1 "Kila kitu huanza kidogo kidogo na baadaye huwa kikubwa isipokuwa majanga. Majanga huanza kwa ukubwa na baadae hupungua. Vile vile kitu chochote hupunguwa thamani pindi kinapokuwa kwa wingi isipokuwa kitu kimoja tu nacho ni tabia njema. Tabia njema inapokuwa nyingi kwa mtu basi huzidi thamani".
Hayo yamesemwa na Nasir Ibin Saiyar.
2. "Leo tumehitimisha vita vya Crusade"
Hayo yalisemwa na Lord Allenby Kamanda wa Jeshi la Uingereza baada ya kuiteka Palestina katika vita kuu ya kwanza ya dunia.
3. "Uko wapi we Salahudin. Sisi tumerejea".
Hayo yalisemwa na Kamanda wa Jeshi la Ufaransa walipouteka mji wa Damascas katika vita kuu ya kwanza vya dunia. Aliyasema hayo makaburini huku akilipiga teke kaburi la Salahudin.
Kuwa Salahudin Al Ayoubi aliwashinda Wakristo katika vita (Crusaders) vilivyoitwa HITTIN mnamo mwaka 1178 na akauteka (akaurejesha mikononi mwa Waislamu) mji wa Jerusalem ukiwemo Msikiti Mtakatifu wa Al-Quds. Pamoja na ushindi huo aliwaruhusu Wakristo, chini ya mpango maalum kuzuru sehemu zao za kidini ili wafanye ibada zao.
Baada ya kumaliza ibada ya Haji, Khalifa mashuhuri, Haroun Ar Rasheed alikwenda kuzuru Madina. Alipofika Madina alipenda asikilize Hadeeth za Bwana Mtume Sallallahu Aleyhi Wassalaam zikisomwa na Imam mashuhuri aliyeandika kitabu maarufu kiitwacho Al-Muwatta ambaye si mwingine isipokuwa Imam Malik. Hivyo basi Khalifa alimtumia ujumbe Imam Malik afike mahala alipo Khalifa na amsomee Hadith. Lakini Imam Malik alimwambia yule mjumbe; "Mwambie Khalifa ya kwamba ikiwa mtu anatafuta elimu basi ni juu yake aifuate, kwani elimu haimfuati mtu".
Kwa kukosa hoja zaidi Khalifa Haroun Ar Rasheed akaenda mahala Imam alipokuwa akifundishia. Na pale akaomba akae pekee pamoja na Imam ili amsomee Hadith. Imam alikataa ombi hili na akamjibu Khalifa kuwa watu wote ni sharti wakae duara katika darsa lake. Kwa maneno yake Imam Malik alimwambia hivi:"Pindi elimu itakapozuliwa kuwafikia watu, basi elimu hiyo haitakuwa nzuri na vile vile haitonufaisha watu walio juu kimadaraka au jamii iliyotukuka , nayo haitanufaika".
Khalifa Haroun Ar Rasheed alipogundua kuwa Imam hayuko tayari kutoa upendeleo wowote basi akaamua kukaa pamoja na wale wote waliohudhuria Darsa kujifunza kutoka kwa Imam.
--
|
|