Sasa ni jino kwa jino - Sheikh Zuberi
 

SHEIKH Ahmed Zuberi wa Dodoma amewaambia Waislamu kuwa wakati wa kupigwa kofi katika shavu la kulia kisha ukamgeuzia adui na la pili akuchape vizuri umekwisha.

Sheikh Ahmed ambaye ni Imam Mkuu wa Masjid Nunge amesema sera hizo za unyonge na udhaifu hazikubaliki kwani Allah (s.w.) amesema "Jino kwa jino". Ikimaanisha kwamba Muslamu hatakiwi akubali kuonewa bali apambane kutetea heshima yake na haki zake zote ilimuradi havuki mipaka.

Akiongea katika hafla moja ya Kiislamu mjini Dodoma hivi karibuni Sheikh Ahmed Zuberi alisema kwamba kutokana na nguvu za dola walizo nazo, viongozi wengi wamekuwa na jeuri na viburi.

Akirejea mfano katika historia Sheikh Ahmed Zuberi aliwataja akina A'ad, Firauni na Namrudha' kwa jinsi walivyoonesha takaburi.

Hata hivyo Sheikh Ahmed alionesha kwamba kibri na jeuri ya viongozi haiwezi kushinda nguvu ya wananchi. Alisema kwamba mshikamano wa watu uliweza kuzishinda jeuri za akina Firauni na wengine.

Naye Sheikh Abdallah Ally aliye Imam Masjid Qubaa aliwataka Waislamu kujitoa muhanga kuutetea Uislamu kama walivyofanya Waislamu waliotangulia.

Aidha, Sheikh Ally alihimiza umoja na mshikamano wa Waislamu wote.

Hafla hiyo iliyokuwa ni kumbukumbu ya mashujaa wa Kiislamu ilihudhuriwa na Balozi Ahmed Diria kama mgeni rasmi. Balozi Diria aliye Mbunge wa Jimbo la Rala Leo (CCM) aliwataka Masheikh wajizatiti kutoa elimu kama walivyokuwa Masheikh wa awali. 
--

Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook