Na Said Rajab
KATIKA toleo lake la Julai 3-9, 1999 gazeti moja la kidini (siyo ANNUUR) liliripoti kwama Kardinali Pengo alikuwa mmoja wa waandamanaji wa Makanisa duniani waliozitaka nchi tajiri zifute madeni ya nchi masikini.
Mwaka huu Ujerumani ndiyo iliyoshika Urais wa mkutano wa wakuu wa nchi zilizomo katika kundi la G8 uliofanyika mjini Cologne kuanzia Juni 18 hadi 20. Russia nayo ina nafasi ya kudumu katika kundi hilo, zikiwemo Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani.
Kundi la nchi hizi tajiri na zenye viwanda vingi duniani lilianzishwa na aliyekuwa kiongozi wa Shirikisho la Ujerumani Chancellor Helmut Coe na aliyekuwa Rais wa Ufaransa Valery Giscard el Estaing mwaka 1975.
Kadri tunakaribia mwisho wa karne hii sekta za uchumi na siasa zimekumbana na changamoto mbalimbali zenye kutisha. Kuongezeka kwa kutegemeana katika uchumi wa dunia (Interdependence within the global economy), masoko ya fedha yanakuwa ya kimataifa (Inteernationalization of finance markets) na changamoto ya maendeleo katika dunia imesababisa kuwa na haja ya kuweka upya mikakati ya kudhibiti uchumi na mfumo wa fedha wa dunia.
Kwa pamoja nchi za G8 zina malengo ya kuwa na tamko moja lenye nguvu katika uendeshaji wa uchumi wa dunia. Kwa hiyo kiini hasa cha mkutano wa Cologne ni kuboresha mfumo wa fedha wa dunia (International monetary syestem) na mfumo wa biashara ya kimataifa (multilateral trade system) kwa manufaa ya kundi la nchi za G8.
Prof. Klaus Gretschmann ambaye ni Ofisa aliyeshughulikia mkutano wa uchumi wa nchi za G8 uliofanyika Cologne anatoa maoni yake katika jarida la Deutcland la mwezi Juni/Julai kwamba"
"Germany will introduce an initiative towards further alleviating the debt burden of the poorest developing contries, the aim being to put these contries in a position to be able to develop their own growth potential".
Yaani" "Ujerumani itatoa pendekezo kuhusu kuzipunguzia zaidi mzigo wa madeni nchi maskini sana zinazoendelea kwa lengo la kuzifanya zikuze hazina yao ya uchumi zenyewe".
Kauli hii ya Prof. haina ukweli wowote kwani lengo hasa la kufutiwa madeni lnadhihirishwa na msemaji huyo huyo katika "paragraph" za mbele za kauli yake:
"Also on the agenda are crisis prevention through development and political cooperation, as well as environmental protection. Increased flexibility needs to be made socially ecceptable. The goverments can only achieve these objectives in conjuction with relevant social groups. For this very reason, the German government has already entered into dialogue with different associations, the churches and non-govenmental organizations".
Yaani: "Vile vile kwenye agenda kuna suala la kuepuka migogoro kwa kutumia maendeleo na ushirikiano wa kisiasa pamoja na kulinda mazingira. Mbinu mbalimbal zinahitajika zikubalike na jamii. Serikali zinaweza tu kulifikia lengo hili kwa kushirikiana na makundi ya kijamii yanayofaa. Na kwa sababu hii, serikali ya Ujerumani imeshafanya mazungumzo na jumuiya mbalimbali, Makanisa na NGOs".
Hiyo ndiyo siri ya maandamano ya akina Kadinali Pengo kule Cologne. Ni jambo ambalo lilikwishapangwa katika agenda za mkutano huo. Na nafasi ya Makanisa katika maandamano hayo ilikuwa ni kuepusha migogoro kwa ushirikiano wa kisiasa kama alivyodhihirisha Profesa Klaus Gretschmann. Nafasi ya Makanisa haikuwa kuyashinikiza mataifa tajiri yafute mzigo wa madeni kwa nchi maskini. Kile kilikuwa ni kiini macho tu. Kufutiwa madeni hakuna maana sana ya kiuchumi bali ni kisiasa. Kama wangetufutia sababu ya kuwepo kwa madeni kwa nchi maskini wangetusaidia sana kiuchumi!
Labda jambo la kuzingatia ni kwamba mfumo wa uchumi unaojengwa duniani hivi sasa una maslahi makubwa zaidi kwa nchi tajiri kuliko nchi maskini. Katika mfumo wa soko huria, sera za kulinda bidhaa zetu au masoko yetu ya ndani zinakufa. Inakuwa 'mwenye nguvu mpishe'. Ni sawa na kiwete kushindana kwenye marathoni na mtu mwenye miguu. Mataifa tajiri yanadhibiti masoko yetu yote kwa ubora wa bidhaa zao na nguvu ya mtaji. Sisi tunakuwa masoko yao ya kudumu na uchumi wetu unakuwa tegemezi kwa nchi hizi. Mazingira ya namna hii ndiyo yanayowafanya wawe matajiri sana na sisi masikini sana.
Mabepari kwa dunia nzima wanaungana pamoja katika majumuiya makubwa ya uchumi kama EEC, vyombo vya fedha vya kimataifa kama IMF na World Bank, kundi la nchi za G8 na taasisi zenye kutoa mikopo kama Paris Club. Lengo hasa ni kuimarisha nguvu zao za kiuchumi na kisiasa. Hivi sasa wanajaribu kutumia sarafu moja inayojulikana kama "Euro-currency" ili waweze kudhibiti zaidi uchumi wa dunia na kuleta ushirikiano wa karibu zaidi wa kisiasa.
Mara nyingi nchi maskini zinakuwa ni majeruhi wa mipango ya kidhalimu ya uchumi ya fedha ya nchi tajiri. Sababu kuu hasa ya kudidimia kwa uchumi wa nchi maskini ni nchi tajiri. Kutoendelea kwetu kiuchumi kuna faida kubwa sana kwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi tajiri. Ndiyo maana wanatuweka katika duara la umaskini kwa mzigo wa madeni.
Nchi zote maskini duniani ziko katika duara la umaskini lijulikanalo kitaalamu kama 'vicious circle of poverty' yaani nchi hizi zina mtaji mdogo, hali inayopelekea ziwe na uwekezaji hafifu ambao unasababisha kuwa na uzalishaji duni, unaopelekea kuwa na kipato hafifu na kipato hafifu inaturudisha pale pale kwenye mtaji mdogo. Kwa hiyo kujikwamua kutoka katika duara hili tunahitaji msaada wa kiuchumi kutoka nje. Sisi wenyewe hatuwezi kwa sababu tumo ndani ya 'kibano'. Wenye kuweza kutusaidia ndiyo hao hao wanaonufaika na kuwepo kwetu katika duara la umaskini; IMF na World Bank wanatupa mikopo yenye masharti na riba kubwa inayosababisha madeni yasiyobebeka.
Kufutiwa madeni yasiyolipika si dawa ya kusaidia uchumi wa nchi maskini. Bali ni agenda ya kisiasa yenye lengo la kuwafanya matajiri waonekane wana huruma na nchi maskini. Wanajisafisha tu machoni mwa walimwengu kwa manufaa yao wenyewe kisiasa.
Ieleweke tu kwamba Makanisa
hayakuandamana kwa lengo la kuyashinikiza mataifa tajiri yafute mzigo wa
madeni wa nchi maskini. Hayana ubavu huo bali yanatumika tu kukamilisha
agenda za wakubwa.
--
|
|