BAADA YA KUZIDIWA
CCM kuanza rasmi siasa za kihuni
 

Na Mwandishi Wetu
 

CHAMA cha CCM kimetangaza kuanza rasmi kupambana na wapinzani wake katika medani ya siasa kwa njia za kihuni.

Aidha, Chama hicho kimedai kuwa wana CCM ndio wenye uwezo wa kuviamrisha vyombo vya dola vimuweke ndani nani

Aidha, Chama hicho kimedai kuwa wana CCM ndio wenye uwezo wa kuviamrisha vyombo vya dola vimuweke ndani nani na yupi vimwache. Kwa ajili hiyo kimewaagiza vijana wa CCM wawacharaze bakora wafuasi wa CUF na wale wenye ndevu ndefu.

Waislamu hasa wenye kufungamana barabara na suna ya Mtume (s.a.w.) juu ya ndevu na sharubu ndio wenye utambulisho wa ndevu ndefu.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni juzi huko Manzese, Katibu Mwenezi wa Chama hicho Wilaya ya Kinondoni Baraka Konisaga alisema kuwa ametumwa (na CCM) awaambie wana CCM kuwa wawashughulikie na wala wasiogope kwani serikali ipo chini yao; na kwamba watangaze rasmi kwamba sasa ustaarabu umeishinda CCM wanapambana kihuni.

Katika kutekeleza uhuni huo, Katibu huyo Mwenezi wa CCM ndipo amewaagiza wafuasi wa CCM wakiona watu wenye ndevu ndefu wawashughulikie.

Aidha, Katibu huyo alidai kuwa CCM ina taarifa kuwa wafuasi wa CUF watafanya fujo siku ya Ijumaa (leo) katika maeneo kadhaa Jijini.

Wananchi waliotoa maoni yao wamesema kuwa taarifa hii ya Katibu Mwenezi wa CCM ni nzuri kwani imetoa picha halisi ya mtizamo na mwelekeo wa chama hicho kwa wananchi wake.

Wamesema tatizo ni pale mtu anapojivika kilemba cha ukoka cha ustaarabu, udugu, uadilifu na malaika wa amani na utulivu asie na ubaguzi, lakini katika hali hii ya uwazi wananchi hawatatiziki.

Akitoa maoni yake baada ya mkutano huo, Bw. Saidi Omar wa Manzese alidai kuwa wananchi wapo kudai kile wanachoamini ni haki yao wanayoporwa na kwamba CCM inafanya kosa kubwa kunasibisha vuguvugu la wananchi na siasa za vyama.

Kwa kosa hilo alisema CCM kwa kutumia serikali yake yaweza kuidhibiti CUF na kuwacharaza bakora wote wenye ndevu, hata ikibidi kuwaua, lakini hiyo haitositisha wimbi la madai ya wananchi. "Wataendelea kusonga mbele hata wakiona wenzao wameuliwa", alisema Bw. Saidi.

Baadhi ya wachunguzi wa mambo wamesema huenda taarifa hiyo imekusudia kujenga mazingira ya kuendesha operesheni ya kukamatwa wafuasi wa CUF kabla ya siku ya uchaguzi ili kupunguza idadi ya wapiga kura. 
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook