NINI magonjwa na husababishwa na nini. Maelezo ya aina mbalimbali yaweza kutolewa kuhusu vitu vinavyosababisha magonjwa. Maelezo hayo hutegemea mazingira na maarifa ya watu.
Baadhi ya watu wa vijijini wanaweza kusema mtoto anaharisha kwa sababu ya meno ya nailoni, kwa sababu bibi au babu yake hajatambikiwa au kachukuliwa msukule.
Bwana afya kwa ugonjwa huo huo anaweza kusema mtoto kaambukizwa ugonjwa huo kutokana na mazingira machafu yasiyo na vyoo pamoja na maji masafi ya matumizi ya nyumbani.
Kwa upande wake Mwalimu anaweza kusema kuwa yote haya huletwa kwa kutokuwa na elimu.
Huwezi kuyatibu vyema magonjwa au kujikinga nayo kama huelewi yanatokana na nini na yanaenezwaje.
Magonjwa yote yanaweza kugawanywa katika makundi makubwa mawili; Magonjwa yanayoambukiza na yale yasiyoambukiza. Magonjwa yasiyoambukiza hayaenezwi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, kinyume chake ni yale yanayoambukiza.
Yafuatayo ni baadhi ya magonjwa yasiyoambukiza. Ugonjwa wa moyo, kifafa, mtoto wa jicho na ugonjwa wa kansa. Magonjwa haya yanatokana na kitu kilichokosekana au kuharibika mwilini.
Mengine ni yale yatokanayo na madhara yaletwayo na vitu vilivyoko kwenye mazingira ambayo hudhuru mwili. Mfano allegies, pumu, sumu, vidonda vya tumboni, kikohozi kiwashacho kutokana na uvutaji wa sigara na kadhalika.
Magonjwa mengine yasiyoambukiza ni utapiamlo, upungufu wa damu, uvimbe wa shingoni (goitre) na ugonjwa wa ini (cirrlosis). Magonjwa haya hutokana na madhara yaletwayo na upungufu wa kitu ambacho huhitajiwa na mwili.
Magonjwa mengine ni yale
ambayo mtu huzaliwa nayo kama kifafa na makengeza. Aidha magonjwa ya akili
(wendawazimu) nayo hayaambukizi.
--
|
|