KANDANDA la kusisimua mno lililonyeshwa na timu ya Kenya katika dakika kumi za kumaliza, wakati walipofunga mabao matatu mfululizo na kujipatia ushindi wa kuifunga timu ya Tanganyika kwa mabao 4-2 kwenye mechi ya kusherehekea Kenyatta Day.
Mechi hii ilichezwa kwenye uwanja uliokuwa na taa huko Jamhuri Park, maili chache toka mjini Nairobi. Itakumbukwa kwamba majuzi Kenya ilipopambana na Tanganyika katika uwanja wa Nakivubo, Kampala wakigombea kombe la Gossage, ilifungwa mabao 2-0.
Katika dakika kumi za kwanza Tanganyika walikuwa moto moto na dakika ya 14 kufika tu Saleh Zimbwe insaidi lefti wa Tanganyika alipochenga akina Nyawanga, Chege na Madegwa na mara akabakia na kipa wa Kenya, Otieno, na bila kupoteza wakati akalichafya moja moto moto likasambaa wavuni.
Dakika nne baadaye Tanganyika wakaonekana kuwa kandanda ni lao, wakati walipojipatia bao la pili. Katika hafu taimu, Tanganyika walkuwa wameongoza kwa mabao mawili kwa yai la Kenya.
Kipindi cha pili hakikuanza kwa nguvu sana, lakini Kenya wakajipatia bao lao la kwanza katika dakika ya 12 baada ya Ouma kulipata boli na bila kumpa nafasi kipa wa Tanganyika Mbarak akalijaza wavuni.
Safari hii Kenya walikuwa wakati wote wanalo boli, lakini hakuweza kujipatia bahati ya kufunga mpaka dakika ya 33 wakati Ouma alipofunga bao la kusawazisha na dakika sita baadaye Edward Otieno akafunga la 3-2.
Kenya tangu hapo ilianza
kuchafuka vikali na goli la nne liliingizwa katika dakika ya 43, na John
Nyawanga. Huu ulikuwa ni ushindi wa Kenya kwa Tanganyika baada ya miaka
miwili iliyopita.
MAJABALI wa African Sports Club wiki hii wameonyesha kuwa wangali bao wanapaswa kuhesabiwa kama mabingwa wa soka katika Afrika Mashariki nzima, wakati kwa mara nyingine walipoonyesha ushujaa wao kwa kuichapa timu kali mno ya Liverpool "A" kutoka Mombasa Kenya kwa mabao 4-1 mbele ya watazamaji kwenye Manisipali Stadium ya Tanga, anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga.
Hii ilikuwa ni mojawapo ya mechi kali mno ambazo zilichezwa katika Tanga wiki hii. Katika mechi ya siku ya kwanza, timu hii ya Sports iliangusha pia Liverpool kwa mabao 2-1 na Liver siku hii walitoka uwanjani wakigomea penelti.
Katika mechi ya siku ya pili, Sports waliingia uwanjani na mastaili mapya kabisa wakionyesha Liver ujuzi ikwa na majabali wake kama akina Nasir Omar, Riziki, Sare, Badi, Mzee Isihaka na wengineo, ilionekana kuwa kavu mno na isio na masikhara hata kidogo.
Boli lilisukumwa vikali kwa muda wa dakika kumi za kwanza na likawa halitulii upande mmoja wa kiwanja. Hata hivyo lakini lilipeperuka na kutua katika miguu ya sentafowadi Hamadi Yusuf ambaye hakutaka kubabaisha na akakatia boli hilo wazi kabisa kwa Salehe Zimbwe aliyeeneza bao la kwanza wavuni.
Liver kuona hivi walianza kuzuia mlango wao kwa nguvu zote na kipa Nyara alionekana akijaribu sana kusevu kiki kali za fowadi ya Sports.
Wakati mmoja kabla ya haftaimu, boli lilimfikia Badi ambaye alimchenga vizuri sentahafu wa Sports Omari Zimbwe na kujaza la kwanza.
Boli liliendelea vikali toka
hapa na mara ikawa haftaimu. Kwenye raundi ya pili defensi ya Sports ikiwa
na Mweri, Omari Zimbwe, Jomo na Mwaliza ilifanya kazi kubwa mno kuzuia
Liver iliokuwa ikishambulia vikali. Salehe Zimbwe aliyekuwa mfungaji hodari
katika mechi hii, hakutaka masihara bali aliongeza mabao mawili zaidi na
kuifanya timu yake kuwa na ushindi wa 4-1.
--
|
|