Issa Ponda hana kosa
Atafutwa mchochezi, mvurugaji
amani,
Asha kwa mfano ndezi, kwa
moto vichakani,
Iwe yao moja kazi, kumtia
hatiani,
Katika upelelezi, ashakwae
hana kosa.
Ashakwae hana kosa, si mvugura
amani,
Hivyo ni vyakwao visa, lengo
tumelibaini,
Ukistaajabu Musa, waona
ya Firauni,
Katika upelelezi, ashakwae
hana kosa.
Kunajambo talinena, lisikize
ka makini,
Mwenye kosa wasi hana,
mvurugaji amani,
Atembea kila kona, na silaha
mabegani,
Katika upelelezi, ashakwae
hana kosa.
Amewaua hadhirina, bila chembe
ya imani,
Kuumba uwezo hana, katutia
misibani,
Mchochezi na fitina, mwamsaka
mtu gani,
Katika upelelezi, ashakwae
kaonewa.
Mengine usitaraji, mwenye
kosa fafanua,
Kama kweli mshakaji, haki
ukitumia,
Mwenye kosa muuaji, amani
katuvurugia,
Mvurugaji amani, raia wema
kauwa.
Muuaji huyo mtu, amezizusha
hasama,
Ameua ndugu zetu, mfano
kama wanyama,
Kutendeka hiki kitu, hatusahau
daima,
Sisi lilobaki kwetu, kura
zetu kuwanyima,
Mvurugaji wa amani, silaha
alotumia.
Bi. B.A. Mohamed,
S.L.P. 4,
Pangani,
Tanga.
Acha kujidhalilisha
Bismillahir naanza, kwa jina
lake Rabuka,
Tena kanipa uweza, kusoma
na kuandika,
Nia ni kuwaeleza, wasia
wangu hakika,
Acha kujidhalilisha, ewe
dada Islamu.
Islamu wa kisasa, kwa kweli
wanishangaza,
Waichukua mikasa, nakupita
itangaza,
Waicheza kwasa kwasa, njiani
bila kuwaza,
Acha kujidhalilisha, ewe
dada Islamu.
Amekuwa hayawani, hujuwi
kikudhurucho,
Kila onacho njiani, wakitaka
uwe nacho,
Yakushinde miwani, yakaapo
kwenye jicho,
Acha kujidhalilisha, ewe
dada Islamu.
Yarabi katuumbia, sura za
kila namna,
Sie twajiharibia, twajiweka
kwa namna,
Ngoziye kuikoboa, nazo nyuso
kuzichuna,
Acha kujidhalilisha, ewe
dada Islamu.
Hivi huna hata haya, kukataa
bara lako,
Vipi wale wa Ulaya, wakitaka
kuja kwako,
Wakimbilia Ulaya, na nywele
kama ukoko,
Acha kujidhalilisha, ewe
dada Islamu.
Mashindano uremboni, ndiyo
hayo mwayaweza,
Utakuta gazetini, uchi mmejilegeza,
Hata huko mashuleni, nao
pia wajikaza,
Acha kujidhalilisha, ewe
dada Islamu.
Acheni mfananisho, kati yako
na kondoo,
Yaja siku ya kitisho, ukate
ndugu na koo,
Kikutoke na kijasho, hiyo
siku ya kitisho,
Acha kujidhalilisha, ewe
dada Islamu.
Nane beti namaliza, kalamu
naweka chini,
Namshukuru muweza, kuniweka
akilini,
Kanijalia uweza, unifae
maishani,
Acha kujifananisha, kati
yako na wanyama.
Asha Juma,
Msamala Muslim Seminary
Sec. Sch.,
S.L.P. 985,
Songea.
Hivi ni kigezo gani, kinachotumika
hasa,
Mialiko ya wageni, kwenye
hafla za sasa,
Mambo haya ya zamani, au
yanaanza sasa,
Kumualika Sumaye, ni kosa
kubwa kabisa.
Sumaye kuwa mgeni, tena huja
kuwaasa,
Masheikh waumini, wote kupigwa
msasa,
Ukafiri hamuoni, mbona mnafanya
visa,
Waumini wote ndugu, haya
ndio mafundisho?
Hemed mjaa fani, nanyi Masheikh
wa sasa,
Hafla hizi za dini, wapi
nyinyi mmenasa,
Mtabeba mgongoni, mafurushi
ya makosa,
Waumini wote ndugu, haya
ndio mafundisho?
Mabakwata tizameni, mnayo
mengi makosa,
Serikali si yadini, ukafiri
ndio hasa,
Mwawaalika wa nini, mbona
nyinyi mwajitosa,
Waumini wote ndugu, haya
ndio mafundisho?
Mengi tasema mbeleni, leo
nimeyatomasa,
Mnayofanya jamani, njaa
ua ututusa,
Tafakarini undani, pepo
tusije ikosa,
Kumualika Sumaye, ni kosa
kubwa kabisa.
Zuberi Mohamed Mwinyi
(Amir),
S.L.P. 61428,
Dar es Salaam.
|
|