Umeme ni moja kati ya maendeleo makubwa yaliyopatikana katika karene ya 19. Imefikia hadi sasa hivi baadhi ya watu hawawezi kuishi bila ya umeme. Kwa kweli, umeme umeleta maendeleo makubwa hasa katika viwanda na mawasiliano. Bila ya umeme dunia hii leo ingekuwa tafauti kabisa!
Lakini umeme, kama ulivyo kimaumbile kuwa hauonekani, umekuwa pia haueleweki sana na hivyo kuwepo nadharia na imani nyingi zisizo na ukweli wowote. Kwa mfano, nimepata kuona kwenye gazeti moja wameandika eti mtoto mmoja alifariki dunia kwa kushika nguzo ya umeme! Hilo haliwezekani kabisa, labda iwe alikamata nyaya za umeme badala ya nguzo.
Nguzo ya umeme kama nia ya mti, haiwezi kupitisha umeme na kwa hivyo hata ukiigusa huwezi kuathirika, hata kama nyaya za umeme zimeigusa nguzo hiyo moja kwa moja, jambo ambalo si la kawaida. Na kama ni nguzo ya chuma, ndio kabisaa! Nguzo ya chuma ina uwezo mkubwa sana wa kupitisha umeme kuingia ardhini na kwa hivyo hata ukiigusa, umeme unapenda kupita kwenye njia nyepesi na kwa hivyo utapita kwenye nguzo yenyewe badala ya kupita kwenye mwili wako na kukuathiri.
Ni kwa sababu hiyo ndio maana ikawa ni muhimu kuunganisha na "Earth" kifaa chochote kile cha umeme. Yaani kwa usalama, chombo cha umeme kitumie plagi yenye pini tatu, moja ikiwa ni ya kuunganishwa na Earth au ground yaani ardhi. Hii ni kwa sababu, ikitokezea hitilafu na baadhi ya nyaya zikagusa zisipotakiwa kwenye chombo chako, umeme huo utapata njia ya rahisi ya kuingia kwenye ardhi badala ya kuingia kwenye mwili wako utakapokigusa. Kwa namna hiyo utanusurika kupata "shoti" ya umeme.
Chengine kisichoeleweka sana ni namna vifaa mbali mbali vya umeme vinavyochangia gharama za matumizi ya umeme. Wengine husema pasi "inakula" umeme zaidi; wengine wanasema kompyuta inakula umeme sana, n.k. Kabla hatujaeleza mchango wa vifaa mbali mbali kwenye bili ya umeme, kwanza tujifunze ni namna matumizi ya umeme yanavyopimwa.
Bili ya umeme huletwa kulingana na idadi ya "units" za umeme zilizotumika. Unit ya matumizi ya umeme ni kilowatt-hour ambayo inaandikwa kwa ufupi, kWh. 1 kWh ndio unit moja ya umeme. 100 kWh ni unit mia za umeme.
Balbu (bulb) ya umeme ya watt 100 (yaani 100W), inahitaji kuwashwa kwa jumla ya masaa 10 kuweza kutumia unit moja ya umeme. (Yaani, 100 watts x 10 hours = 1000 watt-hour = 1 kilowatt-hour). Ukiamua kutumia balbu ya umeme ya 60W, utaweza kuitumia kwa jumla ya masaa 16 na dakika 40 kuweza kufikisha matumizi ya unit moja. Kwa hivyo, ili kupunguza matumizi ya umeme, itabidi utumie taa za umeme zenye nguvu (power) ndogo hasa kwenye sehemu zisizohitaji mwanga mkali. Gharama unazozipunguza ni kubwa sana hasa kama unatumia taa nyingi za namna hiyo.
Kwa mfano, kama nyumbani kwako kuna taa 4 ambazo unazitumia kwa wastani wa masaa 6 kila siku; ukitumia balbu za 100W, matumizi yako ya mwezi yatakuwa 72 kWh (yaani, 4 bulbs x 6 hours x 30 days x 100 watts = 72,000 watts-hour = 72 kWh), yaani units 72; lakini kama utatumia balbu za 60W matumizi yako yatakuwa units 43.2 tu! Na kama utatumia balbu zenye nguvu ndogo zaidi basi matumizi yako yatakuwa madogo zaidi. Kwa mfano kwenye choo, au taa za usalama (security lights) zinazowekwa nje, kwa hizo inatosheleza kutumia balbu hata za 40W. Kupunguza umeme zaidi ni vyema kuepukana na taa zinazohitaji balbu zaidi ya moja. Na jamabo la uhakika zaidi ni kujaribu kuzima taa zote usizozihitaji.
Taa za umeme za kawaida zinazotumia balbu ukizilinganisha na taa za aina ya fluorescent (yaani zile zinazotumia tube ndefu), utakuta kuwa kwa nguvu sawa sawa za umeme ( kwa mfano zote ni za 60W), mwanga unaotolewa na taa ya fluorescent ni mkali na safi zaidi. Hata hivyo, bei ya taa za fluorescent ni ghali zaidi lakini kwa matumizi ya muda mrefu ubora wa taa za aina hiyo unazidi ule wa taa za kawaida zinazotumia balbu.
Kigezo pekee cha kujua kiasi cha umeme kinachotumiwa na kifaa chochote cha umeme ni nguvu (power) ya kifaa hicho ambayo hupimwa kwa kutumia "watt" (kwa ufupi "W"). Baadhi ya watu wanababaishwa na maneno "watt" inayotamkwa "wot", na "volt" (kwa ufupi "V") inayotamkwa kama ilivyo, yaani "volt". Wakati "watt" ni kipimo cha nguvu (power) ya kifaa cha umeme, "volt" ni kipimo cha uwezo (yaani potential au voltage) wa umeme wenyewe. Kwa hivyo unaweza kuona balbu ya umeme imeandikwa 60W, 240V, ikimaanisha kuwa ikiungwa kwenye umeme wenye uwezo wa 240V, balbu hiyo itatumia nguvu ya umeme ya 60W. Umeme wa Tanzania unaotumika kwenye nyumba wanazokaa watu una uwezo (voltage) wa 240V. Uwezo huo ni sawa kwa nyumba zote. Kwa upande mwengine, umeme unaotumika viwandani una uwezo (voltage) wa 400V.
Ili kukusaidia kujua ni kifaa gani kinakula umeme zaidi, hapa chini ni orodha ya baadhi ya vifaa maarufu vinavyotumia umeme, na nguvu (power) zao katika hali ya kawaida:
| Kifaa cha Umeme |
|
| Balbu ya kawaida ya umeme |
|
| Tube ya kawaida ya taa ya fluorescent |
|
| Radio |
|
| Radio-Cassette Recorder |
|
| Video-Cassette Recorder (VCR) |
|
| Televisheni ya rangi ya inchi 21 |
|
| Kompyuta |
|
| Blender |
|
| Pasi |
|
| Feni la kawaida |
|
| Element ndogo ya jiko la umeme |
|
| Element kubwa ya jiko la umeme |
|
| Element ya oven |
|
| Friji (Friza) |
|
|
|