Na Abubakar Marwilo
Napenda kuchangia fikra zangu, lau kidogo kuhusu makala aliyoaandika Batuli Hussein katika gazeti la An-nuur la tarehe Dhulhija, April 16-22, 1999, yenye kichwa cha habari "Jumuiya ziwe na mwelekeo wa kimapinduzi".
Kwanza ninampongeza bi Batuli Hussein kwa kuandika makala hii ambayo inalingana na wakati tuliyonao. Wakati unatudhihirisha kuwa yapo makundi mawili hapa duniani yenye kuvutana kwa nguvu kubwa kwa lengo la kusimisha malengo yao. Kundimoja linapigania haki na kundi jingine linapigania batili.
Muislamu wa kweli hawezi kuukana ufalme wa Mwenyezi Mungu. Lakini bado Jumuiya zetu hazijafanya matayarisho ya kutosha kuelekeya kwenye kufanikisha malengoya ufalme wa mwenyezi Mungu yanafikiwa.
Sidhani kama ipo jumuiya yenye mpango kabambe wa elimu kwa lengo la kuwapata mabingwa wenye elimu za Kiislamu na kadhalika. Pia elimu za kama ipo jumuia iliyoandaa mpango kabambe wa uchumi wa Kiislamu na kadhalika kwa jamii yetu yenye mchanganyiko wa Waislamu na wasiokuwa waislamu. Upo utengano mkubwa kati ya Jumuiya na jamii. Jumuiya zimeshindwa kabisa kueneza huduma za jamii mijini na vijijini. Huku ndiko kuwa karibu na watu na kuwafaa watu. Uislamu unatuhimiza sana kuwa watu wa wanufaa kwa watu. Ndiyo maana Waislamu wa mwanzo walinunua visima kwa ajili ya watu; walikusanya zakah kwa ajili ya wanaohitaji kufuatana na shariah; walitembea mashariki, magharibi, kusini na kuskazini kuelimisha watu na kufanya mengine mengi mazuri. Yale tunayo yafanya leo hayalingani hata kidogo na yale waliyoyafanya na kuyaonyesha kama mfano bora wa kuigwa. Waislamu wa awali.
Tumekuwa ni watu wa maneno matupu na hatuna tofauti yeyote na watu wa nyama vya siasa. Watu wa vyama vya siasa wamekuwa mstari wa mbele kupotosha siasa na kuwahadaa watu.
Mwenyezi Mungu anatutaka Waislamu kuepukana na watu wanaofanya hadaa, kwani hakuna mafanikio yeyote kama utatumia hadaa kuwa ni nyenzo katika harakati za Uislamu. Tunaamrishwa na mwenyezi Mungu kuwa Waislamu wenye imaniya yakini, wenye kuitafsiri imani hiyo katika vitendo vyetu vya kila siku, wenye kusema ukweli, haki na wenye subira katika misukosuko. chombo cha ushauri ni muhimu sana kwa ajili ya kupanga mambo yetu. Jumuiya zimefanywa ni chombo cha watu wachache, hazitoi fursa yeyote ya kuwashirikisha Waislamu katika maamuzi. Kutokana na hili zimejiweka mbali mno na watu; hivyo kupoteza nguvu ya jamii. Kama nguvu hii ya jamii hauna, kwa nini isitoshe kusema jumuiya zimepoteza uhalali wake wa kuwepo. Uislamu ni jamii na kinyume cha hivyo ni vigumu kusimamisha ufalme wa Mwenyezi Mungu.
Kusimamisha ufalme wa Mwenyezi Mungu kunahitaji mpango wa mapato na mali uliyomzuri ili kufanikisha malengoyaliyowekwa na kindi. Jumuiya zetu, karibu zote, hazina mapato wala mali ya uhakika, na kama kawaida zinategemea kuomba. Wafadhili wa hapa nchini wamebadilika kiasi kikubwa kwamba wanatumia fedha zao katika biashara kuliko kutoa kwa njia ya Mwenyezi Mungu. Na kwa ujumla wafadhili wa nje wametusahau kabisa, wanachofanya hivi sasa ni kununua majumba makubwa makubwa katika nchi za Magharibi. Tutafikia vipi malengo yetu kama hatuna mipango ya kilimo; mipango ya zakah na hatuna Bait-mali.
Leo hatuna Aboubakari Sadiq aliyejitolea mali yake yote kwa ajili ya Uislamu, na kisha akaulizwa amebakiza nini? Akajibu: Amebakiza Mtume (s) na Mwenyezi Mungu. Wafadhili wetu wawe wa ndani au nje hawana sifa kama ya Abubakari Sadiq. Sababu: Wana upungufu wa imani na akhera hawaiamini vilivyo.
Ummoja ni somo ambalo bado
halijaeleweka ndani ya safu za uongozi katika jumuiya. Viongozi wao kwa
wao wanasuguana na mara kwa mara wanaodoana kutoka nyadhifa zao bila sababu
ya au za msingi. uchuguzi uliyofanyika umethibitisha kuwa viongozi wengi
wa jumuiya hizo wana upungufu wa mafunzo ya dawah yenye kiwango cha Qur'ani,
Sunnah za Mtume (S) na uzoefu wa uendeshaji wa kitaifa na ki-mataifa. Pia
nafsi zao ni chafu; daima nafsi chafu haiwezi kufaulu. Kazi kubwa ni kuikandamiza
nafsi au kuitaksa. Na kazi hii siyo kazi ya Mwenyezi Mungu; bali ni ya
binaadamu mwenyewe. Mwenyezi Mungu amekwisha tamka wazi kuwa hayuko tayari
kubadilisha mambo yetu, kama sisi wenyewe hatutakuwa tayari kujibadili.
|
|