Soma Qur'an Tuifahamu Dini yetu(25:3)
 

Na: Tahir Rashid

QUR'AN NI KITABU (2:2) na ni MUUJIZA ulio HAI - KISOMWI kilichotakaswa (98:2) Nuru ambayo kwayo (Allah) Humuongoza Amtakaye (42:52).

Ni agizo kwetu kuisoma (73:4) kwani ni ukumbusho kwa walimwengu wote (69:70) Hasa kwa yule anayetaka kushika njia (81:27-28) yakurejea kwa Mola wake (42:10).

Na Kitabu (hiki) hakikutemremshiwa (Mtume Muhammad) isipokuwa abainishie (watu) yale ambayo (1) Wanakhilitilafiana na (kiwe) (2) uongozi na (3) rehema kwa watu wanaoamini (16:64) ili Dini ihuishwe (16:65) kwa amri yake (na) watu waonyeke kuwa hakuna kiongozi ila Yeye (Allah), basi Aogopwe (16:2) Yeye tu. Yeye ndiye mwenye vyeo vya juu, Mwenyekiti (40:15) Kiongozi (wetu) mmoja tu (37:4), Rais wa mbingu na ardhi na yaliyomo kati yake; na ni Rais wa (nchi zote zilizoko) mashariki (na zilizoko Magharibi) (37:5).

Rais wetu huyu (Allah) Ametufanyia hisani kubwa waumini (vile) alivyomleta Mtume akatusomea Aya zake, na kututakasa na kutufundisha Kitabu na hikima (3:164), (ili tusalimike na) upotofu (huu tulionao sasa duniani) ulio dhahiri (3:164). Upotofu huu uliodhahiri ni kule kushika miungu mingine badala yake (36:23-24). Na miungu hiyo si wengine bali ni Viongozi bandia (wanaofarikiana 12:39) tuliowateka (15:96) na kuwapa vyeo (majina) tunavyopanga sisi wenyewe (12:40) pindi walipohitimu katika vyuo vikuu (9:31). Hivyo wao wanavyuoni wetu hawa na watawa (lao moja), wametuwekea dini (isiyokuwa ndiyo) (42:21) tulipowafanya sawa na Rais (Mola) wa walimwengu wote tulipowateua kuwa viongozi (26:98). Imekuaje tumegeuzwa (10:32) na kuingizwa kwenye upotofu kwa kumuweka Rais (Mola) wetu wa Kweli Allah? (10:31). Kiongozi anayeturuzuku kutoka mbinguni na katika ardhi, sio kutupeleka kuomba misaada kwa wazungu na kwa wachina 22:13) anayemiliki masikio na macho, amtoaye mzima katika mfu na kumtoa mfu katika mzima. Na hutengeneza mambo yote (10:31). Imekuwaje? Hatusadiki (10:31) hivyo tungojee kuthubutikiwa na kauli yake kwa kuasi kwetu? (10:33). La!

(Muhammad) alitumwa (kuja) kuongoza na (kutufunza) dini ya haki (chama cha kweli) ili aijaalie kushinda (kuchukua uongozi chama hiki) juu ya dini zote (vyama vyote); ijapokuwa watachukia MADEMOKRATI (WASHIRIKINA 30:31-32) (9:33). Kumbe neno washirikina limebatizwa na kuitwa mademokrati bila sisi kujua utaratibu wa maisha unajaalia watu kukhitilafiana.

IKHTILAFU:

Muhammad (47) kaletwa kubainisha Ikhtilafu iliyoko baina ya watu kwa wale wanaoamini (16:64) (wanaofuata aya za Allah 28:47).

Tujiulize ni nini Ikhtilafu? Jibu: Kwa wale wanaofuata Aya za Allah (28:47) Ikhtilafu ni ile Khabari Kubwa (78:2-3).

Kuwa macho ( ). Yaliyosemwa hapo ni kwamba, kwa wale waumini (28:47) wao Ikhtilafu ni ile Khabari Kubwa. Na nini basi kitakachokujulisha (90:12) hata akajua KHABARI KUBWA ni nini Jibu:

KHABARI KUBWA (38:67) ni yule mwingi wa Rehema, mwenye nguvu, Rais wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake (38:66) Mmoja hakuna Kiongozi (Mungu) ila Yeye (38:65) Hivyo tuonyeke (25:1) kwamba Umma wetu huu ni Umma mmoja, na yeye (Allah) ni Rais wetu (21:92). (Lakini) jambo hili tumejiepusha nalo (38:68) na kulivunja baina yetu (tukafarikiana (21:93) na kuwa makundi makundi (30:53). Hivyo tumeshika miungu (viongozi) wengine badala Yake (42:9),

WITO WA MUHAMMAD

Mlinganiaji wa Allah akiita (46:31) "Enyi watu! Njooni katika neno lililosawa ....., ya kwamba:

1. Tusimuheshimu, wala kumuogopa wala kumuomba, wala kumpenda kupita kiasi [taz: Kamusi neno Abudu (kd)] yeyote yule ila Allah; wala tusimshirikishe na chochote (tusifuate matamanio ya nafsi 45:23); tusije wafanya wengine (wetu) kuwa viongozi badala ya Allah (nao ni wanavyuoni na watawa ambao tunawapigia kura) 3:64 kutomuitikia mlingani huyu (tukadai kuwa maongozi yetu haya, hayana dini); ndio kuwa katika upotofu uliodhahiri (46:32) Na jambo hili la kukataa uungu (Uongozi) wa Kiongozi mmoja ndio "Munkar" (16:22). "Munkari: uzuiliwe (ukataze (3:114), Eh!

Uongozi wa Allah ndio Uongozi (2:120) Kwa hiyo ikisemwa MUNKARI UZUILIWE, moja ya maana ni kwamba usiwepo Uongozi mwingine bighairi ya huu wa Allah. Jambo la leadership (uwongozi) ni wa nani; mtu asishindane nawe. Na walinganie watu kumwendea (kumwelekea kwa maongozi) Rais wako. Bila shaka wewe (Muhammad) uko juu ya uongozi ulio na msimamo (22:67-68). Mwenyezi Mungu anajua yote (wapinzani 38:2) wanayoyatenda (22:69), Hukumu ni Yake siku ya kiama katika Ikhtilafu (hii) (22:69) ya kumpa ukuu na ukubwa binadamu wenzetu tukawafuata (33:47) badala ya Allah ambaye ndiye Mkubwa na ndiye aliye juu, juu, juu, zaidi.(2:255).

(Itaendelea toleo lijalo)

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook