MAKALA
 
Anayeuliza 'Waislamu wanadai nini' hana tofauti na Czar Nicholai wa II
 

Na A.S. Chachika

SIKU za nyuma Waislamu walipokuwa wananyanyua sauti kudaihaki zao, lugha iliyokuwa inatumika kuwakatisha tamaa ilikuwa: "Hao ni Waislamu wa siasa kai. Au ni Mujahidina au ni wakorofi wachache". Kwa vile ihlo halikuwa sababu ya kuwafanya Waislamu wasidai haki zao, basi kazi ya kudai iliendelea siku hadi siku. Wale wasiowatakia heri Waislamu sasa wamebadilisha lugha. Lugha mpya ni: "Kwani Waislamu wana dai haki zipi?" Watu wa aina hiyo kama watakuwa miongini mwa wale waliokabidhiwa dhima ya uongozi wa raia wa nchi, wawe wa ngazi za chini, kati au juu, basi hao wanajifananisha na Czar Nicholai II aliyekuwa Mfalme wa Urusi kabla ya Ukomonisti.

KAWAIDA ya wafalme wengi ni kutokuwa na maingiliano ya karibu na raia. Mara zote hutegemea taarifa za wapambe na Maziri. Lakini kwa kawaida wapembe na Maziri daima hawawi kiungo kizuri kati ya wafalme na raia. Mara zote humpa mfalme taarifa ziel za kumpendeza tu. Hali ilikuwa hivyo kwa Nicholai II ambaye mara zote alikuwa ghorofa ya juu na malkia wakifurahia maisha.

Wakati fulani ilitokea njaa na raia wakahangaika sana kwa kukosa chakula. Mfalme hakuwa na habari sahihi juu ya watu wake. Siku moja wananchi wakaamua kuandamana hadi katika viwanja vya kasri ya mfalme ili angalau mmoja wao apaze sauti na kumwambia kuwa wana njaa na nchi haina chakula.

Malkia alistushwa sana na msongamano wa watu katika viwanja vya kasri akauliza: "Wanashida gani wale?" Akajibiwa kuwa hawana mkate". Kwa maana ya kuwa wana njaa na wamekuja kwa mfalme ili awaokoe. "Kama hawana mkate si wale keki!" Hali hiyo ilidhihirisha namna gai familia hiyo ya kifalme ilivyokuwa haina habari na raia wa nchi ile.

Kwa upande wetu sisi Waislamu wa Tanzania swali letu ni tofauti kabisa na lile la Malkia. Sisi tunajiuliza, Hivi ni kwelii kwa dhati kabisa yuko Mtanzania mwananchi au kiongozi wa ngazi ya chini, kati au juu ambAye hajui kuwa Waislamu wanadai haki zipi za kikatiba? Kama wapo basi wanaishi ghorofa ya juu na ni nadra kwao kuonana na Watanzania wa kawaida. Hawana tofauti na Nicholai II.

Ni hatari iliyoje kama tutafanya tumaini na kukubali kuwa kuna mtu hafahamu madai yetu. Tukifikishwa hapo tutakuwa tumesaidia kufanikisha lengo la mbinu inayoandaliwa juu yetu ya ucheleweshaji (delaying tactic) ili tuache kuendelea kudai tuanze kazi mpya ya kutafsiri mana na aina ya madai huku wenzetu wakiendeleza harakati za maendeleo yao.

Kila mmoja anaona wazi kuwa tumeweka bayana madai yetu na kwa ushahidi ulio na reje zenye takwimu za uhakika. Hakuna upenyo wa kukwepea ushahidi huu. Linalofanyiwa kazi hivi sasa ni kutumia mbinu za ucheleweshaji au kuundiwa mbinu na kutolewa katika mkondo na kuelekezwa kushoto, kuundiwa agenda mpya ili tujishughulishe na kutafsiri, kutoa takwimu za kisayansi ili tuzidi kuchelewa wakati wenzetu wanapiga hatua katika maendeleo yao.

Waislamu tusidanganywe na ahadi zisizotekelezwa. Kitendo cha kuundwa umoja na kufanyika baraza la Idd ya Mfungo mosi mwaka huu lililokufanya jumuiya mbalimali na kumkabidhi Mheshimiwa Rais risala yenye madai ya Waislamu; na Rais kuipokea na kuahidi kuishughulikia, kusitufanye tukalala usingizi mnono na kuamini kuwa sasa tumemaliza kazi. Je, ni kweli madai yetu yamepokelewa? Je, risala ile haikuwa kama "nakala halisi" ya Waraka wa Sheikh Ponda? Mbona waraka wake ulipofika mikononi mwa serikali akaanza kusakwa kama vile wakulima wanavyosaka ngedere walioiba mahindi shambani mwao?

Lakini jambo la kutafakari zaidi pia ni ile kauli ya Mheshimiwa Rais kuwa ameyasikia malalamiko yale na kwa mara ya kwanza pale pale katika kusanyiko la baraza la Idd na kwa mantiki hiyo akaomba apewe muda ili akayatafakari pamoja na wenzake katika Baraza la Mawaziri. Hili la pili ni jambo la msingi a katika utekelezaji wa uongozi wa pamoja. Tunampongeza.

Lakini pia tunayo haki ya kuwapongeza na kuwashukuru na zaidi kuwaombea dua wale waliokuwa waasisi wa kuratibu madai hayo. Wako wengi lakini itoshe tu kusema kuwa, tunaamini Waraka wa Sheikh Ponda ulikwisha fika serikalini. Waraka wa Abu Azizi umekabidhiwa kila kiongozi wa serikali na taasisi zake na taasisi binafsi. Barua za Baraza Kuu ziko Ikulu na ofisi zote zilizokusudiwa zipate. Tuna kumbukizi hadhahiri kuwa yaliyo katika risala ya baraza la Idd ni 'nukuu' za kutoka nyaraka hizo za Mabwana hao. Mkalafu gani ambaye habaini kuweko hila katika suala hili?

Pamoja na hayo tutaaacha kuyakariri madai yetu madam ndimi zetu bado zina uwezo wa kutamka. Kimsingi Waislamu hawadai Utume wala ufalme. Wanataka haki yao ya kuishi kwa njia sahihi ya maisha (Uislamu) ili waweze kutekeleza lengo la kuumbwa kwao. Wanataka haki ya uraia ya kupata huduma za kikatiba kama raia wengine. Wanataka hisa yao kamili katika kulisimamia na kuliendeleza taifa hili kwa ushirikiano wa midhati na wenzao. Ni hakimu gani mwalidifu atakayehukumu kuwa madai hayo sio sahihi?

Ni shahidi gani mkweli atakayekataa kushuhudia kuwa: Tulipokuwa tunaombwa kura tuliahidiwa kurejeshewa makakama za makadhi. Sasa muhula unaisha. Hatujui safari hii tutaahidiwa nini! Kwamba mabinti zetu wanazuiliwa kuvaa stara na kulazimishwa kwenda vichwa wazi wakati wenzao katika Ukatoliki na Uanglikana wanafunika vichwao vyao.

Kwamba nchi haina dini lakini kwa wenye kuona wanaona kuwa ina mwelekeo wa Kanisa lile lililopewa fursa nzuri. Sungusungu walichaa Qur'an tukufu ikawa si lolote si chochote. Kuvunjwa kwa bucha ya mfanyabiashara pale Magomeni kulifanya kuwa ni jinai kati ya serikali na Waislamu wa nchi nzima badala ya kuwa ni daawa ya mvunjaji na mvunjiwa.

Na kwamba FFU ilitumika kwa Waislamu wakati walioua na kuchoma majumba na kuharibu mashamba kule Meru (Wakristo) walipelekwa wasuluhishi kutoka CCM. Kwamba Waislamu wameuawa na serikali kwa kutumia askari na risasi zilizonunuliwa kwa kodi zao ii kuwalinda na kulinda nchi yao na sasa yaonekana serikali hii kama kuna kinachowakera.

Viongozi wanaendelea na kustarehe kwa mvinyo. Ni mwanasheria mgani mtaali atakayesema Waislamu hawana haki ya kulalamika? Ni moyo wa nani ulio mgumu kiasi hicho hata usione huruma kwa adha hizo na kusaidia kuziondoa au kuzikemea au hata kuzichukia tu, kama wapo watu wa aina hiyo, Mwenyezi Mungu atuepushe na kundi hilo. Basi hao hawaishi katika ardhi hii ya Tanzania. Wako ghorofa za juu hawana tofauti na Czar Nicholai wa II.

Nasi tutayatumia mavune haya ili ifikapo elfu mbili tuwe tumeshikana pamoja. Yetu ni subira njema kwa Allah (s.w.), kumcha Yeye na kushikamana katika kamba yake wala tusifarakane. 
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook