Muhadhara wahamia Mahakamani Mwanza
 

Na Abdul-Aman Swed, Mwanza
 

KATIKA kesi ya tuhuma za kuukashifu Ukristo huko Sengerema Mkuu wa Kituo cha Polisi Katunguru amekiri kuifikisha kesi hiyo mahakamani kama Mkristo mtetezi wa Kanisa lake.

Mkuu huyo wa Kituo cha Polisi Koplo John aliyasema hayo Juni 28, mbele ya Hakimu E. Raphael washitakiwa walipotaka kujua anamuwakilisha nani; "Ninawakilisha Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ambayo ndiyo mlalamikaji na pia kama Mkristo mtetezi wa Kanisa langu", alijibu Mkuu huyo wa Polisi.

Ikiwa imefurika wananchi mahakama ya Wilaya Sengerema iligeuka kuwa uwanja wa mhadhara pale mahakama ilipotaka viwasilishwe vielelezo vya kuthibitisha 'kashfa'.

Wanaotuhumiwa katika kesi hiyo ni Athmani Thomas Manoni, Hussein Abdallah Twalib Abdallah na Ramadhani Shabani. Wengine ni Idd Rashid; Hussein Omar, Abubakar Kabunda na Issa Rashid.

Kesi hiyo itasikilizwa tena Julai 6, 1999 ambapo Hakimu amesisitiza mashahidi wote wafike bila kukosa.

Wakati huo huo, Waislamu wa kike na wa kiume wa mjini Sengerema na vitongoji vyake wamelaani vikali unyama uliofanywa na polisi wa serikali ya CCM pale Mwembechai baada ya kuona kanda ya Mwembechai katika Msikiti wa Ijumaa Sengerema.

Aidha, Waislamu hao waliitaka serikali iwachukulie hatua za kisheria wale wote waliohusika na mauaji ya Mwembechai.

Akizungumza katika onyesho hilo Sheikh Idrisa Wasiqa aliwatahadharisha Waislamu na propaganda za vyombo vya habari na kusisitiza mshikamano mwaka 2000: "Tusiwape kura zetu madhalimu kwani malipo yao ni risasi", alisema.
 
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook