Walioteuliwa ni Wakristo watupu
 

Na Mwandishi Wetu
 

UTEUZI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la PPF umefanyika hivi karibuni ambapo Bodi hiyo imejikuta ikiwa na Wakristo watupu kana kwamba ni taasisi ya Kanisa.

Wakurugenzi wapya wa Bodi hiyo ni Bw. Richard M. Kavura, Bw. Joseph Massawe, Bw. Patrick Mwangunga na Bw. Moses Kachima. Wengine ni Africhnus Maenda, Thabita Siwale, Raphale Mlolwa na David Mattaka. Mwenyekiti wa Bodi hiyo ni Bw. Raphael Mollel.

Katika Bodi iliyomaliza muda wake walikuwepo Waislamu watatu ambao ni Balozi Suleiman Hemed, Mhe. Kitwana Kondo (MB) na Bw. Said Nkya.

Baadhi ya watu walitoa maoni yao kufuatia kutangazwa kwa Bodi hiyo wamedai kuwa huenda bodi hiyo imelazimika kuwa ya Wakristo watupu kwa kutokuwepo Waislamu wenye sifa.

Hata hivyo, wengine wamedai kuwa Waislamu wenye sifa wapo ila hawajulikani walipo.

Lakini wapo walihoji kwa kuuliza Je; hata akina Alhaj Madabida hawawajui hao?

Akiongea na gazeti hili mfanyakazi mmoja wa PPF ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema kwamba anaishangaa Kamati ya Alhaj Ramadhani Madabida kuhangaika kutafuta 'data' za kisayansi wakati ziko huko huko Ikulu.

Pamoja na 'data' hiyo ya PPF amesema kuwa zipo 'data' za Tume ya Jiji ambayo imejaa Wakristo watupu utadhani ni taasisi za TEC au CCT.
 
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook