Katika hadithi iliyosimuliwa na Bukhari na Muslim, Mtume (s.a.w.) aliwasifu sana Al-Afariyyin (watu wa ukoo wa Abu Musa). Akasema watu hao walipokuwa vitani au safarini na chakula kikapungua basi walikikusanya pamoja chakula chote kilichosalia na kukigawa tena sawa sawa miongoni mwao.
Au nchi ikiingia njaa - ilitokea njaa kubwa kwa mfano wakati wa Ukhalifa wa Umar. Alichokifanya ni kutoa taarifa kwa viongozi wa majimbo mbalimbali na kuwataka walete chakula cha ziada. Na kilipokuja alikigawa bila ya kujali cheo, madaraka au ukoo wa mtu bali kwa kujali mahitaji tu. Kwa bahati njema njaa hiyo ilikwisha mapema. Lakini miongoni mwa maneno aliyoyasema Umar ni kuwa lau njaa hiyo isingekwisha mapema, basi angewakusanya watu wote wenye njaa na angewagawa kwa familia zenye chakula. akasema hii ni kwa sababu watu hawatakufa wakila chakula hata kama hawatashiba.
3. Kodi (Jizya)
Ni njia nyingine itumiwayo na Uislamu katika kuigawanya mali katika jamii. Tofauti na Zaka na Sadaqa ambazo hupasa kutolewa na Waislamu, Jizya hutolewa na wasiokuwa Waislamu (Dhimmi), wanaoishi chini ya dola ya Kiislamu, kwa ajili ya kupata hifadhi na huduma mbalimbali.
4. Mikopo
Mikopo kama njia mojawapo ya kugawa mali kwa watu wote, Uislamu unaruhusu watu kukopeshana. Mtu anaweza kumkopesha mwingine fedha ama kwa kutumia (matumizi ya kawaida katika maisha) au kwa kumsaidia mtaji kufanya biashara. Tutaliangalia hili kirefu kwenye kurasa za mbele.
Njia za uchumi zilizoharamishwa
Hapa tutajaribu kuorodhesha vipengele vilivyo haramishwa katika kuchuma. Vipengele vya biashara haramu vilivyoorodheshwa nyuma ni miongoni mwa hivyo:
(i) Wizi
Wizi wa aina yoyote ni kitendo cha dhulma na inakharamishwa katika Uislamu.
(ii) Ulevi
Ulevi wa aina yoyote kwa kiwango chochote ni kharamu. Uharamu wa ulevi hauishii kwa unywaji tu; bali pia ni haramu kushiriki katika hatua yoyote ile ya utengenezaji, uuzaji na uandazi.
Anas ameeleza kuwa Mtume (s.a.w.) amewalaani (watu) kumi kuhusiana na pombe - yule anayeikamua, yule aliyehusishwa katika kuikamua, yule anayeinywa, yule anayeibeba, yule anayepelekewa, yule anayeiandaa, yule anayeiuza, yule anayepanga bei yake, yule anayeinunua na yule anayenunulia. (Tirmidh, Ibn Majah).
Kutokana na hadithi hii, inatuwia wazi kuwa yoyote ile ya utengenezaji, uzzaji na unywaji. Pato lolote mtu atakalolipata kama malipo ya kushiriki katika hatua yote ya matayarisho na unywaji wa ulevi, litakuwa ni pato la haramu. Hebu tuangalie hali halisi. Je, hatuwaoni Waislamu wakishiriki kwa ukamilifu katika viwanda vya pombe kama mameneja, makarani, wakemia, madereva, n.k.? Je, hawa wataridhika kuendelea kujiita Waislamu na ili hali kila saa wako katika laana ya Allah na Mtume wake na ibada zao zote hazikubaliwi maadam miili yao imerutubishwa na kipato cha haramu; kivazi chao ni haramu na kila walicho nacho katika mazingira yao kimepatikana kwa pato la haramu?
(iii) Kamari
Kamari imeharamishwa pamoja na pombe kama ilivyo katika aya ya (5:90) na (2:219). Pia hadithi ifuatayo inatubainishia kuharamishwa kwa kamari:
Abdullah bin Amr ameeleza kuwa Mtume wa Allah ameharamisha ulevi, michezo ya habari nasibu, kamari ya karata, na gobairah (aina ya pombe) na anasema: "Kila ulevi ni haram". (Abu Daud).
Hadithi hii inatubainishia kuwa aina zote za kamari dugu dugu, pata-potea, karata, bahati nasibu, (n.k.) ni haram na kwa hiyo pato lolote litakalo tokana na kamari ni pato haramu. Ni muhjimu kufahamu kuwa uharamu wa kamari hauishii kwa watu wawili au kikundi cha watu wachache bali hata kama kamari hiyo itachezwa kitaifa, itabakia kuwa haramu tu. Kwa hiyo bahati nasibu ya taifa, Bima ya Kimataifa, na michezo yote ya kamari iliyotolewa kibali na taifa, yote ni haramu mbele ya Allah na yeyote atakayeshiriki kwa namna yoyote katika michezo hiyo ya kamari atakuwa ameshiriki katika haramu na kipato chochote atakachokipata kutokana na ushiriki wake huo kitakuwa ni kipato cha haramu. Katika aya tulizozirejea hapo juu (5:90 -91) kamari imeharamishwa kwa sababu kuu tatu:
Kwanza, ni uchafu, kamari imeitwa "rijsi". Kamari imeitwa uchafu kwa sababu pesa anazozipata mtu kwa kamari ni za dhulma na haramu. Kufumba na kufumbua mtu amepata maelfu ya pesa bila jasho lolote. Hivyo ni dhulma na ni haramu.
Pili, kamari inajenga chuki na uadui. Hii ni kwa sababu yule aliyeliwa pesa zake kwa maelfu kwa njia hii ya dhulma huwa ana mfundo mkubwa moyoni na anamchukia sana yule aliyechukua pesa zake hata kama ajidai kuwa hajali, ukweli ni kuwa pesa zake zitamuuma sana. Na mara kadhaa wacheza kamari wameishia kupigana na hata kuuana.
(iv) Kipato chochote kinachotokana na utengenezaji wa sanamu na picha za watu na wanyama ni kipato haramu. Rejea katika hadithi zilizotolewa chini ya "Biashara haramu".
(v) Kipato chochote kutokana na umalaya, ngoma na muziki wa aina yoyote ni kipato haramu. Kama inavyobainika katika hadithi ifuatayo:
Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah ameharamisha kipato kutokana na mauzo ya mbwa, na kipato kutokana na kuimba kwa wasichana (singing girls) (Sharki Sunnat).
(vi) Kipato chochote kutokana na utabiri, ramli, na upigaji bao ni kipato haramu, na yote hayo ni kazi ya shetani katika Qur'an Allah (s.w.) ametuasa:
"Enyi mlikoamini! Bila shaka ulevi na kamari na kuabudiwa (kuombwa) asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kutazamia kwa mishare ya kupigia ramli (na kwa vinginevyo); (vyote haya) ni uchafu (na ni) katika kazi ya shetani. Basi jiepusheni navyo ili mpate kufaulu" (5:90)
Kutokana na aya hii upigaji ramli na utazamiaji wa aina yoyote ni haramu na kipato chake kitakachopatikana na kazi hiyo ni haramu pia. Utabiri wa aina yoyote ni haramu, hali kadhalika kipato kinachotokana na kazi hiyo ya utabiri ni haramu. Abu Bakar aliwahi kujitapisha baada ya kugundua kuwa amelishwa kutokana na malipo ya utabiri. Pia kipato kutokana na uchawi ni kipato haramu.
(vii) Hongo (Rushwa)
Utoaji na upokeaji wa rushwa ni haramu na pato lolote lililotokana na rushwa ni pato haramu. Mkoaji na mpokeaji wa rushwa wote wamelaaniwa na Allah na Mtume wake kama tunavyofahamishwa katika hadithi ifuatayo:
Abdullah bin Amr ameeleza kuwa Mtume wa Allah amemlaani mpokeaji rushwa na mtoaji rushwa katika kutoa hukumu. (Abu Daud, Ibn Majah).
Hongo au rushwa ni kiasi chochote anachopokea muhudumu (mfanyakazi) zaidi kuliko malipo yake ya haki katika kutoa huduma alizoajiriwa kwao. Kwa maana nyingine, mtu akipokea malipo yoyote, hata yawe madogo kiasi gani ambayo ni ziada ya mshahara wake katika kufanya kazi ile ile na katika kiwango kile kile cha kazi aliyoajiriwa kwayo, atakuwa amepokea rushwa. Turejee kwa makini hadithi ifuatayo:
Abu Humaid as-Sayyid ameeleza
Mtume (s.a.w.) alimteua mtu katika kabila la Azd aliyekuwa kiitwa Ibnul
Luthiyyah kama, mkusanyaji wa zakat, Aliporudi Madina, alisema: "Hii ni
kwa ajili yenu na hivi ni vyangu (nilivyopokea) kama zawadi Kisha Mtume
(s.a.w.) alitoa hutuba baada ya kumhimidi na kumtukuza Allah akasema: Jambo
lingine ni kwamba nimewateua baadhi ya watu miongoni mwenu kufanya (kuongoza)
shughuli ambazo Allah amenipa mamlaka kwazo. Mmoja wao anakuja na kusema:
'Hii ni kwa ajili yenu na hii ni zawadi iliyopewa. Kwa nini basi asibakie
katika nyumba ya baba yake au katika nyumba ya mama yake na kuona kuwa
angalipewa zawadi au hangelipewa? Kwa yule ambaye mikononi mwake uko uhai
wangu hapana yoyote atakayechukua kitu chochote kutokana na zakati awe
siku ya Kiyama hakutokea huku amebeba kitu hicho mabegani mwake. Kama alichukua
punda atakuwa analia humo begani; kama alichukua mbuzi atakuwa analia (mee
mee) humo begani. Kisha Mtume (s.a.w.) aliinua mikono yake mpaka tukaona
weupe wa makwapani na akasema: "Ee Allah! Nimefikisha ujumbe)? Ee Allah!
Nimefikisha ujumbe)?" (Bukhari na Muslim).
--
|
|