"Na Suleimani alimrithi Daaud na akasema: " Enyi Watu! Tumefundishwa (hata kutambuaaa) usemi wa ndege na tumepewa kila kitu, hakika hii ni fadhila iliyo dhahiri. Na alikusanyiwa Suleimani majeshi yake katika Majini na Watu na Ndege, nayo yakapangwa makundi-makundi (katrika kwenda kwake).
Hata walipofika katika bonde la wadudu chungu, alisema mdudu chungu (kuwaambia wenzie: "Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu , asikupondeni Suleimani na jeshi lake , hali ya kuwa wasikuhisini (hawana habari)".
Basi akatabasamu akilichekea nano lake, na akasema: "Ee Mola wangu! Nipe nguvu nishukuru neema yako uliyonineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kufanya vitendo vizuri uvipendavyo, na uniingize- kwa rehama yako- katika waja wako wema."
Na akawakagua ndege (na asimuone kidege Hud-hud), akasema "Imekuwaje mbona simuoni Hud-Hud au amekuwa si miongoni mwa wasiokuwapo (hapa leo)?"
Kwa yakini nitamuadhibu adhabu kali, au nitamchinja, au ataniletea hoja iliyowazi (ya kumzuilia kuja hapa leo).
Basi hakukaa sana mara (Hud-hud akafika) akasema (kumwambia Nabii Suleiman:- "Nimegundua usilogundua, na ninakujia hivi kutoka (nchi inayoitwa) Sabaa na (nakuletea) habari yenye yakini".
Hakika nimemkuta mwanamke anawatawalia, naye amepewa kila kitu (kinachohitajiwa katika ufalme) na anacho kiti cha enzi kubwa".Nimemkuta yeye pamoja na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu, Na Shetani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia njia (ya Kheri), kwa hivyo hawakuongoka".
(Shetani amewazainishia wasimsujudie Mwenyezi Mungu hakuna huyatoa yaliyofichikana katika mbingu na ardhi na huyajua mnayoyaficha na mnayoyadhihirisha. Mwenyezi Mungu ambaye hakuna aabudiwaye kwa haki ila Yeye, Mola wa (hiyo) Arshi tukufu. Akasema (Suleiman): "Tutatazama kama umesema kweli au umo katika waongo".
Nenda na barua yangu hii na uwafikishie, kisha uwaache, na utazame watarudishiana (maneno) vipi". (Yule Malkia akawakusanya mawaziri wake) akasema: "Enyi wakuu (wa baraza)! Hakika nimeletewa barua tukufu: Imetoka kwa Suleimani, nayo ni: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, mwenye kurehemu.
"Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu na hali ya kuwa mumekwisha kiusilimu".(Malkia akaongezea) akasema "Enyi wakuu! nipeni ushauri katika jambo langu hili, maana sikati shauri yoyote mkpaka mnihudhurie (muweko)".
Wakasema: "Sisi ni wenye nguvu na ni wenye vita vikali, na amri iko kwako, basi tazama ni nini unaamrisha."(Malkia) akasema: "Hakika wafalme wanapouingia mji (wa watu), wanauharibu na wanawafanya watukufu wake kuwa dhalili, hivi ndivyo wanavyofanya (daima)".
--
|
|