BARUA
 
 

Masheikh Zanzibar vipi?

Ndugu Mhariri

HAPA Zanzibar dini ya Kiislamu imeshakufa au inataka kufa kwa kasi ya hali ya juu. Hali ambayo nimeizoea nilipokuwa Dar es Salaam ni kupata mawaidha kwenye Misikiti mbalimbali na mihadhara mbalimbali ikitolewa huko Tanzania Bara inayohamasisha dini na waumini.

Tangu kuja kuishi hapa Zanzibar sasa ni miezi kumi (10) sijawahi kusikia leo kuna mhadhara au leo katika Msikiti fulani atakuja mhadhiri toka pahala fulani kutoa mawaidha. Nilichokiona mimi ni kusali na kusujudu kwa muda mrefu, lakini uhamasishaji wa dini hakuna.

Misikiti yote Zanzibar hutoa hotuba za kufurahisha viongozi wa serikali na ambazo zimeshatayarishwa na kusomwa tu.

Vipi mtu msomi tena wa dini ya Kiislamu unatungiwa hotuba ya Ijumaa wakati kuna mambo kibao yanayofanywa ya uchafu kama changudoa wamezidi, vilabu vya pombe vimezidi, stoo bubu zimekuwa nyingi vichochoroni, Guest House, dhulma imezidi na mengineyo.

Baya zaidi hiyo siku ya Ijumaa baada ya sala hakuna mawaidha kana kwamba hapa Zanzibar watu wote wana elimu ya kutosha na hawahitaji ya ziada wala ukumbusho.

Inaonekana dhahiri hapa Zanzibar Masheikh wanaiogopa serikali na viongozi wake pamoja na Kanisa lakini sio Mwenyezi Mungu. Lakini Masheikh wa Bara wote takriban wanamwogopa Mwenyezi Mungu, kila siku wanatishwa na dola viongozi wa dola, Kanisa na wanafunguliwa mashitaka. Bado msimamo upo pale pale kwa hilo Bara nakupeni hongereni.

A. Jamal,
Box 310,
Zanzibar.



Uongo wa makafiri katika INTERNET

Ndugu Mhariri

MADHALIMU wametoa takwimu ya Watanzania kwa mujibu wa imani ya dini.

Takwimu hizo zinadai kuwa: Asilimia hamsini (50%) ya Watanzania ni wanaofuata dini za jadi (wapagani), asilimia arobaini (40%) ni Wakristo na asilimia kumi (10%) ni Waislamu!!!

Takwimu hizo ni za Septemba 27, 1996. Habari hizo zinapatikana kwenye Kompyuta (INTERNET) kwa anuani ifuatayo:htt://www.genesis.acu.edu/chowning/africa/fsha.htm.

M. Said,
Dar es Salaam.



Waalimu Waislamu wamekwisha?

Ndugu Mhariri

NIMESIKITISHWA sana na taarifa iliyotolewa katika gazeti hili la Aprili 23-29 toleo namba 198 yenye kichwa cha habari "Wanafunzi Waislamu wanyanyaswa ndani ya shule ya Kiislamu".

Jambo la kusikitisha na kushangaza ni kuhusu shule ya Kiislamu kuongozwa na mnaswara, inakuwaje? Si kuzuiwa kuswali, kuvaa stara na kutekeleza yale yanayowapasa wanafunzi hao wa Kiislamu? Nani wa kulaumiwa kama sio uongozi wa Kiislamu unaosimamia shule hiyo?

Hakika jambo hili halina tofauti na UWAWARU, tena ni la kukemea vikali na kufutwa kabisa; kwani Mwenyezi Mungu ameshabainisha katika Qur'an kuhusu jambo kama hili. Rejea sura ifuatazo:

"Enyi mlioamini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasiokuwa katika nyinyi, hao hawataacha kukufanyieni ubaya.


Tahadhari na ilani ya uchaguzi ya CCM 2000

Ndugu Mhariri

SHUKRANI kwako kwa kunipa nafasi hii.Ndugu Waislamu na wote wasiopenda dhulma. Serikali ya CCM imepokea malalamiko ya Waislamu juu ya dhulma wanayotendewa na vyombo vya serikali na Mheshimiwa Rais aliahidi kuwa atayafanyia kazi malalamiko hayo, lakini cha ajabu mpaka leo kimya ndio kwanza wanatafutwa walalamikaji ili watiwe nguvuni.

Si ajabu wameyaweka malalamiko ya Waislamu ili yawemo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM wa mwaka 2000 ili kuwalaghai tena Waislamu wawapigie kura.

Wito wangu kwa Waislamu wote na wengine wanaochukia dhulma tusihadaike na maneno matamu ya takayosemwa katika ilani hiyo maana tumeshajua kama ni mahodari wa kuahidi lakini si watekelezaji.

Hata kama wakitoa majibu ya malalamiko yetu na kuwachukulia hatua wauaji wa Mwembechai katika mwaka wa uchaguzi itakuwa ni geresha tu kwa Waislamu.

Uislamu wetu unatufundisha kutong'atwa na nyoka mara mbili katika shimo moja. Ikiwa mababu zetu wa Kiislamu walisaidiana kuuondoa ukoloni? Basi na sisi wajukuu tushikamane kuiweka nchi katika haki sawa kwa

njia ya demokrasia.
Ibrahim Sant,
Dar es Salaam.
--

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook