HALI ya Uislamu katika vijiji vya Seregete 'A' na 'B' vilivyoko katika kata ya Kidugalo, tarafa ya Ngerengere mkoani hapa ni mbaya kufuatia eneo hilo kutokuwa na walimu wa dini licha ya kuwepo Waislamu wengi.
Vijiji hivyo vilivyoko mwishoni mwa mkoa wa Morogoro na Pwani kupakana na kijiji cha Lukenge mkoa wa Pwani havina Msikiti wala madrasa ambapo Waislamu wanalazimika kufanyia ibada zao chini ya mwembe.
"Hapa ndipo tunaposwalia
baadhi ya Waislamu wengi waliokuwepo hapa kijijini", alisema Bw. Abdallah
Saidi Dakawa akionyesha kiwanja kilichofagiliwa chini ya mwembe huku kukiwa
na mkeka mmoja pamoja na birika iliyoning'nizwa katika tawi la mti huo,
mara baada ya kuulizwa na mwandishi wa habari hizi ni wapi sehemu wanapofanyia
ibada zao. Endelea...
Na Idd Katimba, Tabora
RAIS mstaafu Mh. Ali Hassan Mwinyi amewatahadharisha Waislamu wawe macho na wang'amue hatari iliyo mbele yao ambapo uadui na nguvu zote zilizo kuwa dhidi ya Ukomunisti zimeelekezwa katika Uislamu.
Amewaambia Waislamu kuwa kama ambavyo Ukomunisti umekufa; ni tamaa ya wapinzani wa Uislamu kuona nao unakufa au kusambaratika.
Alhaj Mwinyi aliyasema hayo akiwahutubia maelfu ya Waislamu waliohudhuria kuweka jiwe la msingi la Madrasa na Msikiti wa Mtendeni (TANESCO) eneo la Kiloleni. Endelea..
|
|