DONDOO YA HISTORIA
 
Machozi ya Mwalimu Nyerere yalikuwa ...
 

Na Abubakar Msham
 

Ninapenda kuanza kwa kuirejesha jamii hadi pale Lumumba mjini Dar es Salaam, kwenye kikao cha Halmahauri Kuu ya TANU, wakati aliposimama ghafla Shujaa wa Uislamu, Marehemu Sheikh Suleiman Takadir huku akiielekeza bakora yake kwa Mwalimu Julius K. Nyerere. Marehemu Sheikh Takadir alitamka, "Huyu, katu hatakuja kutujua ndugu zake. Usipoziba ufa utajenga ukuta." Kilichofuatia ni kilio, ati Malimu Nyerere akalia machozi kisha akauliza iwapo Sheikh Takadir alisema maneno yale kwa niaba ya Waislamu. Wote (Waislamu) walikataa, mkutano haukuendelea tena na ndio ukawa mwanzo wa fitina dhidi ya Sheikh Takadir. Mwenyezi Mungu amrehemu.

Ndugu Waislamu , Mwalimu amekuwa mtu muhimu sana katika historia yetu. Mwalimu ametulilia machozi, amekiri maonevu dhidi ya Waislamu kabla ya Uhuru, anaufahamu fika mchango wa Waislamu katika kuleta Uhuru wa nchi hii na anaifahamu Ihsani ya Waislamu kwa wasio-Waislamu. Ni nini lakini ilikuwa asili ya machozi ambayo yalipelekea imani zaidi ya 'kumrembesha' Mwalimu mbele ya macho ya Waislamu.

Kama kanuni ya kibinadamu ilivyo, mtu hutokwa na machozi aidha kwa uchungu na majonzi ya dhoruba au misiba ya maisha, au kwa furaha isiyo kifani.

Lakini machozi ya Mwalimu yanakuja na sura au tafsiri ya ajabu mno! Kwanza, yaonekana labda ni uchungu wa kupewa sifa siyo yake, asiyoipenda na inayomdhalilisha na alihisi kutengwa na jamii nzuri ya ndugu zake aliowategemea.

Hali ile ilihuzunisha mno na hapo imani ya Waislamu juu ya Mwalimu ikazidi kiasi cha kuifikisha jamii ya Waislamu kumtenga Sheikh Takadir katika hali zote japo Shujaa huyo kwa ujasiri wake, ujuzi, hekima na msimamo wake katika dini, hakujutia hata kidogo kumkataa Mwalimu Nyerere. Hilo lilikuwa bora kwake kuliko kumkubalisha Mwalimu kwa Waislamu.

Asili ya machozi yale ya Mwalimu haikuweza kupatikana muda ule kwa kuwa wakati ule agenda muhimu kwa Waislamu ilikuwa ni Uhuru na maisha baada yake. Leo hii historia imetufikisha hapa tulipo kama alivyousia Marehemu Sheikh Takadir, "ipo siku mtanikumbuka.", na kweli sasa tumekiona 'kilichobebwa' na yale machozi.

Basi asili ya machozi ipo katika matunda machungu yaliyopamba katika historia ya utendaji wa Mwalimu na wanae aliowarithisha. Madhila aliyotufanyia ikiwa ni siri na kwa uangalifu mkubwa (systematic injustice) yameatiri jamii ambapo leo gharama ya kuirudisha hadhi yetu imekuwa kubwa mno. Udini umeshamiri bila kuacha ufa, utaifishaji na dhuluma ya mali za Waislamu, kuzima mkondo wa sheria na haki dhidi ya Waislamu kiasi cha kufikia kupigwa, kufungwa na kuuawa kwa mtutu bila haki ikiwa ni gharama ya 'kuwaachia' utawala wale waliomkataa Sheikh Takadir.

Ninadhani asili ya machozi sasa imedhihirika: haikuwa uchungu ila ilikuwa ni kafara ya kulikubalisha Kanisa juu ya jamii ya Watanganyika hususan Waislamu waliokuwa wengi na makini. Yote yaliyotukuta na yanayoendelea kutukuta ni agenda za siri ya Kanisa Katoliki zilizoachwa na wakoloni ili kuendelea kututawala Waislamu kifikra, kiuchumi, kisiasa na kuudhibiti.
 
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook