Soma Qur'an tuifahamu dini yetu
 
 

Kumuabudu Allah:

LENGO la watu kuumbwa ni ili tupate kumuabudu (51:56) (Allah). Kumuabudu Allah, ndio njia iliyonyooka (43:64). Na kwa kushika yaliyofunuliwa kwa Muhammad (43:43) nayo ni kwamba hakuna kiongozi ila kiongozi mmoja tu (21:108), itapelekea kuwa katika njia iliyonyooka (43:43) ambayo yeye Muhammad aliongoza kwayo (42:52) nayo ndiyo njia ya Allah (42:53). Uislamu (6:126) dini ya Mitume wote (42:13)Amri (45:17) kumi za Nabii Musa ni njia ya Muhammad iliyonyooka (6:151-153). Dini hii ndio Allah aliyotuchagulia (2:132) (aliyotusajilia) na kutupendelea (5:3) (kutupa kibali). Kwa hiyo tusife isipokuwa tumeshakuwa Waislamu.

Waislamu ni watu ambao humuheshimu na kumuogopa na kumuomba na kumpenda kupita kiasi kiongozi (Mungu) mmoja tu, kiongozi (Mola) wa mababu zetu waliotutangulia (2:133). Lakini kwa kuwaheshimu na kuwaomba na kuwaogopa na kuwapenda kupita kiasi badala ya Allah (miungu) ambayo haikuteremshia amri na ambayo hatuna ilimu nayo (22:71), wametupambia kuwaua watoto (uzazi wa majira) na dini (utaratibu wa maisha) kuvurugika (6:137). Hivyo kufarakana kwetu katika dini na kuwa makundi makundi tujue hivyo hatuna uhusiano na Muhammad (6:159)

Waislamu si wengine bali ni wale watu wanaoamini aya za Allah (27:81). Wao humwogopa na kumuomba na kumheshimu na kumpenda kupita kiasi (humuabudu Rais wa mjia (wa Makka) (27:91). Kwani Makka ndio mji wao mkuu (Kibla) (2:150) wanaelekea kwa maongozi na baraka (3:96). Muhammad ndiye Mbunge (Nabii) wao wanayemfuata (2:143) kwa sababu Rais (Mola) wao ni Allah (22:40).

Na dini yao (chama) ni Uislamu (41:33). Kitabu chao (katiba) ni Qur'an (27:92). Ifuatwe Katiba hii bila kuzuiwa na yeyote na kampeni ifanyike (28:87) ili watu wamjue Rais wao wa kweli. Namna hivi aya zinaelezwa (6:55) ili (watu) wapate kufahamu (6:65). Na ili njia ya waovu (Marais) ibainike (6:55).

Tumeona kuwa Waislamu ni wale wenye kuamini aya zake Allah (27:81) nazo ni kitabu (13:1) Qur'an aliyoifundisha (55:2) sasa ni nini kitakachokujulisha hata ukajua (kuamini kitabu 2:177) ni kitu gani? Allah anajibu kwa kusema:

"Hakika wanaoamini aya zetuni wale tu ambao wanapokumbushwa nazo huanguka kusujudu, na humtukuza Mola wao kwa kutaja sifa zake, nao hawatakabari (32:15). Huinuka mbavu zao kutoka vitandani wakati wa usiku ili kumuomba Mola wao kwa kuogopa moto na kutaraji pepo na hutoa katika yale tuliowapa (32:16). Mwenye sifa hizi ndiye ambaye kwa lugha ya Kiarabu na sasa Kiswahili huitwa Muislamu.

Uongozi:

Yeye Muhammad kaletwa kutubainishia uongozi (16:64) wa kutiiwa ulio na matokeo bora (maendeleo) (4:59). Kwani suala la uongozi ni jukumu lake (Allah) (92:12). Humuongoza amtakaye (2:272) naye akamteremsha (wanaotaka) kuongozwa (28:56). Hivyo akamteremshia kitabu (18:1-5). Kwa kitabu hicho Allah huwaongoza wenye kufuata radhi yake katika njia za salama (sio njia za upinzani), na huwatoa katika dhulma (shirki 31:13) kuwapeleka katika nuru kwa idhini yake na kuwaongoza katika njia iliyonyoka (5:16)

Uongozi ni nini?

Uongozi si mtu bali ni nyumba (inayoendewa) (5:2) kutafuta fadhila za Rais wao na radhi yake (5:2) (Na zingatia uone kwamba wenye kutafuta fadhila na radhi za kiongozi wao huyo) hupeleka katika nyumba hiyo wanyama wakachinjwe (5:2).

(Kumbuka) mababu zetu waliyaendea mapango au misitu (sehemu za faragha walizoziteua na kuziheshimu) (5:2) na waliandamana nao wanyama wa kuchinjwa (tambiko au kafara) (5:2) na walisaidiana kwa (wema 2:177) na hofu wala hawakusaidiana katika dhambi na uadui (5:2). Wakamlilia (Rais Muumba 39:6) wao kwa shida na matatizo yao. Kauli zao ilikuwa kitu kama hii:

"Eh!Mfalme Mungu - Mungu wa Babu zetu Kajia, Kajiru na Kisumo (linganisha 2:133) ni wewe tu tunayekujua unayetipisha jua angani - tusikie kwani sisi ni wajukuu wao - tumekukosea tu- tumekuja kukuomba".

Na wazee wetu walichokiomba hasa ilikuwa; mvua, kueupushwa na maradhi na watoto (19:5).

Hebu tuone wakati wetu huu: Zingatia kuwa kuta za mapango ni majabali. Je! Huoni kwamba sisi tulichofanya ni kuyaendea mapango (majabali) na kuyavunja vunja. Halafu tukahamisha mapango haya na kuyajenga mjini? Mara tukayabandika jina "nyumba" badala ya kuyaita "mapango ya kisasa". Na humo tukaweka vyumba, vikaitwa ofisi. Na ni ofisini humo tukajaalia (15:96) wenzetu kukaa humo kusimamia uwongozi wa katiba tuliyounda wenyewe. Tukawafanya viongozi (18:102) na wana majina kibao (12:40) kufuatana na wadhifa waliosomea.

Oh! Tuna shida na tatizo sasa. Moja kwa moja huyaendea mapango haya ya kisasa (1) ofisi ya chama au serikali kuomba fadhila ( kama maji) za viongozi tuliowasilimika. Na ili tupate Radhi zao lazima tutoe kitu kidogo (chakula cha mgeni rasmi na vinywaji). Kama shida hiyo ni ugomvi au kudhulumiana huenda kituo (nyumba) cha polisi - huyo Mahakamani. Kama ni maradhi huenda hospitali na kadhalika.

Na kote huko si bure ili upate fadhila (huduma) na radhi zao (msaada) lazima utoe hongo. Mfano utakuta watoza ushuru (wenye kuzitumikia 9:60) anakuambia ah! Ushuru wako ni milioni tatu. Una uwezo wa kulipa?

Sasa wewe pale unajililia eti akusaidie. Basi wewe unampa milioni moja lakini anakuandikia risiti ya laki nne. Ajabu nani amemsaidia mwenzake! Yeye au wewe?

Yote ni mamoja. Hawa tunaowamba wanahitajia vitu kwetu. Na kweli tumekuwa watumwa wao. Hapana maongozi ya mapango ya kisasa (ofisi za chama na serikali) ni dini hiyo. Utajuwaje?

Watu husema dini ni imani. Ikiwa imani ni dini basi jua kuwa ukisema ujamaa ni imani, umesema kuwa ujamaa ni dini. Na hapa ndipo kosa lilipozaliwa. Tukawa wenye makosa (khatiya). Kosa lenyewe ni hili:

Imani yetu hii kwa mfano ujamaa tuliyopambwa nayo nyoyoni mwetu tukaipenda na kuitia (kumbuka seti Benjamin); tuliichukua kutoka kwenye pango la kisasa (ofisi) la chama tawala. Ili hali Rais wetu wa ulimwengu mzima (1:1) ametuagiza wanadamu wote tukuchue mapambo yetu kutoka Misikitini (kwenye masinagogi) (7:31).

Pambo ni nini?

Sura ya 49 aya ya saba inatufahamisha kuwa kilichopendezeshwa kwetu ni imani na ndilo pambo la moyoni. Na usije kufa kabla hujalivaa pambo hilo (3:102). Kwa hiyo imani yetu twatakiwa kuichukua kutoka kwenye pango la kisasa liitwalo Msikiti (7:31) na sio ofisi. Jua kila ofisi ina katiba yake iliyoundwa na watu. Kwa hiyo maongozi yake ni ya kubuniwa na watu. Bali Msikiti nao unayo kitabu (katiba). Na kitabu hiki ni cha Rais wetu Allah (112:1) mmoja. Kwa katiba hiyo kufuatwa itapelekea kufuata maongozi ya Allah (5:16) ili atuongoze katika njia iliyonyooka (4:175), dini yetu aliyoisajili na kutupa kibali jinale Uislamu (5:3).

Kibla

Neno Kibla maana yake ni upande (2:177) unaoelekewa (2:150) kwa maongozi (3:96). Ajabu majumba haya ya Allah (72:18) (Misikiti) yote dunia nzima yameelekea (nyumba kongwe 22:29). Na huu ndio ukombozi wetu (nyumba tukufu 5:97) Rais wetu Allah (ameifanya 5:97) mji wa Makka ndio mji mkuu (mama wa miji) miji yote duniani ielekee huko (6:92).

Humo kipo kitabu (katiba) chenye baraka (9:62). Kwa hayo jua kuwa ofisi (Pango la kisasa) halali kuendewa kwa utatuzi wa shida na matatizo ya watu ni Msikiti. Yenyewe Misikiti hii imeelekezwa Makka. Nasi tuelekeze nyuso zetu huko (2:148, 150, 144, 143, 145) kwani hiyo ndiyo haki iliyotoka kwa Rais (Mola) wetu (2:147) na ndiyo aliyoteremshiwa Muhammad (13:1) na ndilo agizo aliloagizwa kufikisha (5:67).

--

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook