Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya Waislamu wamemtaka Mchungaji Mtikila asipate taabu kuomba msaada wa polisi bali aende tu akautwae Msikiti Masjid Mwinyi na kuufanya Kanisa kama anavyotaka.
Wamesema Mchungaji Mtikila hana sababu za kuwa na hofu kwani hao watu wa kuhofia hawapo ndio maana hata yeye mwenyewe kashawishika kuutwaa Msikiti wao.
Maoni hayo yametolewa kufuatia hatua za Mchungaji Mtikila kuwataka waumini wa Msjidi Mwinyi waondoke Msikitini hapo kwani keshauziwa Msikiti huo.
Katika taarifa yake kwa waumini hao Mtikila amesema kwamba kuanzia Ijumaa ya leo Msikiti huo unasafishwa kwa ajili ya Ibada takatifu. Aidha, akawataka waumini hao (baada ya kukubali Msikiti wao uwe Kanisa) wawe huru kushiriki Ibada za Kikristo zitakapoendelea hapo.
Taarifa hiyo ya Bw. Mtikila Kumb. No. FSC/PWC/99/2 ya Juni 15, imetahadharisha kwamba lau Waislamu hao hawaondoka kwa hiari, nguvu za dola zitatumika. Kama kuwafanya wakae tayari tayari taarifa hiyo zimepelekwa nakala zake kituo cha polisi Msimbazi na kile cha Mtaa wa Pangani Ilala (Police Post).
Waumini wengi waliohojiwa na gazeti hili baada ya taarifa hizo wamesema kwamba maadhali inafikia hatua hiyo Mtikila ana haki ya kuuchukua huo Msikiti.
Wakifafanua walisema maadhali Waislamu wamekuwa katika hali ambayo mtu ameshawishika kwamba anaweza kuwafukuza Msikitini kwao au akapora mali zao za wakfu, basi Mtikila hana kosa kudai Msikiti Masjidi Mwinyi kwamba ni mali yake. Kwani wangekuwepo wenyewe wala isingempitia akilini kuandika barua hiyo, Bwana Harith Salim ambaye alijitaja kwamba ni mkazi wa Mwembechai alisema kwamba hata hivyo Mtikila ameonesha uungwana kuugeuza Msikiti Kanisa angeweza kufanya kilabu cha kuvumbua dhahabu na kuuza mishikaki ya kiti moto.
Bwana mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Abu Hafsa ambaye ni mswaliji wa Masjid Qiblatain alisema anasubiri Ijumaa (leo) asikie Masheikh watasema nini katika khotuba zao.
Bw. Harith alisema anashindwa kuelewa mantiki ya baadhi ya watu kumlaumu Mtikila, wakati wenye Msikiti wao na nyumba zao za wakfu (Waislamu) ndio waliomfikisha Mtikila katika hatua hiyo aliyofikia.
Msikiti anaoutaka Mtikila
ni moja ya nyumba zilizoachwa Wakfu na Hajat Aziza bint Omar
--
|
|