Mafundisho ya Qur'an
Uchambuzi wa hoja za Wapinzani wa Qur'an
 

Hii ndio hoja anayotoa Mwenyezi Mungu:

"Lakini lugha ya yule wanaemuelezea ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu bulbul (16:103) Makafiri wa Kikureishi walikuwa wanatangaza kuwa Muhammad hakupokea wahyi bali anafundishwa na Jabr ambae alikuwa muhunzi wa Kirumi1 aliyekuwa Mtume wa baadhi ya Makureishi. Pamoja na hoja hii Mwenyezi Mungu anaonya kuwa:

"Hakika wale wasioamini Aya za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hawaongozi. Basi watapata adhabu iumizayo: (16:104) Wanaouzua uwongo (wakipita wakitangaza kama hivyo kusema hayo Mrumi) ni wale wasioziamini aya za Mwenyezi Mungu na hao ndio waongo. (16:105).

Maelezo haya hayahitaji kushereheshwa hivyo ni dhahiri wapingao Qur'an ndio waongo na hoja zao ni duni.

Dai kuwa Mtume ni mwendawazimu pia limekanushwa na Qur'an

Hoja yao nyingine ni ya kumtukana Mtume kuwa ni mwendawazimu (44:14). Na walisema (kwa istihizai, 'Ewe uliyeteremshiwa mawaidha! Hakika wewe ni mwendawazimu' (16:6). Dai hili limekaririwa katika (13:47); (23:70, (34:8), (37:36), 44:14) na 68:51 isemayo:

Na wale makafiri hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanaposikia mawaidha (yako) na husema: "Hakika yeye ni mwendawazimu (68:51).

Dai hili kama madai mengine Mwenyezi Mungu analijibu. Je, hawafikiri (wakaona kuwa) mtu wao huyu (yaani Nabii Muhammad) hana wazimu. Hakuwa yeye ila ni muonyaji aliyedhahiri (7:184).

Kwa Neema ya Mola wako wewe si mwenda wazimu (68:2) na aya nyingine nyingi zinazokanusha; kwa mfano; Basi karibuni hivi utaona na wao pia wataona. Ni nani mwenye wazimu miongoni mwenu (67:5-6).

Dai hili nalo halikufanya kazi waliyoikusudia hivyo makafiri wakaibua dai la uchawi. Kuwa Qur'an ni uchawi.

Zimeghafilika nyoyo zao. Na wanasemezana kwa siri wale waliodhulumu (nafsi zao wanaulizana hivi). Ni nani kama ninyi? Je, mnafia katika uchawi na hali nyinyi mnaona? (21:3). Haukuwa huu ila ni uchawi uliodhahiri (34:43). Na ulipowajia ukweli walizua, "Huu ni uchawi na hakika sisi tunaukana (43:30). Dai hili linaendelea kutajwa katika sura (46:7; 61:6) na wanaposema kuwa, "Na wakasema; hayakuwa haya ila ni uchawi ulionukuliwa. (74:24).

Katika aya hizi Mwenyezi Mungu anaonyesha Qur'an "ukweli" ni "alama zilizowazi" (bayyinat) na alama dhahiri (bilbayyinat) na kuwa sio uchawi. Lakini Makafiri wa wakati ule na wa leo wameshindwa kutetea hoja yao ila kudai kuwa Qur'an ni uchawi (sihrum-mubin); sihafun-y'sur) udhaifu wa pili wa Dai hili ni lile tangazo la Mwenyezi Mungu lisemalo, 'Wala si kauli ya mchawi.

Lakini makafiri hawa wakaongezea dai linaloambatana na uchawi, sasa wanasema na Mtume mwenyewe amerogwa.

Tunajua sana sababu wanayokusingizia, na wanaponong'ona, wanaposema nao madhalimu "Ninyi hamfuati isipokuwa mtu aliyerogwa (17:47).

Jibu la dai hili Analitaja Allah (s.w.) kuwa, "Tazama jinsi wanavyokupigia mifano (ya uwongo mara amerogwa, muongo n.k.). Basi wakapotea hivyo hawawezi kupata njia (ya kuwapeleka katika haki). (17:48). Na huu ndio uduni wa dai lao hili.

Katika hali hiyo ya kutapatapa mara hivi mara vile na kama vile kurogwa ni dai jepesi, basi makafiri wameibua dai lingine kuwa Qur'an ni maneno ya shetani.

"Wala mashetani hawakuteremka nayo (hii Qur'an kama wanavyodai makafiri (26:210) wala haiwi kwao (kuiteteremsha Qur'an) na hawawezi (26:211). Katika kisisitiza kuwa Qur'an sio kazi ya shetani Mwenyezi Mungu anafafanua:

1). Naapa kwa nyota zinazoanguka

2). Kwamba mtu wenu (Muhammad) hakupotea wala hakukosa

3. Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake

4. Hayakuwa haya ila ni wahyi uliofunuliwa (kwake)

5. Amemfundisha malaika mwenye nguvu sana... (53:1-10).

Na bila shaka Qur'an ni uteremsho wa Mola wa ulimwengu wote. Ameteremsha haya mhuisha sharia muaminifu (Jibril) juu ya moyo wako ili uwe miongoni mwa waonyaji (26:192-194).

Sema: "Roho mtakatifu (Jibril) ameiteremsha kutoka kwa Mola wako kwa haki..... (16:102).

Ni dhahiri basi Qur'an sio kazi ya shetani. Ukiachilia mbali dai la kuwa ni kazi ya shetani, makafiri wameendelea na kutapatapa kwao na kudai Qur'an ni ndoto zilizovurugika (adghasu ahlam).

Lakini (makafiri) walisema (hayo anayosimulia) ni ndoto zilzovurugika..... (21:5). Dai hili nalo halina ukweli kabisa.

Dai lingine ni la ushairi. Makafiri vile vile walidai kuwa Qur'an ni mashairi.... Bali huyu ni mtunga mashairi tu..... (21:5).

Na husema Oh! Tuiache miungu yetu kwa ajili ya (huyu) mtunga mashairi mwendawazimu? (37:36). Kutumia dai hili Mwenyezi Mungu anaonya kuwa... Basi naapa kwa mnavyoviona na msivyoviona. Kwa hakika hii ni kauli iliyoletwa na mjumbe (wa Mwenyezi Mungu) mwenye heshima (kubwa) wala sio kauli ya mtunga mashairi (kama mnavyosema) ni sehemu ndogo sana mnavyoamini.

Ni uteremsho utokao kwa Mola wa viumbe wote (69:38-43) (69:38-43).

Mwisho wa yote makafiri wamedai Qur'an kaitunga Muhammad au ndio wanasema kuwa hii Qur'an ameitunga (yeye Muhammad) bali wao hawaamini lolote (52:33).

Dai hili limejibiwa kama ifuatavyo. Kwanza Mwenyezi Mungu anawataka wanadamu waifikiri Qur'an ilivyo kama inaweza kutoka kwa wanadamu. Je, hawakuifikiri kauli (hii Qur'an)? (23:68). Hawaizingatii hii Qur'an au nyoyoni mwao mna kufuli? 47:24. Baada ya Mwenyezi Mungu kuwataka wanadamu waifikirie Qur'an, anawajibu kuwa kama haitoki kwake basi wangekuta hitilafu nyingi (4:82).

Pamoja na nasaha hii lakini mwanadamu amezidi ubishi ndipo Mwenyezi Mungu alipomtaka mwanadamu atoe sura moja iliyomfano wa Qur'an kwa kusaidiana na wanaoweza kuwaita (10:38). Hawaizingatii hii Qur'an au nyoyoni mwao mna kufuli? (47:24). Baada ya Mwenyezi Mungu kuwataka wanadamu waifikirie Qur'an, anawajibu kuwa kama haitoki kwake basi wangekuta hitilafu nyingi (4:82).

Pamoja na nasaha hii lakini mwanadamu amezidi ubishi ndipo Mwenyezi Mungu alipomtaka mwanadamu atoe sura moja iliyomfano wa Qur'an kwa kusaidiana na wanaoweza kuwaita (10:38) changa moto ya sura moja inatajwa tena katika sura ya pili aya ya ishirini na tatu (2:23) na kuongeza kuwa wanadamu wawaite waungu wao mighairi ya Mwenyezi Mungu. Sura ya (11:13) inawataka watoe mfano wa Qur'an, (11:13) na sura ya (52:33) inawataka wanadamu na washirika wao watoe hadithi inayolingana na Qur'an.

Baada ya changamoto hii, Allah (s.w.) mjuzi wa muweza wa yote anatangaza katika sura ya (2:24) kuwa:

Na usipofanya na hakika hautafanya kamwe - basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe, uliowekewa makafiri (2:24). Sura ya 17 aya ya 88 inataja watu na majini kuwa hawataweza kutoa mfano wa Qur'an. Changamoto (challenge) hii ilibaki hadi katika miaka 23 ya utume wa Mtume Muhammad na iko hai na itabaki hai milele ndio maana Allah anatangaza kuwa:

Na haiwezekani kuwa hii Qur'an isitoke kwa Mwenyezi Mungu..... (10:37).

Dai lingine la ajabu ni pale makafiri walipotaka waletewe Qur'an nyingine au ibadilishwe kidogo. Dai hili ambalo limo katika sura ya (10:15) linajibiwa na Allah (s.w.) Anapomwambia Mtume wake kuwa sema, siwezi kuibadilisha kwa khiyari ya nafsi yangu; sifuati ila yaliyofunuliwa kwangu. Hakika mimi naogopa nikimuasi Mola wangu, adhabu ya siku iliyo kuu." (10:15). 
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook