Hapo awali mtu aliyekamatwa vitani alikuwa akiitwa "mtumwa wa vita", katika miaka iliyofuatia akawa anaitwa "mateka wa vita" (war captive), na siku hizi anaitwa "mfungwa wa vita" (prisoner of war). Kilichobadilika ni majina tu lakini sifa inayowaunganisha wote hao ni kuwa hawana uhuru kama raia wengine.
Katika ukombozi wa watumwa njia pekee ambayo Uislamu haukuifunga ni ile ya mateka wa vita. Maadamu kuna vita na uadui, mateka wa vita hatakuwa huru. Hata hivyo hao mateka wawe wamepatikana katika vita vya halali kwa mujibuwa sheria ya Kiislamu, na siyo vita yoyote ile. Vita hivyo isiwe ya uchokozi, wala ya kutukuza utaifa au ya kujipanulia mipaka au ya kujipatia mateka, n.k.
Vita vya halali kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu ni kupigana na wavamizi au wakandamizaji ili kuondosha udhalimu. Hivyo basi watu watakaotekwa na Waislamu katika vita vya namna hii ni wachokozi, maadui na madhalimu. Hivyo haihalisi kabisa kusema kuwa watu hao wasikamatwe. Uislamu umelitazama suala hili kwa uwazi. Suala la msingi siyo kama adui huyo mateka wa vita atekwe au asitekwe, bali atendeweje akisha kamatwa. Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu hapo watu hao walikuwa ni wachokozi na maadui, maadamu sasa wamedhibitiwa basi wahurumiwe na wasifanhyiwe ukatili. Katika vita vya Badr kwa mfano wale waliotekwa walipewa na Waislamu chakula bora kabisa kilichoweza kupatikana. Kwa hakika makafiri wengi walishangazwa na kuvutiwa sana na ihsani waliyofanyiwa na wengi wao wakasilimu.
Katika mazingira ya karne ya saba, zama ambazo hazikuwa na magereza, njia ya pekee ya hakika ya kuwahifadhi mateka hao ilikuwa ni kuwaweka chini ya usimamizi wa baadhi ya watu walioshiriki katika vita. Utaratibu huo ulihakikisha kuwa mateka wanapata mahitaji yao ya lazima na jamii inabaki katika hali ya amani na usalama, angalau hadi mwisho wa uhasama.
Umateka haukukusudiwa uwe wa kudumu.
Pamoja na kuwe mateka walitendewa vizuri, Uislamu haukukusudia kuwa mateka hao wadumu katika hali hiyo ya kutokuwa huru, Mwenyezi Mungu ameagiza katika Qur'an:
Basi mnapokutana (vitani) na wale waliokufuru wapigeni katika shingo zao, (wafe mara moja) mpaka mkiwashinda sana, hapo wafungeni (hali ya kuwa ni mateka); tena wawacheni kwa ihsani (wende zao makwao) au kwa kujikomboa. (47:4).
Kwa mujibu wa aya hii mateka hao wangeweza kuwa huru ama kwa kujikomboa yaani "Fidaan" au kwa ihsani (Manna). Mateka aliweza kujikomboa kwa mojawapo ya njia tatu:
(i) Kwa kulipa kiasi fulani cha pesa.
(ii) Kubadilishana na mateka Waislamu waliokamatwa na adui, au
(iii) Kutakiwa afanye jambo fulani lenye manufaa kwa jamii ya Waislamu.
Baada ya vita vya Badr, kwa mfano Mtume (s.a.w.) aliwaambia mateka wa vita kuwa wangeweza kuachiwa huru kama wangewafundisha Waislamu kumi kusoma na kuandika. Hapana shaka yoyote kuwa mateka wa vita siku zote atachagua kuwa mwalimu kuliko kuwa mateka.
Njia ya pili ya ihsani ni kuwa mateka anaachiwa huru bila fidia yoyote wala sharti lolote. Njia hii pia litumiwa na Waislamu.
Masuria na mateka wa vita wanawake.
Mjakazi ni mtumwa mwanamke, na suria ni mjakazi aliyefanywa kuwa mke wa bwana wake. Usuria ulikuwapo tangu zama za kale na ulienea sana miongoni mwa Wayahudi. Hata baadhi ya Mitume wametajwa katika Biblia kuwa walikuwa na masuria kadhaa. Nabii Muhammad (s.a.w.) alipokuja aliikuta taasisi hiyo ya usuria na hatimaye kuuondosha moja kwa moja.
Zama hizo (kama ilivyo siku hizi) baadhi ya wanawake walikuwa wakienda katika midani ya vita ama kuwashangilia na kuwahamasisha askari wao au kuwahudumia majeruhi au yote mawili. Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu mwanamke aliyetekwa vitani anatendewa kama anavyotendewa mateka mwanaume - kwa ihsani na kuhurumiwa. Kwa mwanamke aliyetekwa katika uwanja wa vita huzuka tatizo jingine la ziada. Nalo ni kuwa kwa kawaida wanawake huwa wamo katika hatari kubwa sana ya kutendewa ukatili wa kunajisiwa kwa nguvu (rape) na askari wa jeshi lililoshinda. Hadi leo katika karne hii ya 20 katika kila vita inayopiganwa askari jeshi wakikutana na wanawake (hata kama siyo katika uwanja wa vita) huwaingilia kwa nguvu. Zaidi kuliko hivyo ni kuwa hata kama wanawake hao hawatanjisiwa lakini maadamu wametekwa na kama jeshi lao litashindwa basi wanawake hao huenda wakawa wamepoteza ndugu zao, baba zao na waume zao ambao ndio waliokuwa wakiwakimu na kusimamia mambo yao. Hivyo basi kwa upande mmoja inabidi hatua zichukuliwe kuwahifadhi wanawake hao na kunajisiwa na kwa upande mwingine inabidi kuihifadhi jamii na wao wenyewe pia na ufuska na umalaya. Matatizo ya kujitafutia riziki ugenini, bila ndugu wala msaada wowote kunaweza kuwasukumiza wanawake hao katika umalaya, jambo ambalo Uislamu umeliwekea adhabu kali sana.
Ili kulitanzua tatizo hilo zama hizo na wakati mwingine wowote litakapotokea Uislamu umeruhusu wanawake hao wachukuliwe na kuishi na wanaume waliokwenda vitani. Hatua hii huleta manufaa kadhaa. Kwanza uhusiano wao huwa ni ule wa ndoa. Suria kuhesabiwa kama mke wa hali zote. Tofauti pekee iliyopo baina yake na ndoa ya kawaida ni radhaa, yaani kukubali. Katika ndoa ya kawaida lazima ridhaa ya muolewaji ipatikane. Pili chini ya utaratibu huu hakuna haja ya magereza au makambi yakuwaweka mateka. Tatu utaratibu huu huondosha fitna ya ufuska na ukahaba. Kwa kumpata mtu mmoja wa kuishi naye kama mume, mateka huyo anakuwa amepata maskani ya kuishi, mahitajio yake ya kawaida na ya kimwili na anakuwa amehifadhika na hawezi kugunwa na mtu yoyote au kushambuliwa.
Kumiliki mali kwa mtu binafsi kwa jinsia yoyote inazingatia katika Uislamu, hata hivyo umiliki huo una ukomo.
Falsafa ya Uislamu juu ya maisha inamuona mwanadamu kama Khalifa wa Mwenyezi Mungu hapa duniani kwa hivyo mali atakayomiliki ni kwa dhamana tu siyo kwa hakika, na kwa sababu hiyo ataulizwa jinsi alivyoitumia hiyo mali "yake" na yule Mmilikaji wa hakika yaani Mwenyezi Mungu. Pamoja na hivyo Uislamu unaikubali na kuiheshemu haki ya mtu binafsi kumiliki mali.
Hata hivyo, mali hiyo itakayomilikiwa
iwe imechumwa kwa njia za halali Uislamu utaitambua mali ile ya halali
iliyo chumwa kwa njia ya halali. Vile vile katika utumiaji, mtu asiitumie
mali yake kiasi cha kuteta madhara kwa watu wengine au kwa jamii.
--
|
|