Shule ya Kiislamu Same kukamilika mwaka huu
 

Na Mwandishi Wetu
 

SHULE ya Sekondari ya Kiislamu ambayo ujenzi wake ulianza miaka mitano iliyopita wilayani Same inatazamiwa kukamilika kujengwa mwishoni mwa mwaka huu.

Tamasha la sita la ujenzi huo wa harambee uliowashirikisha Waislamu kutoka mikoa mbalimbali lilimalizika Julai tisa mwaka huu ambapo iliazimiwa kuwepo tamasha jingine mwezi Septemba na Oktoba kukamilisha ujenzi huo ili kuwezesha shule kuanza ifikapo Januari 2000.

Pamoja na kushiriki kivitendo wakiwa kambini kwa majuma mawili, wanatamasha walipata fursa ya kujadili kuanzisha miradi mingine kama hiyo katika sehemu nyingine ili kuwalea vijana wa Kiislamu kidini na kimaadili.

Aidha, waliazimia kuendelea na michango ya hali na mali ili kukamilisha hatua za mwisho za shule hiyo ya Kiislamu iliyo katika mandhari ya vilima vya Kirinjiko.

Shule ya Kiislamu Same inatarajiwa kuchukua wanafunzi Waislamu watakaokaa bweni kutoka sehemu mbalimbali nchini 
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook