Serikali inayatumikia Makanisa - Baraza Kuu
 

Na Mwandishi Wetu
 

RAIS Benjamin Mkapa amepelekewa taarifa inayodai kwamba serikali imekuwa ikiyatumikia Makanisa ambapo hulazimika kuyapa ruzuku kuendeshea shughuli zao.

Aidha, imeelezwa katika taarifa hiyo kuwa serikali imekuwa ikiwajibika kwa Makanisa kwa kuyatengea nafasi maalum za masomo pamoja na kuyatafutia fedha toka nchi na mashirika ya nje yanayoipa Tanzania misaada.

Taarifa hiyo ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu ya hivi karibuni kwa Mhe. Rais Mkapa imedai kuwa serikali inawajibika kwa Makanisa kutokana na makubaliano kati yake na Jumuiya ya Makanisa.

Taarifa hiyo kumb. Na. BK/J.1.5/A-99 imedai kuwa makubaliano hayo ni rasmi ambapo hadhi yake ni ya itifaki inayoifunga serikali ya nchi yetu kimataifa; na kuifunga pia kwenye wajibu wa kuyatumikia Makanisa nchini kwa kushirikiana na serikali na Mashirika ya dini ya nchi za nje za Kikristo.

Ikimalizia taarifa hiyo iliyosainiwa na Sheikh Omar Samata na kutolewa nakala kwa Jumuiya zote za Kiislamu nchini ilimkumbusha Mhe. Rais Mkapa azma ya Taifa letu ya kutobagua sehemu yoyote ya jamii ya Watanzania kwa misingi ya dini.
 
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook