Ya Rabi tunakuomba, salama
utupatie,
Makosa tuliotenda, ya Illahi
tughufirie,
Sasa saa imefika, salama
tushuhudie,
Amani ni fursa adhim,
Jerusalem tuililie.
Mafanikio tuone, Jerusalem
itungarie,
Jerusalem ni nyumbani, sote
tukasalimie,
Tumerithi kwa Nabii Ibrahimu
(a.s.) utufaidikie,
Amani ni fursa adhim,
Jerusalem tuililie.
Jerusalem ni Al-Quds, vitabu
tuvijulie,
Imejengwa kinadhifu, Waislamu
tujivunie,
Mji huu mtukufu, ya Illahi
tubarikie,
Amani ni fursa adhim,
Jerusalem tuililie.
Wakati wa sasa umewadia,
Jerusalem itung'arie,
Rehma nyingi tuombe, na
mema tujifanyie,
Tuwache mtafaruku, umoja
tujivunie,
Amani ni fursa adhim,
Jerusalem tuililie.
Masjid Al-Aqsa, ni adhim
ziara tujifanyie,
Safari zinyepesi, Hajj Trust
ituandalie,
Al-Quds ni aziz ziara, za
kheri tujifanyie,
Amani ni fursa adhim,
Jerusalem tuililie.
Kisa cha Miraj kitukufu,
sote tukifatilie,
Safari ya Rasul Llah (s.w.),
adhim tuizingatie,
Dini ya Kiislamu, kamilifu
ibada tujifanyie,
Amani ni fursa adhim,
Jerusalem tuililie.
Imani Tawhiid, na Taqwa
sote tujihimize,
Kamba ya Ikhwani, imara
wajibu tuishikilie,
Hii itajenga imani, na umoja
itupatie,
Amani ni fursa adhim,
Jerusalem tuililie.
Ikhwani wa Palestine, Yarabi
uwajaalie,
Subra kubwa wapate, dhambi
uwaghufurie,
Neema uwapatie, na Dar-Ul-Salaam
uwajaalie,
Amani ni fursa adhim,
Jerusalem tuililie.
Shairi si fani yangu, watalaam
mnisahishie,
Hili ni langu la kwanza,
hivyo munisaidie,
Makosa niliofanya, ya Illahi
nighurufie,
Amani ni fursa adhim,
Jerusalem tuililie.
Dr. Amur Abdullah Amur,
Dar es Salaam.
Kwa kweli ninashangazwa,
na vijana wa kisasa,
Mambo wanayavamia, bila
hata kuchunguza,
Mwisho wanakurupuka, na
kuanza kutangaza,
Kuweka kali halali, amri
katoa nani.
Kabla hatujatangaza, yatupasa
kuchunguza,
Kwa vitabu kuvisoma, na
watu kuwauliza,
Majibu ukiyapata, sasa kaa
na chunguza,
Kuweka kali halali, amri
katoa nani.
Mola katofautisha, binadamu
na wanyama,
Akili katujaalia, tofauti
na wanyama,
Mambo kujichunguzia, kabla
hatujayafanya,
Kuweka kali halali, amri
katoa nani.
Kufanya hivyo ni bora, kuliko
kusemezana,
Tutajenga umma bora, bila
hata kuzozana,
Tutamrisha Mola , na Islamu
jamia,
Kuweka kali halali, amri
katoa nani.
Bibi Aisha kasema, Mtume
alifundisha,
Laana itawapata, wanawake
hapa hapa,
Nyuso zao kukwaruza, na
nywele kubadilika,
Kuweka kali halali, amri
katoa nani.
Sasa inaonekana, tayari imewapata,
Kwani wamekengeuka, nywele
mpya kubandika,
Wamkosoa Muumba, kwa hiba
aliowapa,
Kuweka kali halali, amri
katoa nani.
Mimi wananishangaza, wanaopenda
kuweka,
Amri wanakiuka, aloiweka
Rabuka,
Eti wanadai kwamba, waume
zao wapenda,
Kuweka kali halali, amri
katoa nani.
Harufu mbaya hutoa, jua linapowapiga,
Madhara mengi hupata, kwa
vidonda kuwatoka,
Na mainzi kuwafuata, kama
wabeba mizoga,
Kuweka kali halali, amri
katoa nani.
Tamati na tamatia, ujumbe
huu sikia,
Kalamu naiachia, ujumbe
kukufikia,
Sasa kazi ninawapa, kuanza
kufuatilia,
Kuweka kali halali, amri
katoa nani.
Jabiri Bakari wa Kibasira,
MSAUD (MTP) Form III,
Survey, Dar es Salaam.
2. Nguo zinahuzunisha, mwajitia
matatani,
Waume kutamanisha, zinachangia
kuzini,
Jamii zatukanisha, zawatia
utumwani,
Wetu vigogo nchini, Kwanini
mwakaa kimya?
3. Nguo hadhi zawashusha,
sawa kama punguani,
Unyama kudhihirisha, nyuso
haya hazioni,
Mavazi haya yachosha, kila
muda twalaani,
Wetu vigogo nchini, Kwanini
mwakaa kimya?
4. Na ukweli waonyesha, wasivyo
kuwa makini,
Uchi wajitembezesha, afadhali
punguani,
Kwanini mwajidumisha, na
kujishusha thamani,
Wetu vigogo nchini, kwa
nini mwakaa kimya?
5. Kwa nini mwajiuzisha,
kusiko taadhimani,
Nyie mwajishughulisha, kujitoa
heshimani,
Vichupi mwajivalisha kuzagaa
hadharani,
Wetu vigogo nchini, kwanini
mwakaa kimya?
6. Ubakaji kuzidisha, jamii
matatizoni,
Na lisilo pendezesha, kwanini
kulithamini,
Kwenu nyie mwajikosha, msiwekwe
hatiani,
Wetu vigogo nchini, kwanini
mwakaa kimya?
7. Sio kuwa na watisha, tu
ninauthamini,
Ndo maana nawajulisha, miili
isitirini,
Heshima mtapandishwa, vaa
vimini chumbani,
Wetu vigogo nchini, kwa
nini mwakaa kimya?
8. Nyie zawafurahisha, nguo
fupi mapajani,
Kwao nyie mwajikosha, msiwekwe
lawamani,
Twaomba kuwasitisha, mwaogopa
kitugani,
Wetu vigogo nchini, kwanini
mwakaa kimya?
9. Twashauri kupitisha, sheria
zilo makini,
Sio kuwachelewesha, kwani
wanawapa nini,
Hapa ninahitimisha, nguo
fupi kumuni,
Wetu vigogo nchini, kwanini
mwakaa kimya?
Abdull Rawph B. Ally
P.O. Box 157,
Hai-Moshi
Tufurahike waumini mwaka mpya kutujia
1. Bismillahi Rahamani, kwa
jina lake Jalia,
Maliki wa duniani, na akhera
yote pia,
Sifa zake kila shani, nashindwa
kuelezea,
Tufurahike waumini, mwaka
mpya kutujia.
2. Ni mwaka wa Kiislamu,
idadi twahesabia,
Hesabu ya Kiislamu, mwanzo
ilipoanzia,
Moja nne tarakimu, mbili
ziro kufatia,
Tufurahike waumini, mwaka
mpya kutujia.
3. Alipohama rasuli, madina
kuelekea,
Kwa idhiniya Jalali, dini
ipate enea,
Hakujali hata mali, na anasa
za dunia,
Tufurahike waumini, mwaka
mpya kutujia.
4. Twamtolea pongezi, kwa
moyo alioutoa,
Kwa uwezo wa Mwenyezi, amri
aliitikia,
Kuitekeleza kazi, nuru ipate
enea,
Tufurahike waumini, mwaka
mpya kutujia.
5. Masahaba nao pia,, salamu
twawatolea,
Kwa moyo walioutoa, mtume
kumsaidia,
Safarini kuelekea, katika
mwaka hijria,
Tufurahike waumini, mwaka
mpya kutujia,.
6. Kushukuru ni lazima, kwa
yule ulimjia,
Kwa kuuwahi mzima, na uhai
kubakia,
Wangapi wameshazama, kaburini
wametua,
Tufurahike waumini, mwaka
mpya kutujia.
7. Ndugu yenu Sulemani, kalamu
naiachia,
Nasubiri gazetini, shairi
litapoenea,
Shime ndugu waumini, nasaha
kuzingatia,
Tufurahike waumini, mwaka
mpya kutujia.
Suleiman Mohamed Abdalla
P.O. Box 5252,
Dar es Salaam
Bismillahr-Rahmani; Allah
Mola jalia;
Leo naishika peni, na mdomo
kuinua,
Yamekithiri jijini, maudhi
yamezidia,
Kitimoto hadharani, ni
wapi twaelekea?
2. Kitimoto mabuchani, dhahiri
yaning'inia,
Mabango barabarani, alama
kuashiria,
Kuwa huko kuliani, kitimoto
kimejaa,
Kitimoto hadharani, Luanda
nimechukia.
3. Kitimoto mitaani, hufugwa
kama ngamia,
Wanaranda majaani, kama
kuku mezagaa,
Ni kero mchikichini, mishikaki
jichomea,
Kitimoto hadharani, kwa
nini twavumilia?
4. Kitimo hasa nani, anayekifurahia,
Anayewapa leseni, kero kutuongezea,
Amekataza manani, yeye wapi
ametoa,
Kitimoto hadharani, kuuza
ati yafaa??
5. Kitimo mitaani, tume itatuambia,
Hivi kwa sheria gani, leseni
yawapatia,
Nchi isiyokuwa na dini,
nguruwe yakumbatia!!!
Kitimoto hadharani, ni
hapo ninapoanzia!
6. Kitimo tangu lini, ruhsa
kuning'inia?
Au ni kigogo gani, moto
anayechochea,
Anachokitaka nini, midomo
tukiinua?
Kitimoto hadharani, Tukianza
kukemea?
7. Mauaji ya jijini, ndivyo
yalivyoanzia,
Paroko yake maoni, Dola
ikamwitikia,
Mwembechai magomeni, serikali
imeua,
Kitimoto hadharani, we
haya!! malizia!!!
8.Kitimoto mabuchani, jiji
mwatuchafulia,
Keenja kama huoni, haifai
nyamazia,
Madhara yake pomoni, na
maradhi mengi pia,
Kitimoto hadharani, balaa
mwatutakia.
9. Kitimoto asilani, hatutakivumilia,
mazingira hatarini, mengi
hima kiondoa,
Tunamuudhi Manani, nini
tutamuambia,
Kitimoto hadharani, wapi
tunaelekea.
10. Kitimoto hamuoni, masheikh
mkakemea,
Kimara barabarani, makongo
kwingine pia,
Kimya chenu cha nini, mabaya
kunyamazia,
Kitimoto hadharani, masheikh
shime kemea.
11. Kitimoto kipingeni, ikulu,
bungeni pia,
Tulaani hadharani, unyama
uharamia,
Wa kuzitoa leseni, nguruwe
kutuuzia,
Kitimoto hadharani, kwa
pamoja twakemea.
K.S. Luanda (Nolo)
Dar es Salaam
1. Kila mara utambuwe, kuwa
cheo ni dhamana,
Hicho kisikuzuzuwe, kujiona
wa maana,
Wakumbuke uwajuwe, ambao
leo hawana,
Cheo ni dhamana.
2. ushikapo madaraka, mjumbe
ama Mbunge,
heshima yako yataka, kwa
wananchi uchunge,
Isije kuharibika, mawazo
nao uchange,
Cheo ni dhamana.
3. Cheo kiko kama maji, huingia
na kutoka,
Kitapotoka hakiji, mwingine
atakishika,
MUNGU ndie mtoaji, humpa
anayetaka,
Cheo ni dhamana.
4. MBUNGE kuwa mkweli, msiwe
waongo-ongo,
Mnapoliliwa hali, toweni
wenu mchango,
Msitafute muhali, wala kuleta
maringo,
Cheo ni dhamana.
5. Tamati KUCHAGULIWA, angalia
uendako,
KURA msipopigiwa, utapata
maumbuko,
Na ukweli utajuwa, punguza
MARINGO yako,
Cheo ni dhamana.
Yahya O. Barshid (Yob)
Madaraka Hote
Morogoro.
|
|