HOJA BINAFSI
 
Jina ALLAH katika Biblia ya Kiarabu
 

Na K. Mtwange
 

KATIKA mjadala juu ya hoja kwamba ALLAH wa kwenye Qur'an siyo YEHOVA wa Biblia tumeona ni bora kutoa ushahidi mwingine juu ya upotofu wa dhana hii. Bila shaka Bwana Muhibu Said amejibu vema lakini kwa wote ambao bado wana mashaka, tunatoa hapa chini aya kutoka katika tafsiri ya Biblia Takatifu katika Kiarabu. Tafsiri hii ya Biblia ambayo hujulikana kama "Al-Kitaab Al-Muqadis' (yaani Kitabu Kitakatifu), hutumiwa na Wakristo wanaozungumza lugha ya Kiarabu (ambao bado wapo kiasi cha millioni 15 mpaka 20 katika Mashariki ya Kati peke yake). Kwa wale ambao hawafahamu herufi za Kiarabu tumetoa vilevile aya kutoka katika Qur'an ili wapate kulinganisha. Katika aya hizi za kiarabu zilizopo hapa chini, neno la Kiarabu "Allah" limepigiwa mstari chini ili liweze kutambulika kirahisi. Baada ya kulinganisha aya hizi inategemewa kila mmoja ataweza kuona kwamba neno 'Allah" linaonekana katika Qur'an na pia katika Biblia, kwani ni neno la Kiarabu lenye maana ya Mwenyezi Mungu. Inshaallah, mifano hii itaondoa mashaka kwa wale walioingizwa kwenye mkumbo wa kuamini kwamba "Waislamu wanaamini Mungu tofauti" kupitia vyombo vya habari vyenye uadui au kwa propaganda za Wamishionari wa Kikristo.

HATUFIKIRII njia nyingine ya kuthibitisha ukweli huu isipokuwa kumshauri kila mmoja mwenye mashaka kufanya utafiti wake mwenyewe bila ya upendeleo.

[Qur'an 1:1 ­ tafsiri ya Kiswahili]

"Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu"

"Bismi Allahi ar-Rahmaan ar-Rahiim"

[Qur'an 1:1-Kiarabu]

[Mwanzo 1:1 ­ Biblia ya Kiswahili]

"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na na nchi"

"Fiy-al-badi' khalaqa Allahu as-Samawawwat wal Ardh"

[Mwanzo 1:1 ­Biblia ya Kiarabu]

[Yohanna Mt. 3:16 ­ Biblia ya Kiswahili]

"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa"

"Li-annhu haakadha ahabba Allahu ul 'Aalama hataa badhala"

[Yohanna 3:116 ­ Biblia ya Kiarabu]

[Luka 1:30 ­ Biblia ya Kiswahili]

"Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu"

"Laa takhaafiy, yaa Maryam, li-annaki qad wajadt ni'mat(an) 'inda Allahi"

[Luka 1:30 ­ Biblia ya Kiarabu]

[Luka 3:38 ­ Biblia ya Kiswahili]

"wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu"

"bni anuusha, bni shiyti, bni Aadama, abni Allahi."

[Luka 3:38 ­ Biblia ya Kiarabu]

[Mathayo 19:17 ­ Biblia ya Kiingereza ­ New King James Version]

"there is none good but one, that is, God"

"laysa ahadun saalihaan illa waahdun wa huwa Allahu"

Yaani "aliye mwema ni mmoja, naye ni Mungu"

[Mathayo Mt. 19:17 ­ Biblia ya Kiarabu]

 
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook