Furaha inayo nafasi katika Uislamu, lakini ni furaha anayoipata mtu kutokana na kutekeleza kwa moyo mkunjufu sheria iliyowekwa na Mwenyezi Mungu. Furaha hiyo ni ya kimwili, kiakili, kisanii (artistic) na kiroho; anaipata mtu binafsi, kikundi, taifa na hata walimwengu wote. Furaha za aina zote hizo hazina mgongano katika Uislamu bali zinakamilishana.
Aidha dhana ya ukamilifu (perfection) pia inayo nafasi katika Uislamu. Kwa mtazamo wa Uislamu ukamilifu ni kule kufuzu mitihani na majaribio anayopata mtu kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika maisha haya. Ukamilifu huo unamuhusu kila mtu, kikundi au taifa. Hivyo kila mtu anahimizwa kujitahidi kuuwania ukamilifu huo na kuwasaidia wenziwe kuufikia. Msimamo wa wa baadhi ya wanafalsafa juu ya kutimiza wajibu pia unapata ufafanuzi bora chini ya Uislamu. Mwanafalsafa Kant aliandika juu ya kile alichokiita "Kanuni ya lazima"(categorical imperative) lakini hakuweza kufafanua. Hivyo "kanuni ya lazima kwa hakika ni sheria ya Mwenyezi Mungu, sheria ambayo Yeye ndiye aliyeipanga na haina budi kutiiwa kwa sababu tu ni sheria yake Mwenyezi Mungu. Kwa hakika wema si chochote bali kutii na kujisalimisha chini ya sheria ya Mwenyezi Mungu. Vivyo hivyo Uislamu haukatai umuhimu wa kipawa cha akili au uzoefu n.k., bali unazitumia nyenzo hizo kama visaidizi tu na siyo vitegemezi.
Imani ya Muumba na athari yake juu ya Uadilifu
Imani ya Uislamu juu ya Mwenyezi Mungu kwa muhtasari sana ni kwamba Yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mfalme Pekee, Bwana na Muumba wa binadamu na ulimwengu wote na hakuna yeyote anayeshirikiana naye kwa hali yoyote katika Dhati, Mamlaka au sifa Zake. Hakuna yeyote anayeweza kumuathiri kwa hali yoyote, wala hakuna yeyote anayeweza kuhakikisha kuwa mapendekezo yake yanakubaliwa isipokuwa tu kwa Rehema Yake, tena basi kama yatakuja kama dua itokayo kwa mja aliyejidhalilisha. Kufanikiwa au kuangamia kwa mtu yeyote kunategemea mwenendo wake yeye mwenyewe. Hakuna mtu yeyote anayeweza kutubia kwa ajili ya makosa ya mtu mwingine; wala mzigo wa mtu yeyote hautabebeshwa juu ya mabega ya mtu mwingine, wala hakuna awezaye kupata malipo mema kwa amali za mtu mwingine mbele ya Mwenyezi Mungu hakuna upendeleo wa aina yoyote hivyo hakua mtu yeyote mwenye nafasi ya kipekee kwa Mwenyezi Mungu wala hakuna familia maalum, ukoo, kabila, rangi au taifa maalum. Binaadamu wote ni sawa mbele yake. Watu wote bila kubagua wanatakiwa wafuate sheria ile ile moja ya Uadilifu kutoka Kwake peke yake na ubora pekee wenye mizani mbele ya Mwenyezi Mungu ni ubora katika kutekeleza sheria Yake. Yeye ni Mwingi wa Rehema anawapenda waja wenye huruma; Yeye ni Mkarimu anawapenda wakarimu;Yeye ni Muadilifu anawapenda wafanyao haki. Yeye ametakasika na aina zote za dhuluma, ufinyu wa fikra, ukatili, uovu, ushabiki, upendeleo na anawapenda watu wanaojiepusha na maovu hayo. Ukubwa wote ni haki yake peke yake hivyo anachukia kiburi na majivuno ya mtu yeyote hata kama yeye anadhani ni mkubwa vipi. Sifa zote za kiungu ni zake peke yake hivyo anamchukia mtu yeyote anayejipa mamlaka ya mwisho juu ya mtu au kikundi fulani cha watu.
Yeye ndiye Mmilikaji wa hakika wa vyote vilivyomo mbinguni na ardhini na chochote ambacho mtu anaeonekana kuwa anakimiliki, kama dhamana tu itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Hivyo kiumbe yeyote anayejifanya kuwa yu huru na mamlaka Yake, au mwenye kiburi cha kuthubutu kuwapangia watu wengine sheria kinyume na sheria za Mwenyezi Mungu au anayedai kutiiwa na ilhali anakiuka sheria za Mwenyezi Mungu anajitumbukiza katika makosa makubwa sana kwani Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mfalme wa watu wote. Yeye ndiye Mpaji wa vipawa, vipaji na hidaya zote hivyo lazima vitumiwe kwa mujibu wa maamrisho Yake. Yeye ni Mjuzi wa Yote na anayajua hata yaliyofichikana katika nyoyo, hivyo hakuna mtu yeyote au kiumbe anayeweza kumdanganya kwa namna yoyote.
Athari ya mafundisho haya
Mtu akizingatia kwa makini sana mafundisho haya ya Uislamu juu ya Dhati na Sifa za Mwenyezi Mungu itamdhihirikia kuwa uadilifu utachipuka kutokana na mtazamo huu mfumo bora kabisa wa uadilifu. Chini ya mfumo huu hakuna mlango wa nyuma wa kuepea kutimiza wajibu wala mfumo huu hautoi nafasi kwa zile falsafa za kikatili zinazowabagua watu kwa misingi ya tabaka, ukoo, nchi, rangi na hivyo kulifanyia haki kundi moja na dhulma kundi jingine. Kwa mfano Lenin, muasisi wa Ukomunisti huko Urusi, alipokuwa anahutubia mkutano wa chama chama cha vijana wote wa Kirusi (All Russian Congress of Youth) alisema hivi:
For us morality is subordinated competely to the interest of class struggle of proletariat.
Tafsiri:
Kwetu sisi uadilifu lazima utumikie maslahi ya mapambano ya kitabaka ya makabwela.
Zaidi ya hayo mafundisho ya Uislamu yasemayo kuwa mtihani wa Mwenyezi Mungu haujafungamana na kipengele kimoja tu cha maisha bali unahusu vipengele vyote, yanapanua uwanja wa uadilifu uwe mpana kama maisha yenyewe, Mtu anatahiniwa na ataulizwa jinsi alivyovitumia vipawa vyake vya kuhoji na kufikiri, vya kufahamu, vya kimwili, ataulizwa pia juu ya uhusiano wake na wenzake. Zaidi ya yote hayo atahisabiwa iwapo aliyafanya yote aliyoyafanya kwa nia ya kumtii Mwenyezi Mungu au kwa ajili ya kuwatii viumbe wa Mwenyezi Mungu. Mafundisho ya uadilifu chini ya misingi hii humstawisha binaadamu katika kila fani ya maisha yake.
Katika biashara pasiwe na viapo kwani hii ni miongoni mwa
Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Maji ya asili hayatauzwa ili kununua malisho yaliyomo pamoja. (Bukhari na Muslim.
Hadithi hizi zinatufundisha kuwa mali asili kama maji, majani, miti ya porini, wanyama pori, madini (n.k.) ni haki ya kila mwanadamu kwa hiyo hapana mwenye haki ya kuzuia mali ya asili na kuifanya yake na kuharamisha wengine wasimiliki. Bali kama mali asili imeshughulikiwa ndio ifae kutumika, itajuzu mwenye kuishughulikia awe na haki ya kudai arudishiwe gharama alizozitoa katika shughuli hiyo. Kwa mfano gharama za mabomba, na mashine ya kusukumia maji n.k. lakini kuyauza maji ya chemchem ya asili au mto ni haramu. Hali kadhalika na kuuza ardhi au mimea iliyoota porini ni haramu.
(vii) Uuzaji wa samaki aliyeko majini, uuzaji wa ndege anayeruka angani (ambaye hafugwi), uuzaji wa maziwa ambayo hayajakamuliwa na uuzaji wa manyoya ya mnyama yangali mwilini mwake ni uuzaji haramu. Ni wazi kuwa mauzo yote haya yameharamishwa kwa sababu bidhaa hizo hazina uhakika wa kuzipata. Ili pawe na haki kati ya muuzaji na mnunuzi bidhaa hizo hazina budi kupatikana kwanza mkononi ndio ziuzwe.
(viii) Uuzaji wa damu na uuzaji wa uhuru wa mtu (utumwa) uuzaji wa nywele na maziwa ya binadamu ni biashara haramu. Vitu vyote hivi si haki ya mwanadamu na havipatikani kutokana na jasho lake, hivyo hana haki ya kuviuza na wala hana hata uwezo wa kukadiria thamani yake halisi. Kama hatuwezi kukadiria thamani ya mvuto mmoja wa hewa au thamani ya tone moja la maji, tutaweza kukadiria thamani ya damu, achilia mbali thamani ya maisha yetu?
(ix) Mauzo ya mbwa, nguruwe, pombe, damu na mzoga ni biashara haramu. Pia ni haramu kuuza picha na sanamu kama tunavyhofahamishwa katika hadithi zifuatazo:
Abu hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah ameharamisha kipato kilichotokana na kuuza damu, mbwa, na kipato cha malaya, Na amelaani mwenye kupokea na mwenye kutoa riba, na mwenye kuchora mwili kwa chale na mwenye kuchorwa mwili kwa chale na mchoraji wa picha (za wanyama) na watu.(Bukhari).
Jabir ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allah akisema katika mwaka wa ushindi (wa kuiteka Makka) wakati alipokuwa Makka. Hakika Allah na Mtume wake wameharamisha mauzo ya pombe; mizoga, nguruwe na masanamu... (Bukhari na Muslim).
(x) Ulanguzi (Kuhodhi bidhaa)
Hili ni neno pana linalotumiwa kwa maana mbali mbali; lakini katika kipengele hiki tutalitumia neno hili kuwakilisha kitendo cha kuteka nyara bidhaa muhimu sokoni kwa kuinunua kwa wingi labda kwabei ya juu kidogo kwa madhumuni ya kuilundika (kuihodhi) na kuifanya iwe adimu ili hapo baadaye itakapokosekana sokoni iuzwe kwa bei ya juu sana na kutoa faida kubwa sana. Biashara ya namna hii ni biashara haram kama tunavyofahamishwa katika hadithi kadhaa zifuatazo:
Umar amesimulia kutoka kwa Mtume wa Allah aliyesema: Mwenye kuleta nafaka (mjini) anazidishiwa rizki na mkusanyaji na mfichaji wa bidhaa hizo amelaaniwa. (Ibn Majah, Dirimi).
Umar amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Anayelundika na kuzuia bidhaa za chakula kwa siku 4 kwa nia ya kupata bei kubwa zaidi, anajitenga na Allah na Allah anajitenga naye. (Razin).
Hadithi zote hizi zimedhihirisha ubaya wa kuzuia bidhaa, hasa bidhaa muhimu kama vile chakula, na kuzifanya ziwe adimu ili kuuza kwa bei kubwa itakayotoa faida kubwa sana. Biashara ya namna hii ni biashara haram na laana ya Allah iko juu ya walanguzi hawa:
Mu'az amesimulia: Nimemsikia Mtume wa Allah akisema" Mbaya ni yule anayelundika bidhaa na kuifanya iwe adimu. Kama Allah akifanya bidhaa kuwa rahisi, yeye anachukia na kama Allah akiifanya kuwa ghali, anafurahi, (Razin, Baihaqi).
Hadithi hii inatueleza sura hasa ya mlanguzi. Ama mtu kuweka bidhaa alizozilima na alizotengeneza mwenyewe au kuuza bidhaa alizozinunua kutoka masafa ya mbali si haramu. Lililoharamishwa ni kule kununua bidhaa katika soko la kawaida na kuzificha ili baadaye uziuze kwa bei kubwa baada ya bidhaa hiyo kuwa adimu katika soko.
Pamoja na Uislamu kulaani ulanguzi, hauruhusu kumkangandamiza mfanya bishara kwa kumuwekea bei ya bidhaa zake. Bei inatakiwa ijiweke yenyewe kulingana na hali halisi ya soko. Bidhaa zikiwa nyingi bei itakuwa chini na bidhaa zikiwa chache bei itakuwa juu. Tunajifunza kutokana na hadithi ifuatayo:
Anas amesimulia kuwa wakati mmoja katika wakati wa Mtume wa Allah bei ya vitu ilikuwa ghali. Wakamuomba Mtume: Ewe mtume wa Allah panga bei kwa nafuu yetu. Mtume wa Allah akajibu: Hakika Allah ndiye anayemiliki bei, anapunguza, anatoa kwa wingi, anatoa riziki, na ninapendelea sana nikutane na Bwana wangu katika hali ambayo hapana yeyote kati yenu atakayenifanya niwe na dhima juu ya damu (iliyomwagika kwa sababu yangu) au mali (aliyopunjwa kwa sababu yangu)! (Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah).
Hadithi hii inatupa fundisho kubwa kuwa Uislamu kama usivyoruhusu kukandamizwa na kudhulumiwa mnunuzi ndivyo hivyo hivyo isivyoruhusu kukandamizwa kwa mchuuzi au muuzaji. Mtume (s.a.w.) akiwa kiongozi mkuu wa Serikali ya Kiislamu, hakuthubutu kutumia madaraka hayo na kuingilia haki za wafanya biashara waliopewa na Allah (s.w.). Jibu lake kwa namna nyingine lilikuwa "anayepanga bei ni Allah (s.w.) kwa bei". Kutokana na hadithi hii hapana yeyote mwenye haki ya kukaa chini na kumpangia mfanya biashara bei iliyo kinyume na ile iliyojitokeza yenyewe sokoni. Kinachotakiwa kifanywe na nguvu za dola ni kutokomeza njama zote za ulanguzi na vikwazo vyote vya uchumi. Kisha kuwaacha huru wafanya biashara wauze bidhaa zao kwa bei halisi inayokubaliwa katika soko huru.
(ix) Kupunguza kipimo cha ujazo au kilo kwa kuharibu mizani au kugonga vipimo vya ujazo ni haramu. Mwenyezi Mungu amewamea vikali sana watu wasiopima kwa uadilifu katika biashara zao.
Maangamizo yatawathubutikia wapunjao (wenzao) Ambao wanapojipimia kwa watu hupokea (kipimo) kamili. Lakini wanapowapimia kwa (kipimo cha) vibaba au mizani (au vinginevyo), wao hupunguza. (83:1-3).
Na timizeni kipimo mpimapo; na pimeni kwa mizani zilizo sawa. Hayo ni wema kwenu na bora mwishoni (kwake). (17:35).
(xii) Kuficha ila (dosari) ya bidhaa inayouzwa ni haramu. Katika hadithi iliyosimuliwa na Bukhari, Baihaq na Al-Hakim, Mtume (s.a.w.) amesema: Muuzaji na mnunuzi kila mmoja lazima atimize makubaliano. Na muuzaji akitoa habari zote juu ya bidhaa anayoiuza pamoja na mfano, kama unauza maharage makavu mwambie mnunuzi mathalan, uzuri wa maharage haya ni kuwa hayajatoboka lakini yana ila moja ya kuchelewa sana kuiva. Mwache mununuzi apime hiari ya kununua au kuwacha.
Kutokana na maelezo yote
haya; juu ya vipengele mbali mbali vilivyo haramishwa katika biashara,
tunaona kuwa biashara japo ni kazi halali yenye hadhi kubwa mbele ya Allah,
haitamnufaisha mwanadamu iwapo mipaka ya Allah (s.w.) haitachungwa wakati
wa kufanya shughuli hiyo.
--
|
|