahadi zake na Kanisa linaitetea, sitegemei serikali kuwa makini kwa vyakula kama bazoka (Gig G) na kadhalika. Kama hatua ya awali wananchi muwe makini na vyakula vyakula hasa vinavyotoka nje.

Hatua ya pili ni ile ya muda mrefu, wananchi (wazawa) wawekeze katika viwanda vya vyakula ili siyo tu kuinusuru jamii yetu na majanga ya kiafya na utasa, bali pia kukuza nguvu za kiuchumi kwa wananchi wetu.
 

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook