BARUA
 

Mtume wetu ni kiigizo bora kwa kusimamisha sharia katika jamii yetu

Ndugu Mhariri

NAPENDA kutoa mchango wangu wa mawazo kwa barua ya Sheikh Bernard Shemweta wa S.L.P. 96 Korogwe iliyoandikwa katika gazeti la ANNUUR la tarehe Muharram 1420 sawa na tarehe ya Kirumi 14-20, 1999. Barua ilikuwa na kichwa cha habari kinachosomeka "Mdahalo wa kuhamisha mada".

Sheikh Bernard N. Shemweta hayuko sahihi katika maelezo takriban yote aliyoyaandika. Ameeleza kuwa Waislamu ni hodari kuhamisha mada kuliko makafiri (madhalimu). Sababu alizozitoa ni kwamba wanashindwa kabisa kuhudhurisha haki zao za msingi kwa Rais wa nchi inapofika wakati haswa wa kufanya hivyo.

Wanazoziona haki ni kupumzika siku ya Ijumaa, kuvaa hijabu, wanafunzi wa Kiislamu waende vyuo vya juu, kuwepo kwenye Parole, uwiano wa watendaji serikalini na lile la kudai Shariah isimame tunalikwepa.

Inadhihirisha kuwa mwandishi wa barua hii yeye ndiye hodari wa kuhamisha mada. Sababu ameshindwa kujua haki za kimsingi ni zipi kufuatana na mazingira yetu tuliyonayo.

Si vibaya nikisema hizi ulizoziandika ndizo haki za msingi na endapo Rais alizikubali basi ni bayana kuwa jamii ya Waislamu itapata maendeleo makubwa na hatimae kupunguza yale makelele ya dhulma dhidi ya jamii yetu. Ni kweli usiyopingika kuwa Waislamu hawana uhuru wa kuabudu kama inavyoelezwa katika katiba ya nchi. Na hili linafanywa makusudi siyo hapa petu Tanzania, bali ulimwengu mzima.

Jambo la kudai Shariah kwa makafiri isimame siyo kweli ingawa ni la msingi katika ibada zetu. Hawatakubali kupitisha bungeni shariah ya Kiislamu kwa ajili ya matumizi ya jamii yetu. Mtume wetu hakufundisha hata mara moja kupita njia hiyo. Mafundisho yake yako wazi kwa mfano haikuwezekana kusimamisha Uislamu Makka na ikiwapelekea Waislamu kuhama kutoka huko na kuelekea Abbysinia na Madina.

Waislamu walipata salama na amani katika Abbysinia na Madina kwa sababu mazingira yaliruhusu hivyo. Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, Mtume Muhammad (s.a.w.) alifaulu kusimamisha Shariah hapo Madina. Kwa nini alifaulu?

Hebu turejee Makka. Wakati huo Mtume (s.a.w.) alikuwa akishughulikia kuwajenga watu imani kwa muda wa miaka kumi na tatu. Wakati huo huo makafiri wa Makkah wakiendelea na ujahili wao dhidi ya ubinadamu na mafundisho ya Mwenyezi Mungu.

Tukirejea Madina, mazingira ya Madina yalitofautiana sana na Makka. Mtume (s.a.w.) wakati huo alikuwa anashushiwa shariah na jamii kubwa kabisa ikimuunga mkono.

Hali ya Tanzania haitofautiani sana hali iliyokuwepo Makka kwa wakati ule. Tazama Tanzania ni nchi inayoendeshwa kutokana na fikra za watu na inatenganisha siasa na dini. Nchi yoyote inayotenganisha siasa na dini haiwezi kuepuka ujahili bila ya hivyo hakuna kitakachokwenda mbele.

Historia yetu inatufahamisha kuwa Mtume wetu (s.a.w.) ndiye kiigizo chetu kilicho bora. Waislamu tumeshindwa kupata mafanikio yoyote kwani tumempuuza Mtume na kuwafanya makafiri viigizo vyetu.

Uislamu ni dini ya mipango. Tuanze kutayarisha mipango ya kuwa na Shuura, uhuru wa kutoa mawazo, utawala mzuri wa majimbo, kiongozi wetu mkuu, mabaraza ya kusimamia haki, elimu, usalama, hazina, kuangalia wasiojiweza, ujenzi wa Misikiti na shule/madrasa, ujenzi wa majengo ya maofisi na uanzishaji miji midogo midogo na hata miji mikubwa kama uwezo upo, kilimo na ufugaji, makazi ya watu na kadhalika.

Haya siyo mazito, kama nia ipo. Penye nia pana njia.

Aboubakari S. Marwillo,
P.O. Box 90242,
Dar es Salaam.


Waislamu hatuko tayari kushangilia dhulma

Ndugu Mhariri

KATIKA harakati za kuondoa dhulma ya ukoloni mamia ya Waislamu wakiwemo Masheikh mbalimbali walishiriki kikamilifu kudai uhuru. Lakini mara baada ya kung'olewa ukoloni ndipo dhulma ikaanza baada ya kundi la wachache kukabidhiwa madaraka.

Masheikh mbalimbali walifungwa, dhulma ikaanza katika elimu, ajira na sehemu nyingi. Mambo yakazidi kuwa mabaya watu wakanyang'anywa mashamba, mali zao na rushwa ikakithiri mpaka leohii ni ajabu na ni mtihani mkubwa kwa nchi masikini kama Tanzania kuwemo karika orodha ya nchi zinazoongoza kwa rushwa duniani.

Wananchi wanabebeshwa mizigo ya madeni wake kimya wafunge mikanda na hiyo ndio amani na utulivu, huku madawa hakuna, barabara mbovu, hata tunapolazimishwa tuseme eti pombe asili yake Tanzania. Tukaye kimya tu.

Na hata kama dini ni imani lakini sio kila imani ya kweli ni ile ya Mungu mmoja tu hana mtoto wala mshirika. Haiwezekani mtu au jabali likawa mungu eti kundi au kabila fulani ndio imani yao. Wote wenye imani kama hizo hawana dini.

Baddy Bashiri Kivinje,
Kilwa Masoko,
Tanzania.

--

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook